Letemzungu
New Member
- Aug 27, 2022
- 1
- 2
Siasa ni kitu chenye athari kubwa katika maisha yetu, ukiacha dini na fedha. Ni siasa ambayo inaweza ikampandisha au kumshusha mtu bila kujali uchumi na uwezo wake. Hata ukiwa kwenye sekta binafsi au hata asasi zisizo za kiserikali bado maamzi ya kisiasa yanakuhusu na pengine kukuathiri.
Wote ni mashuhuda kuna watu walifaidika na uwepo wa serikali ya awamu ya tano nchini Tanzania na kunawalioumia ikiwemo wafanyakazi hewa. Hivyo hivyo serikali ya awamu ya sita kuna waathirika wa aina mbalimbali na hiyo ndo inaitwa siasa hata usipojihusisha nayo, yenyewe itakuhusisha.
Hata hivyo msemo wa "siasa ni mchezo mchafu" umekuwa ukiwakatisha tamaa watu wengi kujihusisha na siasa hasa vijana wakiamini siasa ni za kikundi fulani tu au watu fulani. Uoga inawezekana ndio mchawi anayezima ndoto za watu wengi na wengine kuzikwa na mawazo yao mazuri badala kuyatumia na kuacha alama kwenye jamii kama akina Mwl Nyerere na Mandela.
Vijana wengi wanamitazamo yao kuhusu serikali za kiafrika jinsi zinavyoyaendea mambo ila wanaogopa kuwania viti vya kiasiasa vitakavyoweza kuwafikisha kwenye vyombo vya maamzi na kuleta mabadiliko. Bila shaka ni kwasababu ya matukio ya kikatili ambayo huwa tunayashuhudia wakati wa chaguzi mbalimbali, "kwani wanasema kaya ya muoga nayo ni kaya".
Swali la kujiuliza tutaogopa mpaka lini?, Usingekuwauthubutu wa wazee wetu leo Tanzania ingekuwa huru?. Wanasema moja ya changamoto ambayo dunia inaweza kuwa inapitia ni watu wenye uwezo wa kuongoza kutojihusisha na siasa na badala yake watu wasiokuwa na uwezo ndo wanashikilia hatamu. Hali ambayo inapelekea lawama kuwa nyingi juu ya viongozi katika nafasi mbalimbali.
Kama vijana yatupasa kuichangamkia siasa ili kuleta changamoto na fikra mpya. Tukiwa kama jeshi kubwa tunatakiwa kuwa msitari wa mbele kadiri ya utashi watu katika ulingo wa siasa ili kuleta maamzi yanayofaidisha.
Ni rahisi kuona vijana wanalalamikia mfumo wa uongozi katika serikali na katika vyama kuwa ni wa kurithishana baina ya koo ama kanda huku kukiwa na mchanganyiko kidogo wa watu baki. Kwa mtazamo wa haraka haraka inaonekana ni ukweli licha ya watu wengi kuwa na uwezo mkubwa wa kuongoza Ila watoto wa shangazi ni kama wanapendelewa. Je, ni nani alaumiwe katika hili?.ni mamlaka za uteuzi ama vijana ambao hawataki kujihusisha.
Ukweli ni kwamba tupo kwenye ulimwengu wa ushindani, ambao pamoja na kuwa na uwezo pia, unatakiwa kuwa na hususiano chanya na mamlaka. Uhusiano ambao utakutambulisha uwezo wako na uthubutu wako.
Bila shaka hapo ndio huwa tunafeli vijana tuliowengi na kuishia kulalamika tu. Tumuombe mungu atusaidie tuwe na ujasiri na uthubutu kwa maana kutokutaka kujihusisha na siasa haimaanidhi haitakuhusu.

Upvote
3