Sifa kuu za kabila la Kinyakyusa

Kwa walioolewa na wanyakyusa, Ogopa mtu Wifi. Atajifanya wifi wifi kumbe anatembea na mumeo au mshenga wa mumeo. Mawifi wa kinyakyusa ni balaa usimpe nafasi.
wanaume ndo waamuzi wa maisha yao, sioni shida hata mtu akiwa na wifi wa uongo
Kama umeolewa na bomu ni bomu tu haijalishi ni kabila gani
 
Huu ni mjadala umeanzisha watu tutoe maoni yetu we vipi ulitaka tusifie tu. Watu tuna maoni tofauti eti. Basi usingeweka hapa.
 
Kwa wanyakyusa imezidi. Siyo wote lkn asilimia kubwa wako hivyo. Ni kama wanavyosema wachaga wa machame wako hivi.... Nao siyo wote ila asilimia kubwa wanatabia hiyo.
Mwanamke wa kinyakyusa kuwekwa nyumba ndogo kwake ni ufahari.
kwa wanawake asilimia kubwa wanashindana, kumpiku mwenzie au kuchukua nafasi ya mwenzie huwapa mawazo kwamba wao wazuri zaid kuliko mwenzao. Ni tabia IPO haijalishi kabila
 
kwa wanawake asilimia kubwa wanashindana, kumpiku mwenzie au kuchukua nafasi ya mwenzie huwapa mawazo kwamba wao wazuri zaid kuliko mwenzao. Ni tabia IPO haijalishi kabila

Daima mshindi anakuwa namba moja na siyo namba mbili. Kama wapo mashindanoni ajitahidi awe mke wa kwanza basi. Kwanini watake kuwekwa vimada, wawe wanatoka kwa kufichwafichwa. Unapangiwa muda wa kumpigia simu n. K? Why?
 
Huu ni mjadala umeanzisha watu tutoe maoni yetu we vipi ulitaka tusifie tu. Watu tuna maoni tofauti eti. Basi usingeweka hapa.

Hiyo topic ni swali kwa wanyakyusa wenyewe kama jamii sio wanawake au wanaume au vikundi vidogo vidogo ndani ya jamii yao. Wengine huwa hamridhiki wengine wakiongelewa vizuri lakini hiyo imewekwa mpaka source yake hapo. Ingekuwa inaongelea sifa nzuri na mbaya sawa ongeza mbaya unazijua lkn hiyo ni makala imekopiwa kama ilivyo fuata link uka update hizo sifa zingine walizosahau
 
Wanyakuyusa wanajulukana sana kwa tabia ya ubaguzi na kupenda misifa..

Mbona hujaweka???
Nadhani huwafahamu Wanyakyusa,Wanyakyusa ni watu wanapenda freedom na kuthamini utamaduni wao.Mnyakyusa haoni aibu kuongea kilugha popote pale,wako so confident na hii ndio huwafanya watu kama wewe kudhani ni wabaguzi which is wrong!
 

Wewe si umeiweka hapa nami naongezea hapahapa nilipoiona.
Kila kizuri hakikosi kasoro na zipo nyingine nyingi tu. Usipende sifa tu. Ukweli ndo huo.
 

Mwamushi, Mwamrema, Mwakavishe, Mwatarimo n.k
 
Daima mshindi anakuwa namba moja na siyo namba mbili. Kama wapo mashindanoni ajitahidi awe mke wa kwanza basi. Kwanini watake kuwekwa vimada, wawe wanatoka kwa kufichwafichwa. Unapangiwa muda wa kumpigia simu n. K? Why?
hayo ni maamuzi binafsi ya mhusika, sio wanawake wote wanaotaka majukumu makubwa ya mke wengine ndo maisha waliyojopangia na wameridhika labda kuwa hivyo. Sio suala la kabila fulani, wanawake walioolewa na mi wa kabila Hilo si wapo. Ujinga wa wanaume anampangishia nyumba na kutoa kila mchango ktk nyumba ndogo wakati Ana familia inayomtegemea unadhani kuna anayepoteza nafasi ya kuhudumiwa bila majukumu mazito
 

Nakubaliana na wewe kabisa kuna watu wanaopenda hivyo, na hiyo ndiyo tabia ya wanawake wa kinyakyusa. Si tabia nzuri sasa unakasirika nini?
 
Haya naona unataka pa kuegemea ili utoe jazba zako dhidi ya Hilo kabila. Si unashindana na Wikipedia, endelea. The source remains as it is.
Wewe si umeiweka hapa nami naongezea hapahapa nilipoiona.
Kila kizuri hakikosi kasoro na zipo nyingine nyingi tu. Usipende sifa tu. Ukweli ndo huo.
 
Wanawake wa kinyakyusa wamekuchanganya sana naona, endelea. Ukimaliza wafuate wikipedia
Nakubaliana na wewe kabisa kuna watu wanaopenda hivyo, na hiyo ndiyo tabia ya wanawake wa kinyakyusa. Si tabia nzuri sasa unakasirika nini?
 
Mbona hamuwalaumu akina mangi wakiwachukua ndugu zao kuuza maduka. Kama mtu amesomea kazi husika umuache kwa sababu ni kabila lako watasema tu. Kuna shirika lililokufa kwa sababu wote akina mwa mwa... Sio tabia nzuri kwa vile kuna watu wanakosa nafasi lakini kama wamesoma basi Hanna shida. Mbona Japan walikuwa wana ajiri kwa kuuliza mpaka blood group.
Mwamushi, Mwamrema, Mwakavishe, Mwatarimo n.k
 
1)WANAAMINI KABILA LAO NDIO BORA KULIKO YOTE

Wanaamini kabila lao ni bora kuliko yote na ni lazima kila Mtanzania ajue kabila hilo na kama kuna mtu ambaye halijui basi mtu huyo ni jeuri/kiburi pia ana dharau.


2)WANAJIAMINI SANA


Ni watu wanaojiamini sana hususani sehemu za kazi,wakipewa jukumu fulani kulifanya wanafanya kwa kijiamini sana na huwa hawapendi kuingiliwa 'as long as umempa afanye kitu fulani wanaamini kuwa umemchagua/umemteua yeye sababu unaamini kuwa anaweza kufanya kitu hicho so asiingiliwe mpaka amalize.

3)WANAPENDA ATTENTION


Ni watu wanaopenda sana kuonekana kwa kile wanachokifanya,yaani wanapenda kuonekana na kuthaminiwa kwa kile wanachokifanya na sio zaidi ya hapo tofauti na makabila mengine.


4)NI WACHAPA KAZI


Ni watu wanaojituma sana katika kufanya kazi,mara zote huwa hawapendi kuonekana kazi fulani imewashinda kufanya kwasababu wao wanaamini kuwa kushindwa kuperform vizuri kitu ulichoaminiwa ni AIBU na UDHAIFU mkubwa sana katika maisha.


5)WAKARIMU


Ni watu walioumbwa na karima ya hali ya juu,yaani wanapokea mtu yoyote hata kama hawajui alikotokea ndio kitu kilisababisha mpaka kukawa na matukio ya ajabu ajabu sababu ukarimu huo watu wenye nia mbaya waliutumia katika kufanyia maovu yao.


6)WANASUBIRA


Ni watu ambao hawana papara,huwa hawapendi kukurupuka kwa kitu chochote,wanapenda kungojea mpaka mpaka wapate hali halisi ya kitu chenyewe ndio wafanye maamuzi.

SIFA ZA ZIADA


a)UTANASHATI


UTANASHATi na usafi ni sifa nyingine muhimu kwa kabila hii. Waweza fika kijijini ukakuta bibi na kijumba chake lakn vyombo vyake viko safi kabisa. Wawezakupataka chungu anachopikia usipate masizi


b)HAKI NA SHERIA

Wanyakyusa kwa malezi yao WANAPENDA HAKI NA KUFUATA SHERIA.

C)UMOJA


UMOJA ni sifa nyingine ya msingi: Si msibani tu Wanyakyusa wakoPAMOJA sana kwa kila kitu. Hata mgonjwa akisafirishwa hadi kwa mganga au hospitali kwa kushirikiana (palutato) wanashirikiana pamoja, Uzalishaji mali ndiyo usiseme- Walilima/wanalima kwa pamoja (INDUULA/INDIMYA), na ng'ombe walichunga/wanachunga pamoja (ULUTIIMO),mambo ya furaha kama harusi ndo usiseme,yaani wanahakikisha kwa umoja wao sherehe inafana.
Na wewe ongezea mengine.
 
So what? Bado unavalue kabila tu dunia ya leo? Kazi ipo.
 
mh!nina miaka 14 nikiishi mji huu lakini nahisi huu uzi ni MAKE UP tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…