Sifa na Jinsi ya kujiunga na Duka la Posta Mtandao

Sifa na Jinsi ya kujiunga na Duka la Posta Mtandao

Arnold Kalikawe

Senior Member
Joined
Sep 28, 2016
Posts
152
Reaction score
374
Katika ulimwengu wa leo tumeshuhudia Teknolojia ikipamba moto, sambamba na hilo wafanyabiashara na watumiaji wa bidhaa za biashara wamekuwa wakitafuta namna bora ya kuuza na kuagiza bidhaa kwa njia ya mtandao. Kama tunavyoijua mitandao maarufu ya kuagiza bidhaa kama Alibaba, Amazon, Ebay na kadhalika. Shirika la Posta nao kwa kurahisha huduma ya usafirishaji wa Barua, na bidhaa mbalimbali wakitumia mfumo wa EMS (Express Mail Service) wa kusafirisha bidhaa kimataifa na duniani kote, sasa nao wameamua kuingia katika huduma ya kuratibu huduma za mauzo ya mitandao. Posta imeamua kuja na huduma ya Duka la mtandaoni kuwawezesha wauzaji kutangaza bidhaa zao na pia kuwawezesha wanunuaji au wateja wanaotaka kuagiza basi waagize kupitia duka la posta na kisha kusafirishiwa bidhaa zao mpaka kwenye maeneo wanayoishi.

Duka hili limeungwa na maelfu ya wajasiriamali na wafanyabiashara ambao tayari wanafanya mauzo yao Kupitia duka la Posta Mtandao linalopatikana Zaidi ya nchi 192 duniani:

SIFA ZA DUKA LA POSTA MTANDAO
  • Duka hili linasifika kwa kua hewani masaa yote
  • Duka hili lina lugha za mataifa mbalimbali duniani
  • Duka hili lina fedha za kigeni za mataifa mbalimbali
  • Duka hili lina usalama wakutosha
  • Duka hili kujisajili ni Bure kabisa
  • Duka hili linamuonekano wa kisasa kabisa kama yalivyo maduka mengine makubwa ya mtandaoni duniani.
  • Kila mjasiriamali atakua na Account yake ya duka, ambapo ataweza kuweka picha ya bidhaa zake pamoja na bei, pia ataweza kuona takwimu za mauzo yake, kujua bidhaa gani inapendwa zaid dukani kwake na Kuona Order yoyote itakayotokea.

Ili uweze kufunguliwa duka lako ni lazima uwe na vitu vifwatavyo na kuvituma kupitia email ya duka hili (onlineshoppingtpc@gmail.com)
  1. Uwe mtanzania (NIDA- National Identification Number)
  2. Leseni ya Biashara
  3. TIN namba
  4. Tax Clearance Form

Baada ya kutuma viambatanisho Tajwa apo juu duka lako litafunguliwa, endapo utafanikiwa kutuma viambata hivyo ndugu mjasiriamali, unashauriwa maswala yafuatayo ambayo ni ya Muhimu na yatakuongezea mauzo
  • Kuweka taarifa ya bidhaa yako ili wateja wapate kujua kuhusu bidhaa
  • Kuweka Picha nzuri za bidhaa ambazo ni Picha zenye mvuto na safi.
  • Kuwaeleza wateja wako kua sasa unapatikana katika duka la Posta mtandaoni na wanaweza kufikishiwa bidhaa zao Popote pale waliko ndani na nje ya nchi (Unaweza kuwapa link ya duka lako la mtandaoni.)
  • Kubadili taarifa za bidhaa zako mara kwa mara(Update)ili kuendana na wakati

KWA MASWALI NA MAULIZO WASILIANA NAO KUPITIA
Email: onlineshoppingtpc@gmail.com
 
Back
Top Bottom