Siasa katika elimu au nini maana yake?

Kalinzi

Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
86
Reaction score
14
Wadau
vyuo vikuu kuna kozi zilizoanzishwa ambazo hufundisha masomo ya kufundishia kama vile biology, chemistry, physics , history na mengineyo. Tatizo la kozi hizi ni pamoja na changamoto za kutokuwa na mwelekeo baada ya kuhitimu kozi hizi. Watu huchaguliwa na kuchagua masomo hayo wengi wakiamini kuwa wanaenda kusomea ualimu lakini baada ya kufika huko huambiwa wao si waalimu bali ni wataalamu tu wa somo fulani na hawafundishwi masomo ya ualimu na hivyo kuongeza tatizo la ukosefu wa ajira mtaani.
Baada ya hapo najiuliza je mtaalamu wa kiswahili, biology, geography nk kwa tanzania hana kazi?
Kama tuna watu kama hawa seriikali haioni umuhimu wa kufuta tatizo la walimu katika shule zetu kwa kuwapa vipaumbele hawa na kuwaboreshea elimu yao?
Lengo la kuanzisha kozi hizi katika vyuo vikubwa kama udom, udsm nk ni sababu za kisiasa na malengo yake ni nini hasa?
karibuni wadau kwa mjadala
 
naogopa kusema kama ni siasa inaotumika kuanzisha koz mbalimbali vyuoni kwasababu kinachoangaliwa ni upana wa elimu kidunia, wataluma hawaangalii kwamba watz wanahtaji elimu gani, pamoja na hayo unapewa choice kuchagua koz unayoipenda hulazimishwi kwenda kusoma kozi fulan
 
HIVI UKISOMA DEGREE YA BIOLOGY WEWE UNAWEZA KUAJIRIWA KAMA DAKTALI? Ukisoma shahada ya physics wewe ni rubani? Kama sio basi hata ualimu ni profession kama tajwa hapo juu. Kusoma content kama kiswahili bila teaching methodologies inamanisha wewe ni mtaalamu wa hilo eneo lakini si mwalimu. Hakuna siasa hapa ni haki kabisa. HATA WAHADHIRI WALIPASWA WAPEWE KOZI YA POST GRADUATE DIPLOMA IN EDUCATION SIO KUFUNDISHA TU KWA KUWA ALIKUWA NA GPA KUBWA HAPANA. Ndio maana elimu inamomonyoka.
 
Vyuo viko kibiashara zaidi (kozi nying raia weng) na vijana wanaomaliza form six weng hawatafuti ushaur! Na ukishachaguliwa kozi fulan ndo bas USUMBUFU wa kubadilisha hawatak unless unahamia EDUCATION! La msing kuwen makin juu ya uchaguzi wa kp unatakisoma kabla ya kuapply.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…