Sichanjwi na nikifa roho yangu ikawe laana kwa kila kiongozi aliyesema chanjo ni mbaya

abdulhamis

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2019
Posts
1,436
Reaction score
2,296
Habari wadau, leo nimeona niiweke msimamo wangu juu ya chanjo sababu Maneno yamekua Mengi

Nasema hivi sichanji chanjo yoyote Ile sababu Serikali yangu ilikuwa kila nikilala nikiamka nakuta kuwa chanjo ya Corona haifai na watanzania tusikubali. Ikiwa kama viongozi wote walishiriki kutuambia hayo basi likitokea la kutokea Leo sio tu kwangu mimi hata kwa baadhi ya watanzania wengine ambao wanakataa chanjo kwa sababu ya maneno yao ya mwanzo Basi wa kulaumiwa ni Serikali

Pia ifike Hatua Serikali isituongoze kwa hisia tu sababu nchi ni moja watu wale wale lakini nashangaa Jana ilikuwa tunaambiwa hii sumu tena inaua halafu leo tunaambiwa hii dawa tena inatibu cha ajabu watu ni wale wale waliotuambia jana tena bila aibu leo ni Corona kesho itakuwa nini?

Viongozi wa Tz mbadilike
 
Waziri Gwajima alisema tule tangawizi na malimao,saa hizi kashachanjwa!
Usiwaamini wanasiasa,wakisema kumekucha kachungulie nje kama kweli kumekucha.
 
Kufa utakufa tu uwe umechanjwa au hujachanjwa,maana hakuna atakayeishi milele.
Hizo laana wapelekee ukoo wako wengine unapiga hewa.
 
Sija like tu hapo juu ila namie sichanjwi.
 
Kama unategemea wanasiasa ndio waongoze maisha yako binafsi basi akili huna na Mbinguni huendi
 
We kufa tu kwa ujinga wako
 
Mwisho utaomba viongozi wa Serikali waje wakuongoze kwenye mambo yako na mkeo chumbani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…