Sifa nyingine ya Augustine Mahiga: Yeye ndiye "Shahidi Y" kwenye kesi ya Uhaini ya mwaka 1982/83

Sifa nyingine ya Augustine Mahiga: Yeye ndiye "Shahidi Y" kwenye kesi ya Uhaini ya mwaka 1982/83

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
13,417
Reaction score
23,310
Je, Augustine Mahiga ndiye "Shahidi X" kwenye kesi maarufu ya uhaini ya mwaka 1983?

Yasemekana alikuwa na kumbukumbu mujarab zilizowezesha kuwasambaratisha washtakiwa.

Kitabu cha Kesi ya Uhaini kilitoka mwaka 1985 kilichokuwa kimeandikwa na Marehemu Mnenge S. Suluja. Mhusika mkuu wa washtakiwa alikuwa Thomas Lugangira au ‘Uncle Tom’. Wenzake walikuwa ni Hatibu Gandi au ‘Hatty Mac Ghee’, Kapteni Mohammed Tamim, Kapteni Mbogoro, Kapteni Christopher Kadege, Luteni Badru Rwechungura Kajaja na Kapteni Mapunda.

Wengine walikuwa ni Banyikwa na mkewe, Christopher Ngaiza, Zacharia Hans Pope, Kapteni Rodrick Rosham Robert, na Eugene Maganga. Kingine kilichokuwa very interesting kwenye kesi ni baadhi ya wana usalama kutumia Alphabet kuji-indetify badala ya majina yao yaani walikuwa Mr. X Kama Mabere Marando, Dr. Hassy Kitine, na Mr Y Dr Augustine Mahiga, nadhani pamoja na Mizengo Pinda nk.

Washtakiwa 9 Kati ya 16 Walihukumiwa kifungo cha maisha. Na Jaji Nassoro Mzava. Mwaka 1993 Walitoka kwa Sababu ya Tanzania kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi hivyo wafugwa wa kisiasa walipaswa kutoka Lakini Hatty MCghee alitoka akiwa mahtuti na akafariki Hospital MCghee aliwahi kutoroka pamoja na Uncle Tom lakini akadakiwa Horohoro Tanga. Mawakili Waliotia Fora ni Hussein Muccadam(RIP) Murtaza Larkha, Jadeja Wote walikuwa wa Asia.
 
Stuxnet,

Kwa maoni yangu, upande wa UTETEZI ndiyo uliotia fora ukiongozwa na Wakili MURTAZA LAKHA.

Kwa kweli Murtaza Lakha alikuwa na maswali ya kuwachachafya sana mashahidi wa upande wa mashtaka.

Upande wa mashtaka ulikuwa na wakili anaitwa William Sekule ambaye alifanya kazi nzuri sana ktk kuhitimisha kesi na kuchambua ushahidi na kuuunganisha na washtakiwa.

cc Nguruvi3, Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom