Jamani mwenzenu nusuru yanipate hapa Bongo. Nilikutana na dalali aliyekuwa ananiunganishia na muuza pikipiki maeneo ya Mikocheni. Alidai kuwa pikipiki atakayoniuzia ni mpya, nzuri na haijatumika sana, na bei yake ni sawa na bure na ina vibali vyote.
Nilikuwa na uhitaji nayo kwa kweli, hivyo nikakubali nikaione tufanye biashara. Tukaondoka hadi maeneo ya Kisutu alikodai kuwa ipo.
Tulipofika na kuingia getini kule uani akanionyesha bajaji na kuniambia nilichokuwa nauza ni hii bajaji kiongozi. Nilishangaa kwa kweli.
Ndugu zangu huyu si tapeli? Je, nitaendelea kumuamini? Mtu mmoja nilipomsimulia akaniambia ukiendelea kumwamini mtu wa ina hiyo wewe utaonekana kichaa.
Iko hivi:
Mlipomkamata mliitangazia dunia kuwa ana tuhuma za kuua viongozi wa serikali. Mnafika Kisutu mnasema hapana, sio kuua viongozi bali kulipua sheli ya Mhindi na bado hamna aibu na kuna watu wanawaamini.