masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
Kati ya vitu ambavyo tutamkumbuka Mwalimu Nyerere ni ule u thinker wake. Mwalimu si tu alikuwa na maono ya kisiasa, lakini kiuongozi alikuwa kama mcheza chess. Mwalimu alikuwa na uwezo wa kufikiria mbele madhara au manufaa ya kile alichokuwa ana panga au kukipigia debe kisiasa.
Na ndio maana alipotaka kung'atuka 1980 katika uongozi, wanufaika wa uongozi wake walimsihi asubiri hadi 1985. Aliona giza lililotanda kiuongozi baada ya 1980 na miaka inyofuata. Vuguvugu la kukaribisha siasa za ushindania liziona. Lakini Mwalimu hatutamsahau kwa mipangilio yake kisiasa katika kudadavua siasa na sera.
Mwalimu aliweka msingi wa kisiasa na maendeleo na kusema kuwa, ili tuendelee twahitaji vitu vinne:
- -Watu
- -Ardhi
- -Siasa safi
- -Uongozi bora.
Awamu ya pili, tatu, nne na tano kila moja zimejaribu kudadavua misingi hiyo ya Mwalimu kwa kauli mbiu nyingi za kisiasa.
- Mzee Mwinyi - Ruksa kwa maana ya kufungua uchumi.
- Mzee Mkapa - Ukweli na Uwazi kwa maana ya kuwa na serikali sikivu na makini
- Mzee Kikwete - Ari mpya, Ngugvu mpya, Kasi mpya kwa maana ya kuuinua uchumi
- Mzee Magufuli - Hapa kazi tu kwa maana liwe na liwalo kazi zitafanyika kama ilivyopangwa
Tunapoelekea kwenye kampeni 2025, inabidi CCM wajue wazi $R maana yake nini haswa. Matamko na kauli za Nape na yule DC mstaafu wa Longido, zimeustusha umma wa kitanzania kuwa CCM sasa hakuna common unifying Ideaology. Chama kimekosa dira hata kwa kiwango cha viongozi.
Tunajua mazingira ya Mwalimu kiuongozi siyo kama ya sasa, lakini misingi ninile ile ya kisiasa yaani maendeleo bado yanahitaji vitu vinne, watu, ardhi, siasa safi na viongozi bora.