Sifa moja muhimu zaidi kuhusu kumiliki fremu za biashara kwa ajili ya kupangilia

Aliko Musa

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2018
Posts
209
Reaction score
315
Kutengeneza kipato cha majengo ni moja ya njia ya kujenga utajiri. Njia hii ya kumiliki majengo ya biashara ya kupangisha imeonyesha ufanisi mkubwa kuwasaidia wengine kujenga utajiri.

Kipato cha majengo ya biashara ni kizuri ukilinganisha na faida ya kununua na kuuza ardhi. Tofauti ya kipato cha majengo na faida ya kuuza ardhi/jengo kwa muda mfupi ni;-

✓ Kipato cha majengo huendelea kuingia ukiwa umelala (endapo utajiri msimamizi wa majengo ya kupangisha). Wakati huohuo, faida ya kuuza ardhi unapata mara moja tu (wakati wa kuuza ardhi).

✓ Kipato cha ardhi hitaji kiasi kidogo sana cha muda na maarifa wakati wa usimamizi ukilinganisha na faida ya kununua na kuuza ardhi/majengo.

✓ Faida ili iwe kubwa sana, unatakiwa kuendelea kutafuta viwanja, kuvitangaza na kuviuza kwa faida kubwa. Hivyo, kazi kubwa inatakiwa iendelee kufanyika kwenye maisha yako yote ikiwa utaamua kutengeneza fedha kwa FAIDA YA KUUZA VIWANJA.

✓ Kuanza kutengeneza faida ya kuuza viwanja inahitaji kiasi kidogo cha mtaji fedha ukilinganisha na kuanza kutengeneza kipato endelevu cha majengo ya kupangisha.

Makundi 5 Ya Majengo Ya Biashara.

Majengo ya biashara ni majengo ambayo yamejengwa na hutumiwa kwa ajili ya kuwezesha biashara za huduma na biashara za bidhaa. Majengo ya familia nyingi na apatimenti kubwa hutumika kwa ajili ya huduma za makazi/malazi.

Lakini kwa sababu mmiliki huendesha kibiashara apatimenti kubwa/majengo ya familia nyingi ndio maana huingia kwenye majengo ya biashara. Makundi haya matano ya majengo ya biashara ni;-

(1) Majengo ya ofisi (Office buildings).

(2) Majengo ya ghala/stoo/bohari (Warehouse).

(3) Fremu za biashara (Retail buildings).

(4) Majengo ya viwanda (industrial buildings).

(5) Majengo ya familia nyingi (Multifamily buildings).

Kupangisha fremu za biashara kunaweza kuwa njia nzuri ya kuanzisha biashara ya kupangisha mali. Hapa kuna hatua kadhaa za kufuata ili kuanzisha biashara ya kupangisha fremu za biashara:

(1) Tafiti Soko.

Tafiti eneo ambalo unataka kupangisha fremu za biashara. Jua ni aina gani za biashara zinahitajika zaidi katika eneo hilo na bei ya soko kwa fremu hizo.

(2) Pata Leseni na Vibali.

Hakikisha unapata leseni zote na vibali vinavyohitajika kuendesha biashara ya kupangisha mali katika eneo lako. Hii inaweza kujumuisha leseni ya biashara na kibali cha ujenzi.

(3) Nunua au Jenga Mali.

Nunua au jenga fremu za biashara katika eneo lenye mahitaji. Hakikisha mali hizo zinakidhi mahitaji ya wapangaji watarajiwa na zina miundombinu muhimu kama maji, umeme, na usalama.

(4) Tangaza Biashara Yako.

Tangaza fremu zako kupitia njia mbalimbali kama vile magazeti, mitandao ya kijamii, na mabango ili kuvutia wapangaji. Unaweza pia kushirikiana na madalali wa mali ili kusaidia kupata wapangaji.

(5) Weka Mkataba wa Kukodisha.

Tengeneza mkataba wa kukodisha wenye masharti wazi na haki na wajibu wa mpangaji na mwenye nyumba. Hakikisha mkataba huu unakubalika kisheria na unalinda maslahi yako.

(6) Ubora Wa Huduma kwa Wapangaji.

Toa huduma bora kwa wapangaji wako ili kuhakikisha wanaridhika na wanakaa kwa muda mrefu. Huduma hizi zinaweza kujumuisha matengenezo ya mara kwa mara na usalama wa mali.

(7) Usimamizi wa Fedha.

Hakikisha una usimamizi mzuri wa fedha zako. Weka kumbukumbu za mapato na matumizi na hakikisha unapokea kodi kwa wakati. Unaweza kutumia programu za usimamizi wa mali kusaidia katika hili.Kwa kufuata hatua hizi, utaweza kuanzisha na kuendesha biashara ya kupangisha fremu za biashara kwa ufanisi.

Sifa Moja Muhimu Ya Fremu/Ofisi Za Biashara.

Kuwa njia au barabara ambayo inapitisha idadi kubwa ya watu. Kiwango cha wapitaji (traffic) ni sababu muhimu sana unapochagua kiwanja cha kujenga fremu za biashara.

Sio kila fremu zilizopo barabarani zitapata wapangaji watarajiwa. Moja, zingatia fremu iwe barabarani. Pili, ni lazima iwe ni barabara ambayo inapitisha idadi kubwa ya watu.

Pia, zingatia muda ambao watu wanapita kwenye hiyo njia. Fremu ambayo ipo barabara ambayo watu hupita asubuhi, mchana na jioni huwa na thamani kubwa ukilinganisha na fremu ambayo watu hupita muda wa asubuhi pekee au usiku pekee.

Muhimu; Nishirikishe chochote kuhusu somo hili. Maoni, mapendekezo na ushauri vinakaribishwa. Nishirikishe muda huu, mambo ni mengi utasahau mawazo mazuri ulinayo.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Calls/WhatsApp; 0752 413 711
 
Sawa Mkuu
 
Back
Top Bottom