Zakaria Maseke
Member
- Apr 26, 2022
- 83
- 128
Je, unatamani kusoma sheria au kuwa Wakili, Hakimu au Jaji? Hongera! Soma vigezo na mlolongo wote hapa chini.
Imeletwa kwako nami Zakaria Maseke (Advocate /Wakili )
0754575246 - WhatsApp.
Tuanze na sifa au vigezo vya kusoma sheria
(i) : Kwa ngazi ya shahada (degree).
- Ukitaka kusoma degree ya sheria na umehitimu SECONDARY kidato cha sita (6), unatakiwa uwe umefaulu masomo mawili, kiingereza na historia, uwe walau na “D" mbili na kuendelea. Na kama hujasoma na kufaulu History na English A - LEVEL (KIDATO CHA SITA), labda umesoma sayansi (PCM, PCB, CBG n.k) au umesoma History na English A Level lakini hujafikisha alama “D” ya masomo hayo, na unatamani kusoma sheria, basi uwe una credit ya history na kiingereza kule O level, yaani uwe umeyafalu kwa kiwango cha alama “C” na kuendelea kule kidato cha nne (4).
NB: Kwa kuwa sasa Kiswahili ni lugha rasmi ya Mahakama na sheria zote zinatakiwa kuandikwa kwa Kiswahili, HUENDA wanaotaka kusoma sheria wakatakiwa kufaulu na kiswahili.
-Kama unatokea Diploma, uwe na GPA ya 3.0
(ii) Kwa ngazi ya DIPLOMA (stashahada).
- Ukitaka kusoma diploma ya sheria inategemea una elimu gani:
-Kama umemaliza kidato cha sita uwe na cheti cha form six na walau principal pass moja (D), Subsidiary (S) moja na angalau ‘D’ nne (four passes) za kidato cha nne, ila isiwe za masomo ya dini. NB: Somo moja liwe ni somo la kiingereza (English), na
-Au uwe umehitimu certificate ya Sheria (Certificate in Law (NTA Level 4).
(iii) Kwa ngazi ya CHETI.
Ukitaka kusoma certificate ya sheria unatakiwa uwe na cheti cha kidato cha nne na ufaulu wa angalau ‘D” nne, mojawapo iwe ni ya somo la English.
2: Kama una hizo sifa, hatua inayofata ni kutuma maombi kuchagua chuo unachotaka na kwenda kusoma. Utachagua mwenyewe unataka kuanzia cheti (certificate), stashahada (diploma) au shahada (degree). Kulingana na matokeo yako.
Mfano kama umehitimu na kufaulu kidato cha sita, utaenda chuo kikuu kusoma shahada (degree). Kama umefeli au kama marks hazitoshi kwenda chuo kikuu, utaenda kusoma cheti au diploma na baadae utaunganisha hadi degree ukitaka.
Muda wa kusoma inategemea na level uliyopo (unasomea cheti, diploma au degree). Mathalani, certificate ni mwaka mmoja, diploma ni miaka miwili na degree miaka mitatu au minne (inategemea umeenda chuo gani). Ukimaliza hapo umekuwa mwanasheria lakini sio Wakili.
Unawezaje kuwa Wakili? Au Hakimu? Au Jaji? Kwa sababu Mahakimu na Majaji wanachaguliwa kutoka kwenye watu wenye sifa za kuwa Wakili, basi tutajikita kuangalia mchakato wa kuwa Wakili.
MCHAKATO WA KUWA WAKILI.
Sifa na Mchakato wa kuwa Wakili nchini Tanzania (Bara) unapatikana kwenye Sheria ya Mawakili (The Advocates Act) na Sheria ya Shule ya Sheria Tanzania (The Law School of Tanzania Act).
MCHAKATO WA KUWA WAKILI KABLA YA KUANZISHWA KWA SHULE YA SHERIA KWA VITENDO (LAW SCHOOL), 2007.
Kwa sababu Law School imeanzishwa mwaka 2007. Watu waliosoma shahada (degree) ya sheria kabla ya mwaka 2007 walitakiwa kufata utaratibu ufuatao ili kuwa Mawakili.
1: Uwe na shahada ya Sheria (LLB).
2: Kufanya mafunzo (internship) kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na kwa Wakili wa kujitegemea.
3: Kutuma maombi kwa Jaji Mkuu.
4: Kufanyiwa interview (bar examination) mbele ya Baraza la Elimu ya Sheria / Council of Legal Education (CLE).
5: Kufanyiwa interview mbele ya Jaji Mkuu (Chief Justice).
6: Kuapishwa (admission)
7: Kuandikishwa jina (enrollment) kwenye orodha ya Mawakili (Roll of Advocates).
MCHAKATO WA KUWA WAKILI BAADA YA KUANZISHWA KWA SHULE YA SHERIA KWA VITENDO (LAW SCHOOL), 2007.
Kwanza tufahamu, “Law School ni nini?” Hiki ni Chuo cha Uanasheria kwa vitendo ambacho kinatoa mafunzo yanayolenga kumuandaa mhitimu wa shahada ya kwanza ya sheria (LLB) kufanya kazi ya Uwakili (Uhakimu, Jaji n.k)
Je, ni lazima kwenda Law School? Inategemeana. Lakini jibu la jumla, kama unataka Kuwa Wakili, Hakimu au Jaji wa Mahakama nchini Tanzania, kwenda Law School ni lazima.
Sasa kwa nini nasema inategemeana? Ni akina nani wanaweza kuwa Mawakili au kufanya kazi za Mawakili bila kupita Law School?
Kufatia Marekebisho ya Sheria ya mwaka 2020 (The written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3), Act 2020) yaliyorekebisha Sheria ya Shule ya Sheria Tanzania (Law School of Tanzania Act), sheria inatoa msamaha kwa baadhi ya wanasheria wenye vigezo maalum, ambao kwa mujibu wa Sheria walipaswa kupititia Law School, lakini kutokana na nafasi zao katika Utumishi wa Umma hawawezi kuhudhuria mafunzo hayo. (Hasa watumishi wa Mahakama na wanasheria kwenye ofisi za umma, unatuma maombi kwa Waziri husika unasamehewa kwenda law school). Soma PART XI section 42 ya amendments.
Lakini, kiujumla, kwa ambao wamehitimu shahada ya sheria baada ya mwaka 2007, wanatakiwa kufata utaratibu ufuatao ili kuwa Wakili.
1: Uwe na shahada ya Sheria (LLB). Soma section 8(1)(a)(i) ya Sheria ya Mawakili na Section 11(1) ya Law School of Tanzania Act.
2: Kuhudhuria mafunzo ya sheria kwa vitendo (Post Graduate Diploma in Legal Practice) katika shule ya sheria kwa Vitendo (Law School). Section 12 ya Law School of Tanzania Act, CAP 425.
Kwa wale ambao hawana hizo sifa (labda sio Wakili Mtanzania au ulisomea Uwakili nje ya nchi), mbadala wake ni ‘uwe mwanasheria anayeruhusiwa kuingia Mahakamani kutoka nchi ya jumuia ya madola au nchi yoyote kama itakavyoelekezwa na Waziri husika.’ Section 8(1)(a)(ii) ya Sheria ya Mawakili.
Au ‘uwe ni Wakili katika Mahakama za Uingereza au umeruhusiwa kuwa Wakili kwa mujibu wa sheria za Uingereza.’ Section 8(1)(a)(iii) ya Sheria ya Mawakili
Au, ‘umekidhi vigezo, mfano kupitia maelekezo maalum au mitihani ya kukuwezesha kupata uzoefu wa taaluma ya sheria kwa kuzingatia taratibu za Baraza la Elimu ya Sheria Tanzania (Council of Legal Education).’ Section 8(1)(a)(iii) ya Sheria ya Mawakili.
Au, ‘uwe umekuwa ukifanya kazi za Uwakili nchini Kenya, Uganda au Zanzibar kwa miaka mitano.’ Section 8(1)(a)(iii) ya Sheria ya Mawakili.
3: Hatua ya tatu (ukimaliza law school) ni kutuma maombi (petition) kwa Jaji Mkuu kuomba kuapishwa au kupokelewa (admission) kwenye jumuia ya Mawakili, ukiambatanisha na hati ya tabia yako (certificate of character) na kulipia malipo yanayotakiwa. Section 8(2) ya Sheria ya Mawakili.
Viambatanisho vingine ni kama:
(i) Cheti cha kuzaliwa
(ii) Vyeti vya sekondari (kidato cha nne na cha sita) au diploma.
(iii) Cheti cha taaluma na matokeo yako ya Chuo Kikuu.
(iv) Cheti cha taaluma na matokeo yako ya Law School
(v) Barua ya utambulisho kutoka kwa mwajiri kama umeajiriwa.
(vi)
4: kuapishwa (admission) au kupokelewa na kupewa cheti (certificate of admission). Cheti hiki bado sio leseni ya Kuwa Wakili.
Section 8(3) & (3A) ya Sheria ya Mawakili.
5: Kuandikishwa jina lako (enrollment) kwenye orodha (Roll) ya Mawakili na Msajili wa Mahakama Kuu, kulipia na kupewa cheti cha kufanya Uwakili (Practicing Certificate). Section 8(4) & 35 ya Sheria ya Mawakili.
NB: Mawakili wanapeana vipaumbele (heshima) kulingana na muda ulioandikisha jina lako kwenye Roll, wa kwanza kukutangulia kuandikishwa ndiye mkubwa (SENIOR) wako na akifika Mahakamani inabidi asikilizwe kwanza. Hivyo kuna Seniors na Juniors.
Huku ukubwa sio suala la umri ni suala la kutangulia kuwa Wakili. Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, anabaki kuwa Wakili namba Moja (mkubwa) wa Mawakili wote, hata kama ameteuliwa leo au ulimtangulia kuapishwa.
GHARAMA ZA KUAPISHWA KUWA WAKILI BAADA YA KUFAULU LAW SCHOOL:
Hii ni kwa mujibu wa uzoefu wa Admission zilizopita mpaka December 2023. Itakusaidia kujiandaa kiasi fulani, kukiwa na ongezeko utajulishwa na wahusika.
1: JUDICIARY FEES = 110,000/=
(mnyambuliko wa hiyo judiciary fees ni
-Admission Fee : 20,000/=,
-Practicing Fee : 50,000/= na
-Notary Public & Commissioner for Oath Certificate : 40,000/=.
{Sub total judiciary fees = 110,000}.
2: TANGANYIKA LAW SOCIETY FEES = 396,000/=
(mnyumbuliko wa hiyo TLS fees ni
-Annual subscription fee : 80,000/=
-Deceased Advocates Trust Fund (DATF) - 50,000/=
-Legal Aid Advocacy Centers (LAACs) Wakili house : 200,000/=
-East Africa Law Society : 46,000/=
-Identity Card : 10,000/=
-Journal : 10,000/=
3: TLS AND JUDICIARY SEMINAR
(Seminar before Admission) : 130,000/=
4: STAMPS (MIHURI)
Inategemea unataka Desk au Pocket:
Gharama ya Desk Stamps
-Desk Certification : 72,000/=
-Desk Notarization: 72,000/=
Gharama ya Pocket
-Pocket Certification : 67,000/=
-Pocket Notarization : 67,000/=
Mihuri yote hiyo ni Electronic na unaweza kuamua kuchukua desk au pocket peke yake au yote minne desk 2 na pocket 2.
-Ink (wino ni automatic) : 10,000/= ukitaka unaweza kuagiza wino zaidi ya chupa 1. Kila chupa moja 10,000.
NB: Gharama hizi zinaanza kulipwa soon (punde) tu baada ya kutoka ku appear mbele ya Jaji Mkuu (CJ) for interview.
Kwa upande wa mihuri unaagiza baada ya kuapishwa na CJ.
5: GHARAMA BINAFSI:
Joho: 100,000 au 150,000 au 200,000 etc.
Bib: 10,000 au 15,000 n.k.
Suti: 100,000 au 200,000, 300,000 n.k. kutegemea na uwezo wako.
Picha:
Make-up
Nywele
Usafiri
Cake if any
Sherehe if any n.k.
Kadiri utakavyokua na mambo mengi ndivyo na gharama zinaongezeka.
Kwa ujumla, hizo ndizo sifa, vigezo na mchakato wa kuwa Wakili nchini Tanzania (kwa upande wa Tanzania Bara).
Kumbuka: Ili kufanya kazi za Uwakili unatakiwa uwe umesoma na kufaulu, umeandikishwa jina lako kwenye daftari la orodha ya Mawakili (your name is on the Roll of Advocates), uwe na kibali cha kukuruhusu kufanya kazi ya Uwakili (you have IN FORCE a practising certificate), na uwe na leseni ya biashara (a VALID business licence).
Zingatia, Sheria inasema IN FORCE practicing certificate. Kama una Kibali ila hujakilipia na kukihuisha (ku renew) kila mwaka, huo muda ambao huja renew wewe ni Wakili lakini huruhusiwi kufanya kazi za Wakili.
Kwa ujumla, kama huna hizo sifa zote hapo juu, sheria inakutambua kama “UNQUALIFIED PERSON”. Hauruhusiwi kuwakilisha mtu kwenye kesi Mahakamani, kushuhudia viapo, mikataba na kusaini nyaraka zozote kisheria. (SECTION 39 YA SHERIA YA MAWAKILI)
Mteja, kama utawakilishwa na Wakili ambae hana hizo sifa mfano haja renew hata leseni au kibali, Wakili mwenzake ataweka pingamizi au Mahakama yenyewe ikigundua, huyo Wakili atasimamishwa hapo hapo kuendelea na hiyo kesi, na nyaraka zote alizokuandalia na kesi yote ilipofikia vitatupiliwa mbali, maana vimeandaliwa na mtu ambaye hana sifa.
Utajuaje Wakili wako anaruhusiwa au Haruhusiwi? Ni rahisi sana, chukua simu janja, ingia mtandaoni andika “eWakili”, huu ni mfumo wa kuwatambua Mawakili. Andika jina lake hapo, taarifa zake zitakuja kama anaruhusiwa au haruhusiwi.
Sasa Je, unajua Wakili anaweza kusimamishwa Uwakili kwa muda au kufutwa kabisa Uwakili maisha yake yote? Ikitokea Wakili amesimamishwa au kufutwa Uwakili jumla, anaweza kufanya nini? Nini Wajibu na haki za Wakili? Mambo gani Wakili haruhusiwi kufanya? Ni wapi na akina nani wanaweza kumwajibisha Wakili? Sheria gani zinatumika? Na adhabu zipi zinaweza kutolewa? Kwa hayo yote na mengine mengi tukutane kwenye Makala nyingine.
Natoa angalizo, wale wazee wa kukopi machapisho ya watu na kuweka majina yenu. Ni kosa kisheria. Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejimilikisha andiko hili.
Unaruhusiwa kabisa kushare lakini usihariri (ku edit) yaliyomo. Ni heri uanze kuandika ya kwako mpya.
Imeandaliwa na kuletwa kwako nami ZAKARIA MASEKE (Advocate /Wakili - 0754575246 WhatsApp).