Sielewagi maana ya R.I.P (REST IN PEACE)

samagi

Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
53
Reaction score
34
*R.I.P[emoji779]*
*R.I.P[emoji779][emoji779]*
*R.I.P[emoji780][emoji780][emoji780]*
⚰⚰[emoji24]⚰⚰[emoji24]⚰⚰

*"PUMZIKA KWA AMANI" [emoji779]*

JE KUNA AMANI IPI KABURINI[emoji780][emoji15]

*"MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI"*

HUKO MAHALA PEMA NI WAPI[emoji780][emoji15] JE WAPO WASIOLALA MAHALA PEMA HUKO PEPONI?[emoji134]‍♂[emoji779]

*UTANGULIZI*
Limekuwa ni jambo la kawaida kuwaambia ndugu zetu waliolala ( wafu) wapumzike kwa amani ( R.I.P) na wengine wakaenda mbali zaidi kumsihi Mungu azilaze Roho hizo mahali pema!

BIBLIA INASEMA WAFU WAKO WAPI???
Mwanzo 3: 1 *"Kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi"*

»»» NB: WAFU WOTE WAPO MAVUMBINI HAIJALISHI WALITENDA MEMA AU MABAYA WANASUBIRI YESU AJAPO KUTOA HUKUMU.

R.I.P( PUMZIKA KWA AMANI)
JE KUNA AMANI YEYOTE KABURINI MTU ANAPOKUFA???
Muhubir 9:5 *"Lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa"*

NB: WAFU HAWAJUI NENO LOLOTE WALA HAWANA MAWAZO WALA KUMBUKUMBU YA CHOCHOTE NI KAMA MEZA, JIWE NA VIUMBE VYOVYOTE VISIVYO HAI! KWAHIYO KUWAAMBIA WALALE MAHALI PEMA HAKUNA WEMA WALA GHASIA KABURINI. WAFU WOTE HAWAJIELEW!!

*JE TUKIWAOMBEA WAFU WANAWEZA KUFANYA TENA IBADA?* KUTUOMBEA?? AU TUKIWAOMBEA MUNGU ANAWEZA KUWASAMEHE???
»»» Zaburi 115.17
*"Sio wafu wamsifuo BWANA, wala wo wote washukao kwenye kimya"*

»» Zaburi 143:4
*"Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake,Siku hiyo mawazo yake yapotea"*

»» Mhubiri 9:10
*"Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe"*

HITIMISHO
[emoji116][emoji116][emoji116]
O1. R.I.P.( PUMZIKA KWA AMANI)
Huu ni msemo wa kipagani tena unaokinzana na maandiko maana wafu hawajui chochote hivyo hakuna amani yoyote kaburini mfu hajitambui hajielew ni kama kochi au peni hana ufahamu.

O2. MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI
a) Mungu hapangiwi pa kumuweka mfu

b) Mfu akifa anarudi kuwa udongo

O3. MFU HAWEZI KUKUOMBEA WALA KUOMBEWA DHAMBI ZAKE ZIISHE

a) Wafu hawawezi kutuombea sio bikra Mariam mama wa Yesu wala mtakatifu yeyote aliyekwisha kufa anaweza kutuombea Kwa Mungu, Biblia inasema tuombe kwa jina la Yesu pekeee.. (Wafilipi 2:10)

b) Mtu akifa historia yake imefungwa hawezi kuombewa dhambi zikamtoka,

c) Ibada na maombezi ni kwa walio hai tu

IBADA ZA KUOMBEA WAFU NI UPAGANI NA MACHUKIZO KWA BWANA

*WITO:* TUMKIRI YESU NA KUMFUATA TUKIWA HAI ILI HATA TUKIFA TUWE NA TUMAINI KUWA AJAPO MARA YA PILI ATATUPA MIILI YA KUTOKUHARIBIKA NA TUTAISHI NAE MILELE..!!

Nakuachia swali la changamoto:
*Kama ibada ya kumuombea mfu ina maana kuna umuhimu gani wa kumtumikia Mungu ukiwa hai si usubiri tu ukifa uombewe dhambi zitoke? Je, nani atapewa adhabu ya moto na kupotea milele wakati wafu wote huwa wanaombewa?*

TAFAKARI
 
Mimi nilisha wacha kusema rest in peace au Mungu ilaze roho ya fulani mahala pema peponi! Mimi huwa nasema poleni sana. Kusema hayo kunatokana na ukosefu wa elimu ya biblia. Kama mkristo wa kweli, haitakiwi kutuma rambirambi marehemu za nama hiyo maana ni kinyume na maandiko. Tatizo wengi wanafwata mkumbo bila know how ya biblia.
 
Just to correct you....Yesu..hata rudi kuhukumu mtu sio kazi yake hiyo ni kazi ya Mungu kuhukumu...
 
Eti Yesu atarudi kuhukumu,kwani huko aliko hakuna wa kuhukumu?uongo mwingine wa hovyo sana,naomba nioneshwe kwenye biblia ni wapi Yesu kasema atakuja kuhukumu?
 
Hitimisho 2 (a):

Ni kweli kabisa Mungu hapangiwi pa kumuweka mfu. Na kama kweli wewe ni msomaji mzuri wa biblia, biblia inasema kwamba MUNGU WETU NI MSIKIVU.

Sasa basi, tunaposema Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, pale ni kwamba HAPANGIWI, ila ANAOMBWA. Na ndio maana kauli hiyo huanza na neno TUNAKUOMBA uilaze roho ya marehemu mahala pema peponi, tukiamini kwamba YEYE NI MKUBWA NA ANA UWEZO KULIKO SISI, ndio maana tunajinyenyekeza kwake na kumuomba, sio kumshurutisha.
 
Fact 100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…