aliisaac1000
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 407
- 272
Siasa bwana!! Ila nimeona Tanzania watu wengi elimu ya kupambanua mambo ama ni ndogo kutokana na kiwango Cha elimu au kusudi kutokana na kukumbatia udini au ukabila, na hili lisipoangaliwa litakua janga la taifa letu, mfano mi si mshabiki ila kwa utafiti wangu nimeona wachaga wengi ni chadema, naona ni wapare tu ndio wamejitenganisha, je huu ni ukabila, ujinga au vyote? Na kama nchi hii itaenda kwa mtindo huu si ndio nchi itaenda kumwagika vipande vipande kama unguja na pemba,! Lowassa kaenda cdm nasikia na waarusha nao wanamfuata! Act kigoma, Ningeelewa zaidi kama wangekuwa ni wa jimboni kwake tu ! Ni kitu gani kimelikumba hili taifa, naona tunaelekea kama wenzetu kenya! Bila kujijua, taratibu! Tufanyeje ili tulinusuru taifa letu na mwendo huu?