Kwa bahati mbaya ushindi wa Shein haukuja kwa uanasiasa bora bali ni uchaguzi tu wa CCM ulioangalia masilahi ya Chama chao na wala sio walengwa (Wazanzibari). Amekuwa kwenye madaraka ya juu karibu miaka saba sasa na hajafanya lolote linaloweza kuonekana limesaidia Wazanzibari.Hali hii pia iko kwa wagombea wenzake, walishakaa kama mawaziri Viongozi kwa vipindi vya miaka kumi kumi na hawana la kuonyesha juu ya maendeleo ya visiwa hivyo, nao pia walipewa nafasi kubwa na CCM jambo linalothibitisha kuwa walifanya kazi nzuri kwa chama chao na sio kwa Wazanzibari. Wazanzibari walihitaji wagombea wengine zaidi ya hawa watatu ambao walishapata nafasi na hawakuleta maendeleo!Swali lina kuwa gumu kwa sababu una uliza mwanasiasa huyu ana sifa zipi zinazo mfanya aonekane kiongozi bora. Ubaya ni kwamba kwenye siasa mtu hashindi kwa kuwa kiongozi bora bali ana shinda kwa kuwa mwanasiasa bora. Ndiyo maana tunaona wimbi la watu wanaoweza siasa lakini si viongozi wakipanda vyeo na wale wanaojua uongozi lakini si wazuri kwenye siasa wakikosa nyadhifa. Ni vigumu sana kukutana na mtu ambae ni mwanasiasa mzuri na kiongozi mzuri kwa wakati mmoja na mara nyingi kama tunavyo ona kwetu mambo hayo mawili hayaendani.
NgekewaKwa bahati mbaya ushindi wa Shein haukuja kwa uanasiasa bora bali ni uchaguzi tu wa CCM ulioangalia masilahi ya Chama chao na wala sio walengwa (Wazanzibari). Amekuwa kwenye madaraka ya juu karibu miaka saba sasa na hajafanya lolote linaloweza kuonekana limesaidia Wazanzibari.Hali hii pia iko kwa wagombea wenzake, walishakaa kama mawaziri Viongozi kwa vipindi vya miaka kumi kumi na hawana la kuonyesha juu ya maendeleo ya visiwa hivyo, nao pia walipewa nafasi kubwa na CCM jambo linalothibitisha kuwa walifanya kazi nzuri kwa chama chao na sio kwa Wazanzibari. Wazanzibari walihitaji wagombea wengine zaidi ya hawa watatu ambao walishapata nafasi na hawakuleta maendeleo!
Si kwamba kila atakae pitishwa na CCM ndiyo lazima achaguliwe, hili litabaki swali kwa Wanzinzibari kuwa Shein aliwanyia nini since 2001 alipokua makamu na wanategemea awafanyie nini kama watamchagua awe rais wa Zanzibar kwa miaka Mitano ijayo au Kumi ijayo kama itikadi ya kuachana vipindi viwili haitakoma.
Ukweli kwamba Shein pale kawekwa upo wazi, hakuipigania nafasi yake kuna watu wanaomtaka awe pale hata katika hotuba yake alisema atalinda Muungano na Sera ya CCM ndo itakua muongozo wake. So hizi sera zipo tangu siasa zimeanza na Muungano upo tangu mwaka 64 ila maendeleo yana hali gani??? hali ya uchumi wa Zanzibar na wa Wazanzibari upo vp?? Hajasema nini mipango yake kwa wazanzibari.
Kwa ufupi ni jukumu la Wazanzibari kuwaonyesha wale waliomuweka Shein pale sio wenye sauti ya Mwisho ndani ya Zanzibar ila Wazanzibari ndio wenye uamuzi wa mwisho. kama walivyomtaka Shein na wakampitisha kwenye chama chao nanyi mnaweza kutumia haki yenu ya Msingi kutomchagua then tuone watafanya nini.
October 31 ndo itamuua.
hana chokochoko za KiungujaHaya tena wanajamii CCM imetowa uamuzi utakaogusa mustakbali wa nchi kwa kumteua Dr. Shein kuwa mgombea wa urais wa sehemu moja ya Muungano (Zanzibar)
Tulisikia mengi kutoka kwa wana CCM wenyewe kuhusu nafasi hiyo ilo ikigombaniwa na watu 11. Katika hatuwa ya mwisho majina matatu yalipigiwa kura na matokeo Dr. Shein kuwashinda Dr. Bilali na Shamsi Nahodha. Nimekuwa najiuliza wakubwa wa CCM walitumia vigezo gani vya kuwanufaisha Wazanzibari kwa uamuzi wao?
Ama kwa mimi naona hawa watatu hawana tofauti kati yao kwa maslaha ya Wazanzibari. Naomba ukumbi unisaidie kuiondowa hofu yangu hiyo!
Hana sifa zozote zaidi ya kuwa ni "mtu wa watu." CCM iliizima debate kati ya wagombea wa nafasi ya urais kule Zenj. Hii ingesaidia kuona kwa kiasi kikubwa tofauti ya sera kati ya wagombea wale lakini kwa kuwa tayari kuna usanii wa hali ya juu katika kupata wagombea ndani ya chama hicho basi hawakuona umuhimu wa kuwa na mdahalo. Si ajabu kabisa CCM tayari ina majina ya nani ambao watastahili kumrithi Kikwete 2015 na nani ambao watastahili kupewa nafasi ya mgombea mwenza toka visiwani mwaka huo.