muqawama
Member
- Jun 21, 2010
- 41
- 183
KWENYE SIASA ZA MAREKANI: JE UNAJUA MAANA YA SERIKALI KUFUNGWA (Government Shutdown) ?
🔍 Swali 1: Nini maana ya Serikali kufungiwa?
Jibu: Siasa za Marekani, Serikali kufungwa hutokea pale mambo mawili yanapotokea. Bunge la Kongress linaposhindwa kupasisha mswada wa Matumizi ya serikali shirikisho (Federal government) au Wakala wake. AU Raisi anapokataa kutia saini mswada kama hiyo uliopitishwa na bunge la Kongress
🔍 Swali 2. Nini hutokea Serikali ikifungwa;
Jibu: Wafanyakazi wasio muhimu hupewa likizo isiyo na malipo, na baadhi ya huduma za serikali zisizo za lazima husitishwa. Wafanyakazi muhimu na hutakiwa kuendelea na kazi bila Malipo mpaka serikali ifunguliwe
🔍 Swali 3. Ni muda gani Serikali hufugiwa?
Jibu: Kwa kawaida hakuna muda maalumu itategemea kupasishwa kwa Mswada husika na Bunge au na Raisi
🔍 Swali 4: Je ni muda gani mrefu kabisa Serikali imewahi kufungwa?
Jibu: Mwaka 1995 na 1996 wakati wa utawala wa Raisi Bill Clinton serikali ilifungwa kwa vipindi viwili kuanzia Novemba 14 mpaka Novemba 19, 1995 (kwa siku tano) na kutoka Decemba 16, 1995 mpaka Januari 6, 1996 (kwa muda wa siku 21). Mwaka 2018–2019 wakati huu wa Raisi Donald trump, Serikali ilifungwa Disemba 22, 2018 na ufungwaji bado unaendelea mpaka leo na haijulikani lini serikali itafunguliwa. Sababu kuu ya kufungwa kwa Serikali kipindi hiki cha Trump ni Bunge la Kongress kushindwa kupitisha makadirio ya Bajeti ya Dola za kimarekani billion 5.7 anazozitaka Raisi Trump kujenga uzio wa kuzuia wahamiaji haramu kutoka mexico.
🔍 Swali 5. Je ni watu wengi kiasi gani huathirika na tatizo hili?
Jibu: Mwaka 1995 na 1996 wakati wa utawala wa Raisi Bill Clinton serikali ilifungwa kwa vipindi viwi (kwa siku tano) za mwanzo watu wapatao 800,000 walipewa likizo bila malipo na kipindi cha pili kwa 21 Watu 284,000 walilazimishwa likizo bila malipo na 475,000 walilazimishwa kufanya kazi bila kulipwa mshahara. Kipindi hiki cha Raisi Donald Trump mpaka leo inakadiri Idara tisa kati ya 15 ya Serikali ya shirikisho, pamoja na mashirika na Miradi ya shirikisho, imefungwa au kupunguza huduma. Takriban wafanyakazi 800,000 wa Serikali ya shirikisho wameathirika, ama kwa sababu wameagizwa kwenda nyumbani bila kulipa au kwa sababu wanafanya kazi lakini hawajapata malipo wakati huu serikali ikiwa imefungiwa.
🔍 Swali 6: Je Taifa la Marekani linapata hasara kwa Serikali kufungiwa?
Jibu: Nyakati zote gharama ya kufungia Serikali imekuwa na hasara kubwa kuliko thamani ya Muswada uliokuwa unabishaniwa. Mfano Serikali ilipofungiwa Oktoba 2013, ambayo ilidumu 16, watafiti walikadiria kuwa Kufungwa huko kulisababisha hasara ya kupungua kwa ukuaji halisi wa Pato la Taifa kwa asilimia 0.2% hadi 0.6%. hii ikimaanisha kupotea kwa pato la serikali kati ya dola bilioni 2 na dola bilioni 6.
🔍 Swali 7: Mpaka kufikia leo serikali ya Marekani imewahi kufungiwa mara ngapi?
Jibu: Mpaka kufikia leo kumekuwa na Ufungwaji wa Serikali kwa mara Ishiri na moja (21) tangu mwaka 1976 kama ifuatavyo;
📚 Rejea :
1) Here Are All 21 Government Shutdowns in U.S. History Since 1976
2) Rand Paul rightly says the government shutdown was more expensive than keeping it open
3) Government shutdowns in the United States - Wikipedia

- 2018 (Raisi Donald Trump): Dec. 22 to (Unaendelea mpaka leo)
- 2018 (Raisi Donald Trump): Jan. 20 to Jan. 23 - (Siku 3)
- 2018 (Raisi Trump): Februari 9 – (Siku 1)
- 2013 (Raisi Barack Obama): Octoba 1 to Octoba. 17 - (Siku16)
- 1995-1996 (Raisi Bill Clinton): Disemba 5, 1995, to Januari 6, 1996, - (Siku 21)
- 1995 (Raisi Bill Clinton): Novemba 13 to 19 - (Siku 5)
- 1990 (Raisi George H.W. Bush): Oktoba 5 to 9 - (Siku 3)
- 1987 (Raisi Ronald Reagan): Disemba 18 to Disemba 20 - (Siku 1)
- 1986 (Raisi Ronald Reagan): Oktoba 16 to Oktoba 18 - (Siku 1)
- 1984 (Raisi Ronald Reagan): Oktoba 3 to Oktoba 5 - (Siku 1)
- 1984 (Raisi Ronald Reagan): Septemba 30 to Oktoba 3 - (Siku 2)
- 1983 (Raisi Ronald Reagan): Novemba 10 to Novemba 14 - (Siku 3)7
- 1982 (Raisi Ronald Reagan): Disemba 17 to Disemba 21 - (Siku 3)
- 1982 (Raisi Ronald Reagan): Septemba 30 to Oktoba 2 - (Siku1)
- 1981 (Raisi Ronald Reagan): Novemba 20 to Novemba 23 - (Siku 2)
- 1979 (Raisi Jimmy Carter): Septemba 30 to Oktoba 12 - (Siku11)
- 1978 (Raisi Jimmy Carter): Septemba 30 to Oktoba 18 - (Siku 18)
- 1977 (Raisi Jimmy Carter): Novemba 30 to Disemba 9 - (Siku 8)
- 1977 (Raisi Jimmy Carter): Oktoba 31 to Novemba 9 - (Siku 8)
- 1977 (Raisi Jimmy Carter): Septemba 30 to Oktoba 13 - (Siku 12)
- 1976 (Raisi Gerald Ford): Septemba 30 to Oktoba 11 - (Siku 10)