Siasa zimeua Elimu yetu

Siasa zimeua Elimu yetu

Mfukutuzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2015
Posts
239
Reaction score
175
Nimesikitika sana nilipokuwa katika kupitia matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka huu hasa pale nilipoangalia orodha ya Shule 100 bora na kubaini kuwa ni shule 6 tu za Serikali ndizo ziko kwenye orodha hiyo, inasikitisha sana.

Shule zilizoonekana ni Ilboru ambayo ni ya 35, Mzumbe ya 56, Msalato ya 71, Kibaha ya 87, Tabora boys ya 93, pamoja na Kilakala ambayo imeshika nafasi ya 96 na zilizobaki zote ni Shule binafsi.

Mimi nauliza tu, hii ina maana gani au ndo matokeo ya BIG RESULT NOW?

Haya mimi nasema ni matokeo ya kuingiza siasa kwenye Elimu na kujikuta tukitumia muda mwingi kuongeza kiwango cha ufaulu badala ya kuongeza kiwango cha Elimu.
 
Ha ha serikali ilicheza na akili za wadanganyika alafu toka maajabu yaatokeo mabovu mwaka 2011 na 2012 ikatambulishwa BRN ndani ya miezi mi nane eti matokeo yakapanda

Waka introduce system mpya ya GPA tukaikubali ila mnajua serikali ya CCM ilichofanya?

Walitanua goli, ili mpigaji aone eneo kubwa la kuingizia mpira, kwa maneno mengine waliongeza ukubwa wa mlango, kama mlango ulikuwa mita 2 kupita ni issue wakabomoa wakaufanya mita 10 ili wengi wapite bila kubanana, mwaka uliofuata 2013 matokeo yakapanda

Tukapiga makofi na yanazidi kupanda, nchii hii inaharibiwa sana wenye nayo tumelala, matokeo tangu 2012 ni mabovu na mabovu kila mwaka

Leo wameleta sera mpya, nimeanza kuisoma ila ni majanga.
 
Na vitu vya msingi kama hivi vinazimwa na mijadala ya sinema za uongo wa Amboni
 
Back
Top Bottom