Malcolmx Shabaaz
Senior Member
- Nov 21, 2017
- 128
- 174
SIASA ZA UJERUMANI (ADOLF HITLER NA WANAZI)
Jina la Hitler limepata umaarufu mkubwa sana ulimwenguni kuliko majina ya madikteta wote waliopata kutokea ulimwenguni! Huyu alikuwa na uwezo wa juu sana wa kufanya ukatili ambao si wa kawaida kufanywa na binadamu!
Alizaliwa tarehe 20 April 1889 katika Mji wa Brau Nau Amm Inn nchini Austria; mama yake mzazi alifahamika kwa jina la Clara Hitler na baba yake mzazi aliitwa Alois Hitler Sr. Baba yake Hitler alikuwa ni mtumishi wa umma huko Austria ambako Hitler alikulia.
Hilter alisoma na kuishia njiani ambapo alikatisha masomo kwa sababu hakupenda shule; alikua na ndoto tofauti kabisa na shule. M-Austria huyo mwenye asili ya Ujerumani alijiunga na Jeshi la Ujerumani mwaka 1913 kipindi kuelekea Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, (1914-1918).
Hitler alishiriki Vita Kuu ya Dunia na mpaka mwisho wa vita alikuwa majeruhi na nchi yake ilishindwa katika vita jambo ambalo lilimuudhi sana huku akiamini kuwa kushindwa kwa nchi yake kulitokana na usaliti wa baadhi ya watu. Aliamini kuwa walioisaliti Ujerumani walikuwa Wayahudi, Wajamaa, Wakatoliki na makundi mengine ambayo kuanzia hapo alianza kuyachukia.
Alijiunga na Chama cha Wafanyakazi (Germna Workers Party) mwaka 1919 chama ambacho kilianzishwa mwaka huo na Anton Dlexler. Mnamo mwaka 1921 Hitler ndiye alichaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa chama hicho.
Mpaka wakati huo alikuwa tayari ameshakuwa na nadharia ya ukatili na chuki kubwa sana dhidi ya watu alioamini walikwamisha Ujerumani katika harakati zake za vita.
Alifanya jaribio la mapinduzi katika Mji wa Munich tarehe 8-9 Novemba 1923 akiwa na vijana wake wapatao mia sita (600) jaribio ambalo lilikwama huku yeye na wafuasi wake wengi wakiishia kukamatwa na serikali ya Von Stresseman.
Hilter alipokamatwa alihukumiwa miaka minane gerezani mwaka 1924 lakini alikaa miezi nane na kupata msamaha akawa huru kutoka na alitoka akiwa ameandika kitabu maarufu kwa jina la Mein Kampf (Harakati zangu). Kitabu hicho ndicho kilikuwa na nguzo za U-NAZI (Nazi Principles).
Mnamo mwaka 1932 wakati Ujerumani ikiwa imeumizwa sana na mtikisiko wa uchumi ulioikumba dunia kati ya mwaka 1929-1933, Hilter alipata upenyo wa kuwa mwanasiasa kivutio. Alipata jumla ya kura 11,000,000 na viti 230 Bungeni; alishindwa kura za Urais ambapo Von Hindenburg aliongoza kwa kupata kura 18,000,000.
Kutokana na nguvu ya Hitler na uwingi wa wabunge kutoka Nazi Party kuliundwa serikali ya mseto ambapo Hitler aliteuliwa kuwa Kansela wa Ujerumani mnamo tarehe 30 Januari 1933.
Serikali iliamini kwa kumteua Hitler itakuwa imepunguza matatizo na vurugu zake lakini kumbe ilikuwa kinyume, kumpa ile nafasi kulimfungulia mlango wa kutekeleza ukatili wake kwa urahisi zaidi hasa baada ya Rais Hindenburg kufariki tarehe 02 Agosti 1934 na Hitler kunyakua madaraka kirahisi zaidi.
Njia alizotumia Hilter kuondoa upinzani
· Kujilimbikizia mamlaka; Maamuzi yote alitoa yeye, alifuta mamlaka za serikali za mitaa ili maamuzi yote afanye yeye.
· Aliweka sheria za kuwabagua Wayahudi; Wayahudi walionekana kuwa wapinzani wakubwa wa sera za Ki-Nazi, hivyo basi, aliamua kuweka sheria za kuwabagua ili kuwanyamazisha. Mwaka 1935, zilitungwa Nuremberg Laws zilizowapokonya Wayahudi uraia wa Ujerumani na kuwapoka mamlaka ya kukosoa.
· Alifuta baadhi ya vyama vya upinzani huku vingine vikijiondoa vyenyewe kwa hofu; Social Democratic Party, Central Party na vyama vingine vilifutwa rasmi mwaka 1933.
· Kufutwa kwa vyama vya wafanyakazi; Alianzisha German Labour Front huku vyama vyote vikitumbukizwa humo na kiongozi mkuu wa wafanyakazi aliteuliwa na Hitler, aliitwa Dkt Robert Ley.
· Kumezwa kwa Taasisi za Kidini; Hitler alimteua Askofu Mkuu bwana Ludwig Muller huku Wajerumani wote wakilazimishwa kuabudu katika kanisa moja, German Christian Church. Viongozi wengi wa kidini waliomkosoa aliwaua na wengine aliwafunga; kwa mfano Pasta Martine Niemoller alihukumiwa kifo!
· Kuanzishwa kwa kambi za mateso na mauaji; Alianzisha kambi za kutesa na kuua wakosoaji, kwa mfano Sobibor, Treblinka, Majdanek na zingine nyingi ambako inakadiriwa Wayahudi milioni sita waliuawa (6,000,000).
NB: Hitler alijiua tarehe 30 April 1945 kwa risasi huku mkewe kipenzi Alijiua kwa sumu; wawili hao miili yao ilitumbukizwa katika shimo lenye kufuka moto ili maadui wasiipate wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, 1939-1945.
Akhsante, tukutane siku nyingine.
Malcolm X.