whitehorse
JF-Expert Member
- Aug 29, 2009
- 2,565
- 4,432
Mimi nimeajiriwa katika kampuni ya wahindi. Nina ajira nao ya kudumu (permanent) huu ni mwaka wa 3 sasa. Juzi niliumwa sana nikaenda hospitalini. Baada ya vipimo dr anasema nahitaji vipimo zaidi na kuna dawa za matibsbu natakiwa kutumia. Pili anasema kwa muda wa siku 12 zijazo natakiwa kupumzika na kufanya vipomo kwa kila siku ya 3 hadi ifike Mara 4 huku nikiendelea na dose. Dr aliniandikia report vizuri ili nipeleke ofisini kwa ajili ya kupewa likizo ya mapumzuko ya ugonjwa -sick leave. Huko ofisini ndipo nilikutana na mshangao kuwa eti nimebakisha sick leave ya siku 2 tu baada ya hapo nitaanza kulipwa nusu mshahara. Nikauliza jamani ni lini nimechukua likizo ya ugonjwa nikajibiwa tangu uanze kazi hadi leo Una jumps ya ED 61. So zikifika 63 naanza kupewa nusu mshahara. Nikabaki mdomo wazi nisijue cha kufanya. Sasa naomba msaada maana Mimi ni mwanamke Nina watoto 4 na mume. Kuna siku ambazo watoto waliumwa, mume pia na hata Mimi. Zote zimekuwa zangu na je sheria ya likizo ya ugonjwa inasema hivyo kweli? Naomba msaada wa dhati naumia mshahara wenyewe hautoshi nikilipwa nusu je? Mmnaona nadhulumiwa haki yangu.