Siasa za Katiba: Tujiulize, Katiba Tiba ya Maadili Yetu? By January Makamba

Siasa za Katiba: Tujiulize, Katiba Tiba ya Maadili Yetu? By January Makamba

Selemani

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2006
Posts
947
Reaction score
294
Tujiulize, Katiba tiba ya maadili yetu?


Na January Makamba

Posted Jumatatu,Oktoba14 2013 saa 12:54 PM. Tujiulize, Katiba tiba ya maadili yetu? - Habari - mwananchi.co.tz


Mwaka 1986, nikiwa na umri wa miaka 12, nilipanga mstari nje ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga nikiwa sehemu ya wananchi wengi waliofurika kwenye ofisi hiyo, majira ya jioni.

Wote tulikuwa tukisubiri ugeni mkubwa uliongia kwenye mji wetu mdogo wa Lushoto. Wakati giza linakaribia kuingia, mgeni wetu akaingia na msafara mdogo, akateremka akiwa ameshika fimbo mkononi. Mwili ukanisisimka!

Ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kumwona Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa karibu.

Msisimko ule ulibaki nami kuanzia siku ile na nikapata hamu ya kumfahamu zaidi. Taswira niliyopata ni kwamba alikuwa mtu wa ajabu, mtu mwenye sifa za ziada.

Kadri miaka ilivyokuwa inaenda, taswira sahihi ya Mwalimu iliibuka: Kwamba ni kweli alikuwa mtu wa ajabu kwa maana ya kwamba aliijenga nchi yetu katika taswira yake, kwamba alijulikana na kuheshimika dunia nzima.

Kwamba, aliwapenda watu wake, lakini hakuwa malaika kwani alifanya makosa na hakufanikiwa katika yote aliyotaka yatokee.

Pia, kwamba miujiza ya kifimbo haikuwa ya kweli, bali tuliamini na kuaminishwa hivyo kwa sababu sisi wenyewe tulitaka kumweka juu ya uwezo wa binadamu wa kawaida.

Takriban asilimia 68 ya Watanzania wamezaliwa baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka madarakani na pengine asilimia 44 baada ya kuwa ameshafariki dunia. Hata hivyo, kwetu sote bado yu hai, siyo kwa sababu tunaona picha zake, bali kwa sababu kwa kila jema tunalotaka kulitengeneza tunamtaja na kwa kila baya tunalotaka kulikemea pia tunamtaja.

Kwa sasa tunatengeneza Katiba Mpya ya Tanzania, lakini sijasikia sana tukimtaja Mwalimu na kukumbuka wasia wake wakati huu tunapojadili jambo hili kubwa.

Ningependa nitumie fursa hii kuukumbuka wosia wa Mwalimu ili utuongoze kwenye jambo hili adhimu. Wakati wa uhai wake, Tanzania ilitengeneza Katiba Mpya tano; 1961, 1962, 1964, 1965 na 1977 - na Zanzibar mara mbili na kufanya mabadiliko kwenye Katiba ya sasa (ya mwaka 1977) mara 13.

Mabadiliko yote haya yalikuwa ni katika jitihada za kuijenga Tanzania njema zaidi – kama ilivyo dhamira ya Rais Jakaya Kikwete alipoanzisha mchakato huu wa sasa. Katika nyakati zote hizi, Mwalimu alisema mambo kadhaa ambayo yanaweza kutuongoza kwa sasa.

Nataka niwakumbushe hotuba yake ya Juni 28, 1962 ndani ya bunge akijadili pendekezo la Serikali la kuunda Jamhuri ya Tanganyika, ambapo mezani kulikuwa na rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Tanganyika.

Mwalimu alieleza kwamba ulinzi wa haki za wananchi, ulinzi wa uhuru wa wananchi, ulinzi wa urithi wa taifa, ulinzi wa thamani ya mtu na vitu wanavyovithamini, haupatikani kwenye Katiba, bali kwenye misingi na maadili ya taifa (national ethics).

Katiba haizuii vitu viovu kufanyika, bali maadili ya taifa ndiyo msingi wa makatazo yote-kwamba makatazo ya mambo maovu yaanzie ndani ya damu na nyoyo zetu, ndani ya asili yetu, kwamba ifike pahala kwamba jambo hili au lile Watanzania wasikubali lifanyike siyo tu kwa sababu limeorodheshwa kama katazo kwenye Katiba bali kwa sababu siyo asili ya Utanzania, siyo sehemu ya maadili yetu.

Mjadala wa sasa wa Katiba Mpya umejikita zaidi kwenye kuorodhesha makatazo yanayopaswa kuingia kwenye Katiba, kana kwamba Katiba ndiyo itaunda hulka, utashi na maadili.

Hulka ya uchapakazi hailetwi na Katiba, hulka ya udokozi haiponywi na Katiba – bali na maadili ya kitaifa. Binafsi, naamini kwamba tuwe na mjadala wa aina hii na mjadala wa aina hii hauanzii kwenye majukwaa ya siasa, bali ndani ya familia.

Tujiulize, vijana wa sasa au wazee wa sasa, wanaishi kama alivyoishi yeye? Kilele cha mafanikio ya mwanadamu yeyote ni kuendelea kuwa hai mara baada ya kufariki – kwa kuacha kumbukumbu ya mambo mema ambayo hayafutiki wala kusahaulika, kwa Kiingereza wanasema ‘immortality'.

Kupitia uongozi wake, wosia wake, maandiko yake, lakini hasa kwa kuitazama taswira ya Tanzania, Mwalimu bado yu hai. Uamuzi wa kumuua utakuwa wa kwetu sisi wenyewe tuliobaki.

January Makamba ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
 
Katiba haizuii vitu viovu kufanyika, bali maadili ya taifa ndiyo msingi wa makatazo yote-kwamba makatazo ya mambo maovu yaanzie ndani ya damu na nyoyo zetu, ndani ya asili yetu, kwamba ifike pahala kwamba jambo hili au lile Watanzania wasikubali lifanyike siyo tu kwa sababu limeorodheshwa kama katazo kwenye Katiba bali kwa sababu siyo asili ya Utanzania, siyo sehemu ya maadili yetu.
Uzuri wake yetu ilikuwa inalazimisha maadili kwenye katiba na haki za raia zisiminywe kwenye huduma zinazotolewa na taasisi au mashirika ya serikali. Leo hii baadhi ya haki hizo tulizonazo; wanasiasa wa mlengo wa kushoto na taasisi zenye kupigania haki za ubinadamu kwenye dunia ya kwanza ndio wanapigana ziwekewe sheria hata kwa unusu ukilinganisha na haki alizopewa mtanzania.

Viongozi na baadhi ya taasisi za serikali zinaweza kuwa zilikuwa azieshimu taratibu za sheria zetu, lakini haki hizo zilikuwepo na kuweza kuwapa nguvu wanaharakati hata mahakamani kwenye kumtetea mtanzania, leo hizi haki zikipotea kwakweli wahusika wa kudai katiba mpya shurti warudi vijijini kuwaomba mshamaha watanzania. Haki za mtanzania na maadili yaliyo sisitizwa kwenye kujitazama kama jamii ni rare kwenye katiba yeyote duniani mungu asaidie watu waachiwe nafasi za utu wao.
 
Tangu mlipotuletea huu ujinga wenu wa Kodi ya Laini za Simu nimekushusha mno Makamba na haitatokea nikae nikuamini tena kwani wote ndio wale wale tu.Hapa kama ilivyo kawaida yenu CCM mnatujoki tu hapa hakuna hata jambo moja mnaloliongea likatoka mioyoni mwenu na mkalisimamia.CCM na UNAFIKI ni kama SAMAKI na MAJI vile.
 
huyu makamba si ni uleule uzao wa panya? ni mchumia tumbo tu hana lolote.
 
Ni kweli katiba haiweza kujibu maswali yote kuhusu maadili ya watanzania juu ya taifa lao, lakini pia uwepo wa katiba nzuri ni jambo muhimu kurejesha baadhi ya mambo ambayo yamekosa mwelekeo kwa wanajamii. mahali popote penye maadili mema pana utaratibu mzuri uliopangiliwa na wenyeji wa mahali hapo wanaridhia na kukubaliana na utaratibu huo, kwa maana nyingine panasheria zinazowabana wafuate kile kinachotakikana na jamii. wengi wanapendi kurudi miaka ya wazee wetu kwa kusema enzi hizo jammi iliuwa na madili bora kuliko sasa lakini wanasahau kuangalia taratibu zao zilivyokuwa. Chukulia mpangilio wa jamii ya kimasai na jinsi wanavyolinda mila,tamaduni na maadili ya jamii yao , asiye jua anaweza akafikiri vinatokea kirahisi lakini sio kweli, upo utaratibu unaowaunganisha pampja na wote wanakubaliana nao na ndio maana wanaufuata haijalishi umeandika kama tunavyoandika katiba au umendikwa kwenye mioyo yao.

Ni navyoamini katiba ni kipande kimoja cha utaratibu tena kipande muhimu, lakini vipande vingine vinatakiwa kuwepo toka ngazi ya familia hadi taifa kupata watu bora walio tiyari kule maendeleo kwa umoja. sipendi watu washushe thamani ya utengenezaji wa katiba bora kwa kudhani maadili yatajengwa na vipande vingine vilivyo baki, si nadharia nzuri kwani katiba inao umuhimu mkubwa kuunganisha jamii tokea ngazi za familia na kutengeneza taifa hivyo ni muhimu makubaliano ya wazi yakafanyika kuongeza umiliki na utayari wa kutawalio nayo.

Na inapofika maadili yamepolomoka sana kama ilivyo Tanzania sheria nzuri iwe katiba, miongozo mingine, mila na desturi zinazo simamiwa vizuri ni njia nzuri ya kurejesha maadili, kwa maana nyingine hatakama utatengeneza miundo mbinu mizuri ya kurejesha maadili ya jamii toka familia hadi taifa bila wasimamizi bora jamii kama ya watanzania ambayo imeanza kuzoea kujitanua bila kujali engine haiwezi kusaidia chochote.

Kunaswali lingine muhimu kujiuliza, wengi tunaafiki maadili yalikuwa bora zaidi enzi za mababu kuliko sasa, jambo amabalo hata mimi naamini, je yalihalibikia wapi? ni kwenye ngazi ya familia au kwenye jamii?. majibu ya hapo ndiyo yatatoa picha wapi pakutia mkazo kuweka miundombini ya kurekebisha uharibifu ulipo tokea tusonge mbele.
 
Back
Top Bottom