OMARI KITOMARI
Member
- Sep 12, 2021
- 6
- 10
1. UTANGULIZI
Awali ya yote naomba kuwashukuru Jamii Forums kuandaa hii story of changes kwa wale watakao shiriki kila mmoja atakuwa na mtazamo wake ivyo itawapelekea jamii forum kupata mawazo mengi zaidi lakini wametoa fursa kwa watu mbalimbali kushiriki na watakao shinda basi kile watakachopata kitawaamasisha kuendelea kuwa rafiki wa mitandao na watashukuru kuwa mtandaoni lakini kwa manufaa zaidi ivyo wanaweza kuwa chachu kwa watumiaji wengine.
2. MADA
Nimeona niizungumzie siasa kama sura inayoweza kubadili maisha ya watu kulingana na kwamba ndio msingi dira ya maendeleo maana kila jambo lolote linalo wahusu wananchi utakuta linasimamiwa na siasa kwa maana ya kwamba kila sekta ambayo watu mbalimbali uenda kupata huduma utakuta inasimamiwa na wizara yoyote na wizara inaongozwa na katiba sheria na kanuni mbalimbali hivyo siasa ikiamua jambo hata kama sheria yake haipo litatungiwa sheria na itaanza kutumika pale tu itakapokuwa imepitishwa na bunge ambao ndio uwanja wa siasa kisha rais aliyeko madarakani ambae ndie refarii wa siasa akiisaini tayari imepita na kuanza kufanya kazi ivyo ndivyo nguvu ya siasa inavyofanya kazi kwa watu wake ndio maana nikaiita sura maana ikiamua jambo hakuna wakuishinda
3. NGUVU YA SIASA
Hapa naomba nioneshe nguvu ya siasa na nitachukua mambo machache yaliyoanzishwa na siasa na yalivyoleta tija mbalimbali kwa mfano tulikuwa hatuna TRA lakini siasa ilianzisha na mpaka sasa maendeleo mengi yanategemea makusanyo ya kodi itokanayo na shughuli mbalimbali zinazofanywa na watu sheria yake ilipitishwa bungeni kwenye serikali ya awamu ya tatu mpaka leo hakuna asieijua TRA.
Jingine katibampya walitokea wanasiasa wakaanza kudai katibampya kipindi cha awamu ya nne kwa kutumia nguvu ya siasa kila mtanzania alijua na maoni yakakusanywa hatimae bunge la katiba na rasimu ikapatikana mpaka leo ipo na imetokana na siasa ivyo siasa ikiamua jambo linawezekana maana rais wa nchi ndio mwanasiasa namba moja hata kama atakuwa hayuko kwenye siasa sana kitaaluma maadamu ni kiongozi mkuu wa nchi lazima atokane na chama cha siasa kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria zetu.
Jengine tumeona siasa ilivyopitisha sheria ya uharifu mitandaoni kuna baadhi ya watu wamefungwa na kulipa faini kwa sheria hii wapo waliopatwa na tuhuma mbalimbali za uchochezi hasa kwa kuandika maandiko yalioikosoa serikali maana walivunja sheria kwa kupost maudhui ambayo yalionekana ni kinyume na sheria hiyo ya mitandao ya kijamii iliyotungwa awamu ya tano na wananchi walianza kuwa waoga kupost maudhui kama hayo ambayo wengine walitiwa hatiani ivyo nguvu ya siasa ikashinda na sheria ipo mpaka leo pamoja na wanaharakati mbalimbali kuisema vibaya pamoja na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu kuipigia kelele lakini siasa ilishinda sheria ipo mpaka leo inatumika na kuwatia hatiani watu mbalimbali wanaoikosea.
Hii ni pamoja na sheria ya madini nayo ilikuja kuangalia upya mikataba ya madini hasa baada ya Rais wa awamu ya tano kubaini mapungufu kwenye mikataba ya madini na akabainisha hasara ambazo tumekwisha pata watanzania kutokana na mikataba pamoja na sheria zilizokuwepo tukalazimika kutunga sheria mpya inayotumika mpaka leo kwenye madini na wakati wa vuguvugu ilo kila mtu aliona na alijua kinachoendelea kwa sababu lilikamatwa na siasa yapo mambo mengi yenye tija ambayo siasa imeyasimamia na mpaka leo tunanufaika nayo ndio maana nikasema sura hii ya siasa ikitumika vizuri inaweza kubadili maisha ya watu wake.
4. NJIA ZINZOWEZA KUTUMIKA
Kwanza ifahamike kuwa ukiachilia mbali utawala wa Mwenyezi MUNGU mamlaka hizi zinazotokana na siasa zimekuwa zikiwaambia wananchi wake zitabadili maisha yao na kuwaletea maendeleo mbalimbali kwa kutumia vyanzo vya mapato ambavyo mamlaka hizi zinaanzisha lakini wamekuwa wakitoa ushauri mwingi kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana kama kufanya biashara mitandaoni ndio maana tunaona biashara nyingi mitandaoni lakini bado mamlaka ikaendelea kutenga pesa kwenye halmashauri zote nchini ambazo ni asilimia 10% ili vijana na wanawake na wale wenye ulemavu kukopa bila riba ili kujiletea maendeleo pamoja na hilo
Bado nguvu ya siasa hapa haikutumika sana maana toka limeanzishwa mpaka leo tungeona wahusika wakinufaika asilimia japo 90% na tungeona maendeleo yao kwa haraka na tusingekuwa na watu wenye muda wa kupoteza hasa kufanya vitendo visivyofaa kwenye jamii kama matumizi ya mihadarati na mambo mengine yanayofanana na hayo lakini tusingekuwa na kundi kubwa la dada zetu wanaouza utu wao kwa thamani kidogo sana na kuambulia kupata maradhi mbalimbali
Lakini tusingekuwa na watoto wa mtaani maana tungekuwa tumeona watoto hawa wanaokimbia ugumu wa maisha huko kwenye familia zao hawatoki huko maana huwezi kukuta mtoto wa tajiri mtaani hata wakiwemo ni wachache sana tofauti na masikini
Tumekuwa na wazee ambao wamekosa huduma huko majumbani na kukimbilia kwenye vituo vya kulelea wazee hivyo hilo siasa ingeliangalia kwa jicho kubwa zaidi na kuweka mkazo kwa kuwa na uwajibikaji mkubwa kama ilivyo kwanye maeneo mengine leo hii maisha ya watu yangekuwa yamebadilika sana sasa sura ya siasa ikisema hatuitaji watu wasiofanya kazi
Tunahitaji watu wanaojishughurisha yote yangewezekana maana kungekuwa na mkazo unaoshurutisha watu kujua fursa zooooote zinazopatikana na kwa utaratibu upi na watu kuziendea na maendeleo yangepatikana kwa kasi zaidi ukienda kwenye upande wa kilimo asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima kwa mujibu wa takwimu za serikali asilimia 70% ya watanzania wanafanya kilimo hivyo sura hii ya siasa ingewaangalia zaidi wakulima wa chini sana ambao wanatumia jembe la mkono na wakafanya kilimo cha msimu tu na kuvuna mazao kidogo na kukosa manufaa kwenye kilimo basi tungehakikisha tunatoa trekta kila kitongoji ili tuhakikishe tunafanya kilimo lakini wataalamu kila serikali ya kijiji ili watumike kushauri njia nzuri ya kufanya kilimo ikiambatana na upatikanaji wa pembejeo n.k.
Sasa watu hawaendelei maana siasa haijaamua kwa vitendo kama nilivyoonesha huko nyuma jinsi siasa ilivyotumika kuleta tija kwenye baadhi ya mambo bali nadharia kwenye maeneo kama hayo niliyoyataja kwenye namba nne.
5. HITIMISHO:
Asilimia kubwa ya viongozi wengi wanaoshika dora wanatokana na siasa sura hii ya siasa inayotazamwa na wananchi kama dira ya maendeleo kwao inaweza kuchochea maendeleo kwa watu wake kama nilivyoonesha kwenye andiko langu nashauri wananchi wasitegemee kupata maendeleo hivi karibuni kwa kutegemea siasa maana kuna maeneo wanaweka mkazo na mazingira yanakuwa rahisi kupata unachohitaji kuna maeneo mengine mkazo unakuwa kidogo sana hivyo tusibweteke tuongeze bidii kwenye kutambua nini tunahitaji na kuhakikisha unakipigania kwa nguvu zote lakini tutumie mitandao ya kijamii vizuri kwa kuingia kwenye darasa mbalimbali zenye tija na malengo yetu lakini tusikubali kuishi bila malengo maana tutajipoteza kwa kuamini hilo vitu vyote vinavyochangia kupatikana maendeleo havitoki mbinguni tunatengeneza sisi watu kwa nini vinapatikana kwa gharama kubwa maana yake hakuna utashi wa kisiasa duniani kwa watu wao.
Asante sana jamii forums haya ni mawazo mbalimbali ambayo tumeyatoa kupitia ninyi tunawatakia kila lakheri najua mtakuja na mengi zaidi naombeni ushirikiano wenu.

Upvote
1