MwanaPekee
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 382
- 385
Kwa muda mrefu nimekuwa nikimfuatilia ndugu yetu na Mtanzania mwenzetu Bernard Membe katika harakati zake za kuutafuta Urais wa JMT. Kwa sasa nimefanikiwa kung’amua sifa zake tano (5) ambazo binafsi naona kabisa kuwa zinamfanya asiwe mtu sahihi kwa nafasi hiyo kubwa na takatifu. Sifa hizo ni kama ifuatavyo:
Amekosa unyenyekevu: Miezi iliyopita katika mitandao ya kijamii ulisambaa ujumbe wa sauti, Ndugu BM akiwa anamsema vibaya Rais wa nchi na viongozi wengine wa CCM. BM alikubali kuwa sauti katika ujumbe huo kweli ni yake, lakini akabaki na msimamo wake kuwa hawezi kumuomba mtu radhi sababu hajakosea chochote. Ameendelea kutunishiana misuli na viongozi wa Chama hadi walipofikia hatua ya kumvua uanachama. Binafsi naona kuwa alikosa tu sifa ya unyenyekevu na kuomba radhi ili maisha mengine yaendelee kama kawaida.
Mjivuni: Hivi karibuni BM akiongea na baadhi ya watu wa Mkoa wa Lini alisikika akisema uchaguzi huu bila yeye kuwapo utakosa mvuto. Alisema kuwa yeye pekee ndiye “Mnogeshaji”. Logically ni kuwa hakuona mtu mwingine yeyote nchini, mwenye sifa kama zake au kumzidi yeye ambaye anaweza kunogesha uchaguzi wa mwaka huu. Huo ni ujivuni na kujiona yeye ni bora kuliko Watanzania wengine wote.
Mtu wa masharti mengi: BM akiongea na watu hao alitoa sharti kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimsafishe ili aweze kuchukua fomu za kuwania nafasi ya kugombea Urais wa JMT, vinginevyo angefanya maamuzi mengine. Pili, juzi ametoa sharti kwa vyama vya upinzani kuungana ili awe mgombea wao. Binafsi naona kama ni mtu anayependa kutoa masharti mengi ili atekeleze jambo fulani. Wananchi tunakuwa katika wakati mgumu maana tutakiwa kutimiza masharti yake ili tu atuletee maendeleo.
Mvunja sheria: Kwa nafasi yake na uzoefu wake katika siasa alipaswa kujua kuwa muda wa vyama kuungana na kusimamisha mgombea mmoja umepita, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 na kufanyiwa Revision 2019. Sheria inataka vyama kutoa taarifa ya kuungana miezi mitatu kabla ya Uchaguzi, na lazima azma hiyo iridhiwe na Mkutano Mkuu wa Kila Chama kinachoungana. Tafsiri ya Uchaguzi ni kuwa ni mchakato unaoanza pale vyama vinapoanza Kutafuta Wagombea na unahitimishwa pale Mshindi Anapotangazwa. Hivyo vyama vimechelewa kuungana, BM analazimisha kutokea uvunjifu wa sheria kwa faida zake binafsi.
Opportunist: Mfumo wa Tume ya Uchaguzi, hasa namna inavyopatikana na wajumbe wake haujaanza leo, au awamu hii ya uchaguzi. Malalamiko ya vyama vya upinzani kudai kile wanachodai kuwa ni Tume Huru hayajaanza awamu hii. Mwaka 2015 BM alipokuwa akiona kuwa ana nafasi kubwa ya kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM, Tume Huru haikuwa agenda kwake. Hivyo hivyo kwa miaka ya nyuma ambapo yeye alikuwa akitangazwa na Tume hii hii kuwa mshindi wa Ubunge. Swali la kujiuliza, ni kipi ambacho leo kimemfanya aone kuwa Tume ina mapungufu ikiwa miaka yote amekuwa kimya? Binafsi naona kuwa ni mtu anayetafuta fursa kwa manufaa binafsi. Kwake ameona ili aweze kupokoleka Upinzani basi aimbe wimbo wao, ikiwa miaka mingine yoyote amekuwa akiuona huo wimbo kuwa ni kelele.
HITIMISHO

Watanzania tunapaswa kuwa waangalifu sana na aina ya viongozi tunaowachagua. Ni wakati sasa kwetu sisi wanachama wa vyama hivi vya upinzani kupaza sauti kubwa ya Kuwakataa watu kama hao, ambao wanatoka kwenye vyama vyao katika hatua za mwisho za uchaguzi, na baada ya uchaguzi wanatugeuka na kurejea tena huko walikotoka, maana kimsingi ndiko iliko historia yao ya Siasa, na mtu hawezi chafua legacy yake kirahisi hivyo.