SoC02 Siasa na wasomi imegeuka dili ndani ya dili

SoC02 Siasa na wasomi imegeuka dili ndani ya dili

Stories of Change - 2022 Competition

Bosi Kalewa

Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
7
Reaction score
4
Dili kubwa Afrika na Tanzania ikiwemo, ni siasa. Wahadhiri na wasomi wanatoweka vyuoni kama sauti za tausi pale Ikulu. Wanajiingiza kwenye siasa na harakati za kipuuzi kwa mgongo wa demokrasia. Wamechoka kuchakaa kwa vumbi la chaki.

Badala ya kufundisha watoto vyuo vikuu. Wameacha kusaidia kama taifa tujikuamue. Wanatumia uwezo wa akili zao kuwaandikia wazungu 'maandiko' ha kuomba mamilioni. Wakipewa wanaenda kwa masikini na mapoyoyo kuuliza nani maarufu kati ya Lissu na Zitto.

Umaarufu wao unamsaidia nini mama yangu kijijini? Asiyejua utamu wa maji safi tangu taifa hili liundwe na kina Nyerere na wenzake? Wanapewa mabilioni ya pesa wanayatumia kwa maswali ya kijinga kwa mtu ambaye hajui hata zahanati inafanaje?

Na sisi watoto wa mjini tunachekelea kuambiwa na hawa wasomi wahuni, kuwa Lissu maarufu kuliko Zitto. Wasomi hawatumii usomi kutusaidia. Ukiuliza, eti demokrasia. Lakini ukizama ndani zaidi unagundua suala hapa ni pesa.

Wanasiasa wanapiga kelele jukwaani ili wapate ajira kwa mgongo wa kutetea maslahi ya Taifa. Na wahuni hujificha kwenye kivuli cha usomi wanaendesha harakati za kihuni ili wapate pesa za wazungu. Afrika tunaangamizwa na watu walioelimika kuliko wasioelimika.

Mtu anaanzisha tasisi ya kutetea haki za binadamu. Lakini shughuli zake hazina tofauti na za Ufipa na Lumumba. Ukweli ni kwamba wanasiasa na wasomi wa Afrika, wanatumia matatizo ya watu kujineemesha tu. Hawana chembe ya uzalendo wala uchungu.

Demokrasia imeletwa kama dini zilivyoletwa toka magharibi ma mashariki. Tunaambiwa dini imekuwa biashara. Hata demokrasia ni biashara pia. Tukitaka kusonga tuwapuuze wanasiasa na wanaharakati wachumia tumbo. Huhitaji msaada wa FBI kuwajua wachumia tumbo. Maana wako wazi kama vazi la kahaba.
 
Upvote 2
Hakika, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom