Sifa nyingine ya Augustine Mahiga: Yeye ndiye "Shahidi Y" kwenye kesi ya Uhaini ya mwaka 1982/83

Usimuone vile vile zakaria hanspope ni mafia uyo
 
Sasa baba angu kumbe umekulia kwenye nyumba ya kizalendo kabisa, kwanini sasa unaungana na matapeli wa nchii na kujitahidi kuwapamba shida nini ? Njaaa au?
 
Hata Mkono ameshindwa kuvivaa viatu vyake KWELI ??

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Comrade upe tupe Hadithi za Comrade Dr Mahiga naimani unazo nyingi SANA Maana namkubali Sana huyu Dr
Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Juma Thomas Zangira alikuwa mtu wa intelligence miaka ya mwanzo ya Uhuru wetu wa Bendera, na alikuwa karibu sana na Oscar Kambona. Alikuja kufungwa baadae na alipotoka ndio akawa na kibarua pale Kilimanjaro Hotel enzi hizo.
Alihukumiwa kwa kesi ya espionage au uhaini, kwa makosa ya kuwasiliana, kukusanya taarifa za siri kati ya mwaka 1971-1977 na mzungu John Wilson kuhusu msimamo wa Tanzania ktk nchi za Rhodesia na mtazamo wa Nyerere ktk maswala ya uchumi wa nchi.

Huyo mzungu John Wilson alikuwa (alijifanya) mfanyabiasha. Hata hivyo hukumu yake ya miaka 20 jela ilitenguliwa na majaji Nyalali, Kisanga, Lugakingira wa Mahakama ya Rufaa hadi miaka 13. Sababu walishindwa kuproove kimaandishi maelezo aliyokuwa akimtumia huyo John Wilson. Zilipatikana barua za huyo mzungu tu wala si JWTZ. Na yeye alisema aliyokuwa akimwambia ni mambo ambayo hata vyombo vya habari magazeti, radio vilikuwa vikiripoti. Ukaonekana ni ushahidi then kifungo kikapungua ila alionekana ni tishio kwa usalama wa taifa, Tanzania law report 1980.
 
Natamani kujua ushiriki wa Hanspope katika tukio hili ila sijapata wa kunisimulia

Sent using Jamii Forums mobile app
Hans Pope (senior) alikuwa Regional Police Commander, Iringa, kabla ya kupelekwa Mkoa wa Ziwa Magharibi (West Lake Region) ambao sasa ni Kagera. Nakumbuka picha yake ilipochapishwa magazetini hapa nchini, 1972, baada ya kuuawa na askari wa Amin waliomteka Mutukula.

Katika picha ile, mwili wake ulivimba sana. Amin alisema jeshi letu lilikuwa na Wachina na Hans Pope ulikuwa ndiyo ushahidi huo. Hans Pope alikuwa na damu ya Kijerumani, siyo ya Kichaina, ingawa sura yake katika picha ile ilikuwa kama ya "Kichaina" kwa sababu ya kuvimba sana. Naikumbuka sana picha ile. Ilikuwa ukurasa wa kwanza magazetini.

Watoto wake ndiyo hao wawili Zacharia na Harry waliohusika na mpango wa kumpindua Nyerere, 1982, pamoja na wanajeshi wengine.

Zacharia alikuwa captain kikosi cha mabomu na Harry (RIP) alikuwa rubani wa Airwing. Walishawishiwa kuingia kwenye uhaini kwa hisia kuwa Nyerere kumsababisha kifo cha baba yao kwa kumpeleka kuwa RPC Wes Lake Region .
 
Shukrani,je kwa miaka ya sasa kwanini majaribio ya kumpindua raisi hayatokei,au watu wameridhika na Hali hii,nidhamu,au wanajeshi wa siku hizi wamepoa??
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukrani,je kwa miaka ya sasa kwanini majaribio ya kumpindua raisi hayatokei,au watu wameridhika na Hali hii,nidhamu,au wanajeshi wa siku hizi wamepoa??

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyakati zimebadilika halafu vyombo vya kimataifa kama UN na AU zikikuwekea vikwazo hufiki popote. Hata nchi za West Africa hususan Nigeria na Ghana ambazo zilikuwa na matukio mengi ya mapinduzi toka majeshini ziliacha before mid 1990s.

Pili demokrasia ya vyama vingi ikiheshimiwa ndiyo suluhisho la kuutoa utawala mbovu usiokidhi matarajio ya raia kwenye uongozi. Ndiyo maana tunawashangaa hawa akina Pole Pole na Bashiru Ally wanapomsaidia Magufuli kuuua UPINZANI kwa kununua wabunge au akina **** Nkamia wanaposhabikia kuongeza muda wa Rais kutawala.

Hawa wote inabidi tuwachukie kama ugonjwa wa COVID19 kwa kuwa wanatupeleka kwenye nyakati za giza
 
Okay
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…