Siendi Mkoani Ng'ooo!! Dar es salaam is the future! Mikoani ni didimizo la uchumi binafsi

lara 1

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2012
Posts
15,700
Reaction score
29,164
IGWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Jamani HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI LARA 1!! (Hii sio dini na mimi sio nabiii so sitegemei wote mseme AMINA kuitikia pasi kupinga hoja yangu! You may agree to disagree! Ila jamani tutunze staha na ustaarabu wetu! Tuwe wavumilivu na ubishi uwe wa hoja tu si kutukanana! Aksanteni.

BACK TO TOPIC

Naomba nieleweke sisemi mikoani ni kubaya ama hapafai kuishi all i am saying is the future is brighter in Daresalaam, kuliko mikoani. Kwa mambo mengi Jiji la Wazaramo limetishaaaa!!! Siropoki tu ama kuleta ushabiki nina grounds zangu za kutoa hii hoja binafsi, kwanini huning'oi mjini hata kwa greda!

1. Mkoani watu wamerizika ila Dsm chochote utakacho achieve WE BADO SANAAAAAAA! People are moving mountains. Mkoani mtu akiwa na nyumba 2, magari 2, anaheshimika si kitoto na anahesabika kati ya wenye uwezo. Ila mjini unaweza kuwa hata na commercial buildings 3 ila kwenye list hata hujanukia kuwamo! Kabisaaaa! So huku DSM haurelax, ni mpambano 24/7. Ofisini ukianza ujenzi wa tubanda twako, utasikia flani ana ghorofa 2, na amenza kujenga commercial! Unabakia Whaaaaaaaat? Kumbe mimi bado sanaa eeeh? Unakaza buti. Ukijikamua kupeleka mtoto IST, unasikia jirani yako kapeleka U.K au U.S Orange Country huko. WITH THE CITY IT IS NEVER ENOUGH!!! Ila mkoani watu wanakusifia unajiona umefikaaa, ukistuka ushazeeka. Kama unabisha jiulize ulivotoka jijini kwenda shamba watu uliowaacha wako wapi na wewe uko wapi?

2.Mji COMPETITION IS TOUGH! DEADLY! Ukiwa mkoani una C.P.A wewe bonge ya bosiii! Mkuu wa branch. Mjini C.P.A kama 30 hivi ofisi moja, na wenzio sio tu kuwa ni C.P.A bali hadi CIMA, CFA, ACCA, MBA, hadi Cerificate za law humo humo, degree 3! Yaani usifikiri na hivo vyeti wamepozi wanakungoja uwafikie? Nooooooo! Wanaongeza continuously, graduation baada ya graduation. Yaani hadi ushinde competition ulimi unaning'inia hoi bin taaban. Automatically unajikuta una aspirations kubwaa, sky is the limit, unajiburuzaje usiachwe nyuma? In the end unajikut na wewe ni somebody! Ila mkoani CPA kila mtu anakuita Bosi, basi na wewe unajiona bosi kweli kweli unabweteka. Matokea yake ulioanza nao unasikia wako UN! IMF! US EMBASY! Unabakia nilisomaga nao wale! You remain wondering how you became second rated in life since mligraduate wote UDSM, BCOM, Accounting 2004!!!!!! Tena wewe ulikuwa kipanga wao!

3. Life is damn expensive!!!!! Money is never enough! Akili inakuchemkaa utapataje hela zaidi! Comforts zinageuka luxury matokeo yake suala la kusaka pesa unaligeuza Vita vyako binafsi! Huku umeajiriwa, utawaza biashara, utawaza kila kitu ilimradi jiji lisikushinde. In the end you become a master wa kusaka mahela hadi unatoboa! I got a friend ni Monitoring and Evaluation Manager wa NGO kubwa tu, hapo hapo ana ki NGO chake, hapo hapo Analima kilimo mkoa huko, hapo hapo ana Kampuni, na juzi kapata U Country director NGO ingine anahama kule! Kote huko kupambana na bills na kuokota kila senti. We mkoani ukiwa kwenye NGO kubwa tu, hio pesa life ilivo affordable utapanga li mansion na kuwa mtu wa kuheshimika hadi basi!

4. Fursa hapa mjini ni nyingi mnoooo! Sijui hata nianzie wapi kwenye hili! I have a cousin, aligraduate 2010 ila pasi zake hazikuwa nzuri so akapewa hela na uncle mkopo wa 5m atafute ustaarabu, sio mtu na degree kula kulala tu. Akafungua ki pub tu local na fremu ya pembeni akawa anauza pombe reja reja wine, wisky na vingine. Mungu kambarikia the business is now BIG! Kalipa 5m za watu na naprofit ya laki 6 daily akitoa cost zote duka limekuwa la jumla sio rejareja tena. Na pub ameitanua imekuwa bar. Wala hatafuti kazi tena! Kazi gani utalipwa laki 6/day? Mjini ukiwa na ubongo kidogo tu, hakuna linaloshindikana.

5. Ukiwa mjini unakuwa na VISON KUBWA! BIG DREAMS! BIG AMBITIONS! BIG ASPIRATIONS! SKY IS THE LIMIT! Yaani people always look at the BIGGER PICTURE! Kwa jinsi mambo yanavoenda race automatically you think of next century like tomorrow! Dogo tu nilimuuliza ukiwa mkubwa utajenga nyumba? Akanijibu nani ajenge nyumba? sijengi nyumba najenga GHOROFA!!!!!! And he is like 8yrs! Small Boy Big thoughts!!!! (Zikiwa kubwa sanaa ndo wanauza sembe na meno ya tembo!) Jirani yangu alikuwa FN manager multinational moja, mshahara 4m na nini, akaacha baada ya miaka kadhaa tu! Kila mtu anamwambia kijana umebugi men! Kuresign ni blander kubwa uliyoifanya! Akawaambia No! Mi sikwenda pale like niwe nimeajiriwa pale like forever! Mpaka nizeeke! Mi nilienda kutafuta MTAJI! Baaaaaaaass! Nyie 3M mnaiona ya maana sanaa bt sio, kwa mwaka its approximately 36m, of wish i wanna make that per month or 2. Hio 36, ukitoa expenses na mda ninaoshinda ofisini, saving ni marginal sanaa! Siku hizi ana yard ya magari, analima huko mkoani, na ku import mavitu toka china! Ametajirika 20 times QUICKER, kuliko alivokuwa multinational. And he is only 34. HE SAW THE BIGGER PICTURE!!!!!!!!!!!!

Bottom line is kama unaweza rudi DSM ucheze na BIG BOYS in the CHAMPIONS LEAGUE!!! ILa kama imekubidi kukaa mkoani usiwaze kimkoa mkoa! THINK BIG ki darisalma darisalama! Ukijihisi umetoka kimaisha njoo town upimishane na uliowaacha ubavu! Itakusaidia kutokurizika na kubakia nyumaaa!

Having said that may i also stress that MAISHA POPOTE! WEWE TU NA AKILI YAKO! ni msemo wenye nguvu ila hufifizwa na mazingira na attitude ya watu waliokuzunguka!

Karibuni kwa HOJA ZENU!
 
Umesema kweli mkuu, kwa sie wataalamu wa kuzunguuka mikoani na wilayani (Vasco da Gama) tumeyaona haya tena unakuta mtu labda ni Afisa nini sijui wa Halmashauri ya Wilaya kila mtu anamwona somebody na wengi wamejisahau, ila kikubwa nilichokusoma lara 1 kwa maneno mengine ishi pale ambapo pana changamoto nyingi bila hofu huku ukiweka miundo mbinu ya kupambana na hizo changamoto na hata kama upo mikoani usibweteke na umaarufu wako maana mikoani kama una nyadhifa flani hawa watu kama wakuu wa mkoa, wilaya na maafisa wengine wa ngazi za mkoa mnakuwa mnaonana nao na kama una issue mbalimbali inakuwa rahisi kupata support sasa kwa favour hizi za mikoani kama hutokuwa makini utajisahau.

Ila mie nakomaa na huku huku mikoani kijijini kabisa Ihayabuyaga kwa malengo ya muda flani then nitaibukia sehemu na investment kubwa si unajua hata mchezaji wa mpira wa miguu kiwango kikiwa si kizuri sana huuzwa kwa mkopo timu nyingine ili apate uzoefu then baadae akirudi kwenye timu yake anakuwa juu, ndo na mie kama nipo kwa mkopo huku Ihayabuyaga najikusanyakusanya ili nitimbe mjini kupambana na changamoto
 
Last edited by a moderator:
Ulichosema ni kwel hata me nina ushuuda mkubwa sana coz nimezaliwa hapa nimesoma hapa na kaz nafanya hapa yani hata kijijini huwa naenda mwezi wa 12 tena kwa matukio maalum. Dar,arusha ,kilimanjaro,mwanza, ndo kila kitu
 
we lara inaonekana uko so addicted with money naona hata jamaa wanaokuzunguka full mapene mwanzo mwisho umenikumbusha dada mmoja anaishi sinza msomi flan iv yaan kupiga naye story tu lazima uwe na hela........ ukiwa huna kitu hta salam yke hupat kibembe akuone unaendesha gari ya gharama jicho litamtoka hilo mixer kuuliza watu jaman yule kaka anafanya kaz wp??? Ngoja cku agundue gari uliazima na una kazi ya kawaida tu dharau na nyodo utakazofanyiwa mbona utajuta,,,,, lara au ndyo ww??????? .......jaman sawa tupende hela lakin cyo kwa kias cha kuwavua utu watu wengine kisa hawana kitu
 

Hahahaaaaaaaaaaa! Thinking is freee!!!!!!!!! Mie hapa sina cha usomi, wala hata 100 sina mission town tu. Wala sipendi pesa! Bt it doesnt mean nayosema ni ya uongo ama hayapo!!!!!!!!!

Afu natoa stori za watu wenye pesa upate INSPIRATION, ningeandika jirani yangu afisa TRA kanikopa misimbazi miwili ungeendelea kusoma hii habari? LOL! Wote tuna shida sema tunajifunza kwa waliotoboa!

BTW mi sina nyodo yoyote coz sina hata 100 bank! Nimechokaaaa!
 
Mbona hata Dar mkoani tu?

Safari ya Korea vipi?

Hahahaaaaa! Sema wewe uliyevuka bakhari, safari ya bado banaaa! Kule inabidi kujipanga sanaaa, sitaki kukurupuka! Sasa kujipanga huku nishaona dalii nitafika 40 sijapangika! lol! zilijaa kidogo nimeuguaaa miez 2. Tutafika mdogo mdogo.
 
Kwa Masikitiko makubwa sana tena sana !! Wewe Lara1 kuishia JF na Oysterbay tu...!!! honestly wewe kwako ni IKULU..Ocean rd. Tungelikwa na presida like YOU. I wish to see you leading our country.
 
Hahahaaaaa! Sema wewe uliyevuka bakhari, safari ya bado banaaa! Kule inabidi kujipanga sanaaa, sitaki kukurupuka! Sasa kujipanga huku nishaona dalii nitafika 40 sijapangika! lol! zilijaa kidogo nimeuguaaa miez 2. Tutafika mdogo mdogo.

Pole.

I hope you are getting back in the swing of things.

Panga game vizuri tu. Hata hapo Dar unaweza kuibua issue wakati unajipanga ukaghairi safari kabisa.Si unaona wakulu wenyewe hawaishi kupishana?

Mara Obama,mara Bush, mara Clinton, mara rais wa China, mara Waziri Mkuu wa Thailand, mara Tony Blair, mara Oprah. Na wengine wanaokuja chini kwa chini ndo usiseme.
 
Mmmh!!!

Kwangu mimi binafsi ninaona kama nje ya Dar es Salaam ndipo kuliko na fursa zaidi kutopoza kiuchumi kuliko hapa jijini.

Kama ningelikuwa nimesoma vizuri uchumi labda hili ningelieleza kwa mapana zaidi maana naamini kuna nadharia zake.

Ugumu wa kutoboza hapa jijini huanzia pale ambapo fursa unayoiona ni lulu, wenzako wanaweza kuiiga na kukupiku kwa uwezo wa shekeli walio nao.
 
Hamza Kalala alitunga wimbo wa 'tutabanana hapa hapa Dar' kwa hiyo hakuna jipya juu ya hilo.

Mimi naona mikoani kuna satisfaction. Mikoani ukitengeneza channel zako za pesa zikakubali watu wanakuwa na attention kwako kishenzi, unaonekana babu kuuubwaa na hii ndiyo raha ya maisha yenyewe, yaani recognition for achievement. Nani asiyependa kujulikana na kusifiwa na kuonekana kijogoo! Mikoani ukizibamba pesa zako unazifurahia na kila mtu anakukubali ni rahisi kuwa celebrity wa huku, ha ha haaa!! Dunia ndiyo ilivyo aliemkoani anamponda wa kijijini, aliye Dar anamdharau wa Mkoa, aliye Dubai anamdharau wa Dar, aliye Japan anamdharu wa Dubai aliye Marekani anamponda alie Japan.

But for sure fursa zipo kila mahari, mtaji mkubwa ni BRAIN yako tu, dunia ya leo huhitaji kuishi DAr ili upate changamoto za kutafuta pesa. Dunia yote iko kwenye kiganja hata aliyeko mkoani unaona wanayoyafanya wengine duniani kote. That is why kuna vijogoo kuanzia bush, small towns hadi big cities kama ambavyo kuna choka mbaya wengi kama sisimizi kwenye miji mikubwa kama Dar. And for your information hakuna sehemu watu wanalalia mabox kwa wingi kama ilivyo Dar! Maisha ya slums huko DAr huwezi kuyaona mkoani, Dar mko kwenye fursa ndiyo lakini wengi pia wanakimbia Dar.

Mifoleni ya magari Dar vipi kila kona ni foleni Dar yooote, inauma na inasikitisha! Hata ukiwa na gari lako Dar hulifurahii!!
 
mimi napendaga tu uandishi wako unapoaanza na igweeeeeeeeeeeeeeee, nakumbuka muvi kinaijeria miaka ya 2002
 
Very true!!! Kuna jamaa mkoa fulani hivi alipata CPA longtime na kwa miaka kibao pale mjini alikuwa CPA holder peke yake na after some years ndio akaongezeka jamaa hazina ndogo nae CPA holder! Basi jamaa mji mzima ikizungumziwa CPA ni yeye tu! Jamaa kabweteka na vijisenti vya huko na sifa kibao (ni kichwa ile mbaya) lakini kiukweli maisha yake hayafanani kabisa na CPA holder wa kipindi chake.

Marafiki wake wengi ninaokutana nao wanasema walikuwa wanamuambia jamaa arudi mjini ili atumie vizuri kichwa chake lakini jamaa hataki!! sasa fainali uzeeni wenzake wako kwenye mashirika ya kimataifa na Government Agency za ukweli na wamejiendeleza sana kielimu wengine hadi PHD while mshikaji yuko halmashauri huko kama CIA anasubiri kustaafu na CPA yake kashakubali matokeo.

Changamoto za mjini zinafundisha sana,daima unajiona upo nyuma kama hupigi hatua vile.
 
Hv si nshwahi sema i lovee this mdadaaaa mi ndo maana wameshaamua kuniiita wa daslam hapa job...mi kila miezi miwili nakuwa nshakata kafast jet kangu ka kwenda na kurudi hata laki haizidi..nkasafishe macho tuuuu
ingawa angalau pesa zangu huku mkoani hazitumiki kivileee kwahiyo napata hata salio la kuinvest
kiroho safiiii
 
mi ndo kwanza naelekea kijijin kulima matango mjin pamenishinda kila kitu hela nani wa hivo bora niende kijijin chakula nachukua shambani maji najichotea tu mton mboga unachoma mwenyewe original kutoka shambani kelele za magari hamna (sitaki shida mimi)
 
Sehemu nyingine ukitembeza nyama choma round za bia kwa sana kwa wapambe then ukiwa na Range Rover tatu na ndege ndogo na nyumba kadhaa basi wewe ni billionaire wakati the number one richest man in Tanzania hajathubutu kujiita billionaire
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…