Siasa za visasi: Rwanda yapandisha ushuru kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania

Status
Not open for further replies.
sitashangaa kusikia balozi za nchi mbili hz zikifungwa,,,,kama mwenendo ndo huu.pk is a loser in this game
 
Ujinga hapo wanawaumizi wananchi wao,anayepeleka mizigo atapandisha bei za bedhaa zake ili kufidia hilo ongezeko la ushuru
 
Dear Mr President,


Tukiendelea namna hivi hata wananchi wako watakudharau kama sio washakudharau, enough with diplomacy with Rwanda. Time for affirmative actions, funga mipaka ya nchi dhidi ya warwanda, tusiruhusu kitu chochote kiingie kwa barabarani, anga wala bahari, funga mazao yanayoenda rwanda na vile vile waambie vijana wafunge DRC hakuna kuruhusu kitu. Mwite balozi wako arudi Tanzania tufunge hata diplomasia nao kwa muda mrefu. Na waambie vijana wako wakae tayari kuanzia JWTZ, JKT na Ex-JKT na EX-JWTZ. Huyu mpuuzi asituumize kichwa
 
Ni wakati sasa serikali ya Tanzania ipandishe ushuru wa bidhaa zinazotoka Tanzania kuingia Rwanda mfano Mchele, etc, na tuone nani ataumia zaidi
 
Atakayeumia ni Mnyarwanda wa kawaida, maumivu kwa mwenye gari yatakuwa ni ya muda tu. "Any cost added to a product, that very increment is charged to the end user". Huyo kimbao mbao PK sidhani kama ni mwanauchumi, ameamua kutumia udikteta tu kuleta hayo japo hajui anayeumia ni mnyarwanda wa kawaida. Wahima bwana, ni kama Ngamia, ukimruhusu aingize kichwa tu, mwili mzima atauingiza tu!!!!!
 
rules of the game will teach him a hard lesson.... watu hasa watanzania hatuna haja ya kuogopa kuhusu hivi vita ya kagame dhidi ya tanzania..
kuna watu wenye hulka kama ya kagame hilo lazima tulikubali, watu hawa huwa wanaweza kutangaza vita na mtu yeyote(hata mungu ikibidi), huku wakijua fika hawawezi kushinda vita husika.
madhara ya huo upuuzi aliochukua ni makubwa saaaana kwa wananchi wake maana ni wazi KWENYE SOKO HURIA hakuna bei elekezi katika kila bidhaa. na kama ilivyo kwa wafanyabiashara wote duniani, faida watakayoipata kutokana na ongezeko la ushuru ni kubwa kuliko kama ushuru usingeongezeka.
wanyarwanda imekula kwao na kwa hili linatusaidia zaidi kwa sababu KAGAME anazidi kuongeza sababu za kuchukiwa na wananchi wake.
 
It takes two to tango, kama unadhani CCM haihusiki, subiri joto la jiwe. Unakumbuka after vita vya Mtukula, tulivaa matairi ya gari, mbunju na maduka ya kaya.

watusi shida kweli kweli, kuwapokea kama wakimbizi tu ishakuwa nongwa, just weight your days are numbered.
 


Mkuu, anapoamua kupandisha gharama za road toll kwa magari ya tanzania kuelekea rwanda nadhani amejaribu kucheza smart. as one of the post here imesema wafanya biashara sio watu wanaopenda kupata hasara.


  1. hauoni kwamba anapunguza nafasi ya wafanyabiashara wa rwanda kutumia any possible means ya usafiri kutoka tz kuingia kwao?
  2. kwa uamuzi huo inamaanisha kwamba.. ili waweze kutengeneza faida za kutosha lazima waweze kupunguza gharama za uendeshaji, ikiwemo kutumia njia zingine za usafirishaji wa ardhini ikiwemo kutoa mizigo yao kutoka kenya??
  3. na pia kuhusu hao wafanya biashara watakao tumia ku_import kupitia bandari ya dar, hauoni watakuwa wanajiondoa wenyewe kwenye soko maana hawataweza kushindana na wenzao wanaoingiza bidhaa zao kutokea kenya ama inchi nyingine.. as kwenye soko kutakuwa na tofauti ya bei kwa bidhaa ambazo zitaweza kuwa katika ubora sawa??
 
Hapa serikali irudishe compliments tu na magari yatakayo toka Rwanda yapate same treatment for now at least we should gain whilst they are still reinforcing their strategy of diverting their cargo to Mombasa.

we dont have to return the favor to them.. itakuwa sawa na kumpiga chura teke..

lengo hapa ni kutengeneza mazingira bora ili huduma zirejee na kuondokana na hivyo vikwazo.. otherwise.. kuna mengi tu yatatokea
 

NIambie ni lini Umoja wa Mataifa ulipeleka vikosi vyake Iraq, Somalia au Afghanistan? au hujui kuwa hizo nchi zote UN haikuhusika? nchi zote ambazo UN imehusika kwa kupeleka vikosi vyake zimetulia kabisa......the balcans-cosovo, yugoslavia, macedonia, liberia, ivory coast, sierra leon, cambodia etc etc, ziko tuli kabisa....hizo ulizoorodhesha SI UN iliyohusika.....nakupa hili somo bure.
 
Mimi nilijua wamekatalia magari yetu kuingia inchini mwao kumbe wameongeza fee kwenye magari. Sisi acha tuendelee kutoa misimaha ya kodi.
 
Mimi nilijua wamekatalia magari yetu kuingia inchini mwao kumbe wameongeza fee kwenye magari. Sisi acha tuendelee kutoa misimaha ya kodi. Leta hoja zenye mashiko na ambazo zitaleeta manufaa kwa taifa na sio huu upuuzi.
 
Ifike mahali hii cold war iishe. Tena tuache kabisa kushabikia haya mambo. Haipendezi kuwa na jirani ambaye hamsalimiani hata kama wewe ni tajiri na una kila kitu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Kagame ni arrogant. Suluhu na yeye ni kupitia mtutu wa bunduki tu. Tumng'oe tu huyu muhuni.
 

Tuchukulie ya kwamba wewe uko sahihi,

a. Ni kwa kiwango gani mchango wa pato la nchi yetu unatokana na upokeaji wa mizigo ya Rwanda kupitia Tanzania? Isitoshe kama wao watatumia bandari ya Mombasa ni kwa kiwango gani sisi tunapungukiwa na fedha za kigeni?

b. Sisi kama Tanzania tunategemea nini hasa toka Rwanda ambacho tukiamua nasi kuongeza road toll tutaumia? Vile vile kwa kiwango athari hizo zitasababisha ongezeko la gharama za maisha nchini?

c. Je sisi tukifanya kulipizia kisasi wao wataathirika vp kutoka Tanzania?

Tanzania kiuchumi Rwanda ni kama tone la maji kwenye ndoo. Ila Rwanda kuna analotafuta kwetu ni bora tu tufunge mjadala tulisubiri hilo jambo kwani wanazidi sasa. Bandari ya Tanzania mizigo ya Rwanda inaweza kutokomea na pamoja na mafuta yao wanayoagiza bandari yetu ikawa na nafasi ya kubeba mizigo zaidi ya kutoka Zambia na Malawi. Vile vile Congo tukishamaliza kazi yetu tunaimarisha uhusiano wetu mambo yanakuwa safi kabisa kwani Congo inabeba Rwanda, Kenya, Uganda kwa pamoja kwenye economic viabilities.
 

mkuu ukubwa wa pua si wingi wa kamasi.
 

Kwa tafsiri ya haraka, bidhaa za TZ zirakuwa bei juu wkt za nchi nyngne zikiwa chini na kusababisha bidhaa za TZ zisinunulike,hvyo hasara kwa wa TZ.
 
Last edited by a moderator:
Mnalalamika nini wakati mlisema Kuwa uchumi wenu ni bora na hamuwahitaji hao wanywarwanda



Mmeanzisha threAds zaidi ya 20 kuishambulia nchi yenye watu laki 2


Aibu sana hiii
 
sipati picha ingekuwaje kama kagame angekuwa rais wa taifa kubwa kama tz.
Na sielewi kwa nini Tanzania tunamdekeza kiasi cha kuomba suluhu nae.inachefua sana.

Kama Kagame angekuwa rais wa Tanzania tungekuwa na maendeleo makubwa tofauti na sasa chini ya msanii Kikwete!
 
watanzania hautpaswi kulialia kwanza tumshukuru mungu kwa kutuweka kwenye mlango bahari hii ni changamoto tuboreshe huduma katika bandari yetu hayo ya Paulo kugomea bandari yetu tuliyafahamu tokea mapema na hatupaswi kuhamaki huyo Paulo ana matatizo sana nadhani Rwanda kama ndo ingekuwa na bandari HAKI YA MUNGU TENA TUSINGEKUNYWA MAJI NA hakuna rangi tungeacha kuona lakini hiyo ni maskini jeuri mwache atapetape tu siku sio nyingi kwa kenyata nako kitanuka mm nashauri serikali yetu iboreshe mazingira ya bandarini Paulo hana ujanja one day atakuja sasa hivi si kiburiiiiii
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…