Second hand
Member
- Jan 20, 2013
- 72
- 6
Jana nilimtembelea jirani yangu ambaye amehitimu hivi karibuni udom, shabaha ya kutembelea ilikuwa ni kupata 'machache' kuhusu udom kwasababu nami ni mwanagenzi mtarajiwa. Aliponiona tu akaniuliza kwa wahka: "we ni mwanachadema". Inawezekana alisema hivyo kwa sababu nilivaa shati la khaki ambalo linaendana na 'gwanda 'la chadema kwa kiasi kikubwa. Nikamjibu 'Ndiyo' , nilijibu hivyo ili nisikie anasema nini kuhusu kujihusisha na ukada {cdm} udom. "Siasa ziache huku huku nyumbani, ukienda chuoni na hizo harakati hautamaliza hata semister moja" alinambia Sijafika chuoni kushuudia lakini hili suala limekaa vipi? Katika nchi ambayo inasemekana inaongozwa katika misingi ya sheria na utawala bora ambayo inampa mtu: haki na uhuru wa kufungamana na kiitikadi na chama chochote.