Siasa ya Tz na shule nyingi

Siasa ya Tz na shule nyingi

falsafa hai

New Member
Joined
Feb 19, 2013
Posts
4
Reaction score
0
Ni ukweli usiofichika kuwa siasa za nchi hii zinatupeleka pabaya hasa baada ya kuzizidisha hata kwenye mambo ya msingi na ya kitaaluma. Hivi serikali hii na sera zao za bora shule nyingi zitatimiza ndoto ya watanzania kuwa nchi yenye neema na kujiweza? Anguko hili la kitaaluma linaathiri haswa familia masikini ambazo zilitarajia japo mtoto wao mmoja naye siku moja atakuwa wakupigiwa upatu kwa kuwa kinara kitaaluma. Lakini ndoto hizi huzimwa na vishule vilivyo zunguka vijiji na kata na kuendeleza kuzima ndoto za watanzania. Hakika shule nyingi kwa sasa wanafunzi wanahudhuria tu na hawajifunzi kitu. Katika saikolojia ya elimu si kweli kwamba darasa la wanafunzi 100 wote hawana uwezo wa kupata 50% ya alama za mtihani baada ya kufundishwa kwa usahihi katika mazingira sahihi na mwalimu sahihi. Je uozo huu unatoka wapi??? Wataalamu, wanasiasa na serikali tumeacha kuitamani Tanzania bora ya kesho na zaidi tunatamani mishahara, posho na vyeo. Napenda kuwakumbusha kuwa kamwe hamtakuwa salama kwa kuwanyima watanzania wenzenu fursa ya maisha bora wayatakayo kwa kuwanyima elimu au kuwapa kiini macho cha elimu isiyo na kiwango kwa kuwa kesho watagundua hiyo janja ya nyani na watawageukia kuwadai.
Napenda kuwashauri kuwa ni bora kila wilaya iwe na shule nne bora kuliko kuwa na utitiri huu unaojenga bomu la kutulipua wenyewe.
Najua ni kawaida ya watu wengi kudharau maneno ya namna hii, lakini ile dakika ya kudaiwa ikifika watu hao huwa wapole sana lakini hakuna tena njia ya kurekebisha.
Wadau nawauliza HIVI KWELI SIASA YA NCHI HII INACHAKUJITETEA KATIKA PIGO KUBWA LA KUFELI WANAFUNZI NAMNA HII?? :nono: Sote kwa pamoja tutafakari na kuchukua hatua sahihi sasa.
 
Back
Top Bottom