Siasa za Pemba na muujiza unaojitokeza na kupotea

Siasa za Pemba na muujiza unaojitokeza na kupotea

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MWANADAMU NA MUUJIZA

Binadamu tunapenda muujiza kwa kuwa inarahishisha kufikiri.

Kwanza nataka kukutoa hofu juu yangu ili nikufahamishe kuwa mimi hupenda kuukubali ukweli unapodhihiri na hii ndiyo sifa inayomnyanyua binadamu yeyote yule akathaminika achilia mbali wale wanojiita wasomi.

Ukisikiliza kile ukipendacho ukaukataa ukweli heshima ya usomi wako itakwenda chini. Nimeangalia ‘’clip’’ ya mapokezi makubwa aliyopata Dr. Hussein Mwinyi Pemba. Niliyoyaona kwenye clip ni tofauti ya hali ya Pemba kama tunavyosikia.

Hali ya Pemba hivi sasa ni kuwa tunaelezwa na wananchi wa Pemba wenyewe kuwa wananyimwa vitambulisho ili wasipige kura.

Nani anawanyima Wapemba vitambulisho na kwa sababu gani? Ipo clip hapa ya tatizo hili mimi kwa kurahisisha utambulisho nimeipa jina "Ngoma za Vita Zinapashwa Moto Huu ni wakati wa Masheikh wa Zanzibar Kuzungumza."

Ukisikiliza ‘’clip’’ hii moyo utaingia hofu ya hayo yanayoweza kutokea. Haya yanafahamika hayahitaji maelezo zaidi.

Miezi michache iliyopita tumeona CUF ilivyokufa Zanzibar kwa dakika moja au ukipenda nukta moja katika "Shusha Tanga Pandisha Tanga Safari Iendelee..."

Wimbi hili nimetafuta mfano wake pengine duniani sijaona. Maalim kahama na wanachama wote na ofisi zao mitaani kwa dakika moja na kuzigeuza ofisi zote kuwa zambarau.

Wanachama, ofisi zao na bendera ndiyo "symbols" za nguvu ya chama. Chama kikiwa hakina vitu hivi kama viaashiria basi jua hapo hakuna chama.

Katika hali kama hii sijaona juhudi za CCM kukijenga chama chao Pemba au hata Unguja au kusikia hotuba za kuwavutia wale waliokuwa wanawapinga kuvutika kuwaunga mkono, ila nilichosoma ni taarifa kuwa Dr. Mwinyi apokelewe na yaorodheshwe majina ya watakaotoka kumpokea.

Huu ni ujumbe kutoka serikalini. Hiki ni kichekesho.

Haiwezekani kujenga chama chochote kwa namna hii au kuhamasisha wanachama kwa mtindo huu. Chama hakijengeki kwa vitisho vya "roll call," chama kinajengwa kwa mapenzi na ari ya wanachama wenyewe.

Lakini hapa ndipo ulipo muujiza wenyewe. Dr. Hussein Mwinyi kapata mapokezi makubwa Pemba kama ‘’clip’’ inavyoonyesha.

Binadamu tunapenda miujiza kwa kuwa huhitaji kufikiri sana kujua kwa nini kishowezekana kimewezekana.

Nayasema haya nikitazama historia ya TANU vipi watu masikini na wasio na elimu walivyounda TANU kikawa chama kikubwa cha kupigiwa mfano Afrika nzima.

Chini ya mwaka mmoja TANU na Nyerere wakawa wanafahamika Tanganyika nzima na wananchi wanakiunga mkono chama.

Wanachama wakitoa nyumba zao kufanya ofisi za TANU.

Walifanya haya kwa ari na mapenzi sio kwa vitisho.

Hebu tuangalia hali ya leo mapokezi ya Dr. Hussein Mwinyi.

Muujiza gani umefanyika kuwaleta wananchi wa Pemba ngome ya ACT Wazalendo kujitokeza kwa wingi kiasi hiki?

Ni hii hofu ya jina kutoonekama katika daftari la mahudhurio au ni mapenzi ya dhati kwa Rais ‘’Mtarajiwa?’’

Au ni silka ya binadamu ile "cunning, wily people," watu walio na uwezo mkubwa wa ghilba na kulaghai.

Nasema haya kwa sababu CCM Pemba haijaweza kupata kiti hata kimoja katika miaka yote ya uchaguzi kutokea 1995.

Sasa cha kujiuliza ni hao washangiliaji wametokea wapi?

Kuna kitabu "The Ugly American," ni ‘’novel’’ na ‘’movie’’ kuhusu watu wa Mashariki ya Mbali katika tabia zao za ujanja wa kujifanya wajinga na wewe ukaamini kuwa ni wajinga kumbe ile ni mtego wao wanatega wanapokutana na adui.

Yawezekana tuliyoshuhudia ni katika sura mbili za Pemba?

Ikiwa yapo yaliyofanywa na CCM Pemba kupata wanachama na kuungwa mkono mimi yamenipita ningependa sana kujifunza kutoka kwenu kwani miujiza haifanyiki tena siku hizi.

Kila cha kustaajabisha lazima tukieleze kisayansi.
 
Hivi huko Pemba hakuna maendeleo yoyote yaliyotokea tangu wapate uhuru? Je, maendeleo hayo yanafanywa na nani? Hivi kweli vyama vya upinzani Zanzibar na Pemba vinaweza kweli kuwa na ushawishi kuzidi CCM?

Hivi kweli Maendeleo yanayofanyika/ Wengine watasema sio maendelo bali ni dhuluma inaweza kuendelea hadi pale Seif Hamadi awe kiongozi mkuu? Je, Vyama vya upinzani ndio vitakavyoleta maendeleo ya kweli?

Titaona mengi kabla ya October lakini Watanzania sio wajinga.
 
Viongozi huchaguliwa na mfumo kura za wananchi ni kivuli tu cha kupima imani. Huu ndio ukweli mchungu ila ni mfumo wa duniani kote kabla ya kuteuliwa na kupitishwa kuwa mgombea lazima system/ deep state team ikukubali baadaye ndio wananchi wapewe nafasi ya kufanya uchaguzi. Vinginevyo dictatorship/uasi ama mapinduzi vitumike

Deep state team inaweza kumteuwa yeyote ata akiwa ni mpinzani ikiwa tu itaaonekana ndio mbadala muafaka. By the way ata iweje huyo mgombea wa CUF akishinda urais kwa 90% hawezi kupatiwa kwa maslahi mapana ya Taifa. Sharif Hammad ni chaguo la watu lakini akiachiwa nchi ni kiama kwa Tanzania...How?Why? When? Where? Only paranoids can understand and manipulate the situation! Kipi bora mtu wa zamani mwenye kuvalia mavazi mapya/Old person in a new clothes? Au MTU mpya mwenye mavazi ya zamani?

Mtoa mada anafahamu vizuri historia ya akina Tumteneke Sanga, Abeid Karume, Jumbe, Oscar Kambona, Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kujadili siasa zinazoendelea ni kujitoa ufaham usio wa ulazima sheria huwa zinapindishwa kwa maslahi ya umma.

Tatizo sio kusema ukweli Je ukweli huo ni kwa manufaa ya nanii? Nichomekee tu pindi ikionekana CCM kubakia madarakani ni hasara kwa taifa ama itasababisha amani kutoweka daima nchi itaachiwa wapinzani kwa muda utakaopangwa sio jambo rahisi kuwa kiongozi mkubwa wa nchi ya democracy kwa kura tu. Deception is a state of mind and mind of the state by James .
 
Nasema haya kwa sababu CCM Pemba haijaweza kupata kiti hata kimoja katika miaka yote ya uchaguzi kutokea 1995.

By Maalim Mohamed Said. Hii sentensi nimeipenda sana.
 
Ee Mungu uliyetukuka. Iepushe nchi hii na mabalaa. Wape ufahamu watawala na watawaliwa wa namna bora ya kuishi katika ulimwengu huu uliouumba ili watu wajue mambo mema wayafuate na mabaya wayaache. Ee Mungu; kheri imo mikononi mwako na shari imo mikononi mwako. Wewe ndiye unayeweza kutuonesha njia iliyonyooka. Tunaomba utuoneshe.
 
Back
Top Bottom