Sielewagi maana ya R.I.P (REST IN PEACE)

Yesu ni mungu wa wapi?mnajiita wasomi lakini ni empty kabisa,rudi kaikague biblia vizuri itakueleza huyo unaemuita mungu ameelezewa vipi
Wapumbavu hawataelewa hili, ila Biblia na Qur an vinaonesha wazi kuwa Yesu ni Mungu
 
Mwisho wa siku kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe..

Mbona hujaongelea kuhusu roho ya mtu na ulimwengu wa kiroho?
Tueleze basi ilivyo na kifo..
 
Mkuu,
Asante kwa nyuzi yako nzito na yakinifu.
Mimi binafsi hupenda watu wanaopenda upembuzi wa jambo na kulitafakari kwa undani.
Ulioyanukuu yanaleta sense lakini kuyakubali moja yumkini kujiweka katika fungu tofauti na wanadamu.
Kiwango kikubwa cha maisha ya mwanadamu hutawaliwa na imani, hivyo basi imani humfanya mwanadamu Huyu asielewe mambo na kuishi kama robot.
Mwanadamu ana imani siku zote kwamba wanaokufa wanaenda kwa mungu kungojea hukumu Siku ya mwisho ndio sababu waliobakia humtuma marehemu wao kwa mungu na vilio mweke mahali pema peponi in mayai tu ndio hawana uhakika kama yapo wangeagiza akaangiwe mayai.....!
 
Kwa akili yako unadhani yale yote yanayofanyika baada ya mtu kufa huwa anafanyiwa marehemu?Na watu wanaposema R.I.P unadhani wanamwambia marehemu?
Kama unadhani hivyo tafakari tena jinsi unavyofikiri.
Mambo yote haya hufanyika kama tu ishara ya kuonesha watu wameguswa na kifo cha marehemu na hawana lugha yoyote tamu ya kuelezea matarajio yao na faraja kwa wanaobaki isipokuwa kuamini kuwa ipo amani baada ya kifo.
Ni sawa na unapomwambia mtu lala salama wakati mtu akilala,anakuwa hajui nini kinaendelea juu yake na wakati mwingine hana uwezo wa kujihakikishia usalama anapokuwa usingizini.
Ama unamwambia mtu safiri salama wakati yeye si dereva wala rubani.Hana uwezo wa kubadilsha chochote iwapo Mungu ataamua vinginevyo,sasa unataka kutuambia tusiseme hivyo kwa kuwa tunajaribu kumpangia Mungu tunavyotaka sie?
Maneno haya hutolewa kama faraja tu ya waliobaki ili kupunguza maumivu ya kuondokewa na mpendwa wao,kwani wakati wewe unazungumzia habari za mavumbini,bado biblia hiyo hiyo imezungumzia habari za mateso baada ya kifo.Na hata hivyo hujui pia ni hatua zipi hufanyika hadi ukawa mavumbi.Hatujui vizuri Yesu alipotoa mfano wa Lazaro na na yule tajiri kama ni uhalisia ama ilikuwa mfano tu.Labda utuambie ni dhambi gani ukisema R.I.P na usiposema utapata thawabu gani?
Ni sawa unapomwambia mtu amani iwe kwako na usiposema hivyo ndipo atakosa amani?Ubishi na Upinzani mwingine hauna maana . Tafakari
 
Mambo ya imani ni magumu hakuna mwenye uhakika 100% kwamba anachokiamini ni sahihi, so it's better to shut up na kuamini unachokiamini
 
Just to correct you....Yesu..hata rudi kuhukumu mtu sio kazi yake hiyo ni kazi ya Mungu kuhukumu...
Ingawa Yesu siyo Mungu mweza yote, amepewa mamlaka na uwezo wa kuhukumu na Mungu.

Mathayo 25:31,32
31 Wakati Mwana wa binadamu atakapofika katika utukufu wake, na malaika wote pamoja naye, ndipo atakapoketi juu ya kiti chake cha ufalme chenye utukufu. 32 Na mataifa yote yatakusanyika mbele yake, naye atawatenganisha watu, mmoja kutoka kwa mwenzake, kama vile mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi.

Mathayo 7:21-23
21 Si kila mtu anayeniambia, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali yule anayefanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni ndiye atakayeingia. 22 Wengi wataniambia siku hiyo, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii katika jina lako, na kufukuza roho waovu katika jina lako, na kufanya matendo mengi yenye nguvu katika jina lako?’ 23 Na hata hivyo nitawaambia waziwazi: Sikuwajua ninyi kamwe! Ondokeni kwangu, ninyi wenye matendo ya uasi-sheria.
 
Jamaa una hoja ya maana sana saa nyingine kufanya vitu kwa mazoea hutuharibu sana
 
Nionavyo mimi kwa nini ibada za mazishi zipo ?
Marehemu yeye anakuwa ameshamaliza safari yake hapa duniani,kwa hiyo Ibada inatukumbusha sisi tuliobaki HAI kuwa hatma yetu sisi pia itakuwa kifo.hivyo TUBADILIKE.
Ahsante mtoa mada fikirishi .
 
Inakuwaje Tunapokufa?

Jibu la Biblia

Biblia inasema: “Walio hai wanajua kwamba watakufa; lakini wafu, hawajui lolote kamwe.” (Mhubiri 9:5; Zaburi 146:4) Kwa hiyo, tunapokufa, hatupo. Wafu hawafikiri, hawatendi, wala kuhisi chochote.

“Utarudi mavumbini”

Mungu alieleza kile kinachotokea tunapokufa aliposema na mwanadamu wa kwanza, Adamu. Kwa sababu Adamu alikosa kutii, Mungu alimwambia hivi: “Wewe ni mavumbi nawe utarudi mavumbini.” (Mwanzo 3:19) Kabla ya Mungu kumuumba Adamu “kutoka katika mavumbi ya nchi,” hakuwepo. (Mwanzo 2:7) Vivyo hivyo, Adamu alipokufa, alirudi mavumbini na kuacha kuwapo.

Jambo hilohilo hutokea kwa wale wanaokufa wakati huu. Inapozungumzia kuhusu wanadamu na wanyama, Biblia husema: “Wote wametoka katika mavumbi, nao wote wanarudi mavumbini.”—Mhubiri 3:19, 20.

Kifo si mwisho wa mambo yote

Biblia inalinganisha kifo na usingizi. (Zaburi 13:3; Yohana 11:11-14; Matendo 7:60)
Mtu aliyelala usingizi mzito hajui jambo lolote linaloendelea. Ndivyo ilivyo kwa wafu pia, hawajui lolote. Hata hivyo, Biblia inafundisha kwamba Mungu anaweza kuwaamsha wafu kana kwamba walikuwa wamelala na kuwapa uhai tena. (Ayubu 14:13-15) Kwa wale ambao Mungu huwafufua, kifo si mwisho wa mambo yote.

Inakuwaje Tunapokufa? | Maswali ya Biblia
 
Bado sijaona mahala inayo sema mimi yesu ndio nitakaye hukumu watu....ila ulicho weka ni yesu atakapo rudi na kuwakana wakristo na kusemq yeye hakuacha mafunzo hayo...na kikubwa kitakacho mrudisha duniani ni kwa sababu alipazwa mbinguni hakufa msalabani kama mnavyo dhania atarudi duniani na ataishi na ataowa na atapata watto na atakufa kama wati wote watakavyo kufa kwa sababu ni binaadamu na kila binaadamu ataonja mauti.
 
[QUOTE="Ngwango, post: 25818275, member: 465883 in mayai tu ndio hawana uhakika kama yapo wangeagiza akaangiwe mayai.....![/QUOTE]

We jamaa umeanza vizuri sana ila hapo mwisho umesababisha mpaka nimepaliwa na chai kwa kucheka, sijui umeazima wapi akili ya kumalizia hii post!
 
[QUOTE="Ngwango, post: 25818275, member: 465883 in mayai tu ndio hawana uhakika kama yapo wangeagiza akaangiwe mayai.....!


We jamaa umeanza vizuri sana ila hapo mwisho umesababisha mpaka nimepaliwa na chai kwa kucheka, sijui umeazima wapi akili ya kumalizia hii post![/QUOTE]
Mkuu,
Pole kwa kupaliwa.
Sio ajili ya kuazima ni yangu tu ni sababu ya upembuzi yakinifu ninaoufanya juu ya jambo.
Hudhuria msiba, uone uoga watu wanao. Wanavyoogopa Maiti na wanavyomtambua Mungu kwamba yupo sio sawa na wakati leta tulivyo hapo sala zote zinaombewa safari ya marehemu kinachobaki hicho tu! Mayai akifika.
 
Wafu wapo wapi?
 
Wafu wapo wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…