Siasa na utaalamu: Wakili albert msando na conflict of interest

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Posts
1,334
Reaction score
1,466
Unaposhitakiwa mahakamani na swahiba wako inauma na inaashira kumaliza uswahiba na urafiki wenu. Adui anapotetewa na rafiki yako ili kukuangamiza akimtumia rafiki yako kwasababu anakujua vizuri wote wawili wanania ovu ya kuhakikisha unashindwa.

Ni nadra sana duniani rafiki yako au mwanasheria wa kampuni anapofanyakazi kumwakilisha mfanyakazi dhidi ya kampuni husika hiyo inaitwa conflicts of interest. pamoja na haki zote kisheria mtu ambaye anadai mahakamani anayo na ana haki ya kuwakilishwa vyema na wanasheria ila haitaacha makovu na kutukuaminika kama mwanasheria ama wa kampuni husika, taasisi au kiongozi kushirikiana na mtu mwenye nia ya kushitaki na kuwamsaidia kisheria dhidi ya kampuni husika.

Albert Msando aliungana na ZZK kabwe kuishatiki CDM. Kesi hii inatumia fedha za chama, muda wa chama na kusimamisha baadhi ya mambo muhimu kwa sababu ya uchu wa watu wachache.

Albert Msando ni mwanasheria mzuri ila haifai tena kuwekwa eneo lolote nyeti la chama kwani anaweza kukiangamiza chama. Sio vibaya yeye kuwatetea wateja wake, ila lazima ajue ana conflicts of interest na chama.

Kama yeye ni diwani wa chadema ambaye anategema wanachadema wamuunge mkono kwenye harakati zake za udiwani na Chama kimemwona ZZK ni msaliti wa chama amabye ana nia ovu ya kukiangamiza chama, na chama kupitia kamati kuu kimetangaza wazi ZZK asipewe ushirikiano wowote na kiongozi au mwanachama wa chadema kwa maswala yote ya chama! Je hii kauli kwanini isimhusu Msando moja kwa moja.

Ningependa huyu jamaa naye atangazwe stutas quo yake ndani ya chama. Wanachama wameitikia wito wa kumwona ZZK ni kirusi je wakili wake huyu ambaye zaidi ya kumtetea mahakamani ameonekana kwenye mitandao ya kijamii akikandia uongozi, akieneza chuki na kutangaza waziwazi kuwa maamuzi ya Kamati kuu hakubaliani nayo. Sasa yeye anatetea maamuzi ya chama gani?

Hii ni standard ya taasisi yeyote ile duniani iwe ni UN, Taasisi binafsi, chama cha siasa nk. Hatuwezi kuendelea kuishi na ndimi mbili. Kama chama kimeamua kupambana na virusi naomba kitoe maelekezo kuhusu huyu jamaa. Je yeye naye anahusika kwenye tamko la kamati kuu kuhusu kumtenga ZZK ama tamko lile linahusu wanachama wengine tu ? Je fedha anazolipwa si ndizo zile zilizotoka kwa akina Mwigulu?

Chief Mkwawa anapenda haki na usawa.
 
Haki bana inawezekana kabisa kwa standard zote zzk anaonewa na wahafidhina ambao kwa uwezo wao wamesambaza sumu unajua hao ndiyo mwisho wa siku ni wasaliti na inawezekana alberto msandao anawafahamu vizuri kwanini haisaliti nafsi yake ?
 
Huyu hafai hata kidogo. Namchukulia km adui mkubwa wa CDM na anastahili kupuuzwa kabisa.
 
Kwa hiyo mtu yeyote atakayemuunga mkono Zitto afukuzwe sio..!?! Demokrasia haiko hivyo. Acheni watu waonyeshe hisia zao.
 
Kwa hiyo mtu yeyote atakayemuunga mkono Zitto afukuzwe sio..!?! Demokrasia haiko hivyo. Acheni watu waonyeshe hisia zao.

Tunataka watu waoneshe hisia kwa waume au wake zao na sio kwa cdm. Mtu km zitto wa la hasimamishi halafu unajifanya ana hisia. Go away
 
kwa ushauri wako huu chama kitapoteza wanachama wengi. Vipi prof. Baregu naye afukuzwe?. Kwakuwa uko nje ya system ngoja nikuache. Ila ungejuwa ungesema hata slaa afukuzwe. Ila juwa kwamba sio kila aliyepinga maamuzi yale alijitokeza kwenye vyombo vya habari, kunawengine wanaonekana kuunga maamuzi hayo tu kwa afya ya chama kwa kuwa hili linaonekana nichama kimesimamia na siwatu flani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…