Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,497
- 4,775
MOYO WA CHUMA.
1.Jina jipya tumepewa,Yanga tunaitwa chura
Hatuna tena ngekewa,Simba azidi parura
Ila kweli twaonewa,kisa twakosa ngawira
Kuishabikia Yanga,uwe na moyo wa nondo.
2.Ama kisa jezi zetu,rangi yake yachukiwa
Kilio Jangwani kwetu,magoli twashindiliwa
Yanga inaukurutu,inafaa kufuliwa
Kuishabikia Yanga,uwe na moyo wa nondo.
3.Kama tunabaguliwa,tunapocheza mpira
Chenga nyingi twazoliwa,zinatupoteza dira
Kipenga twapuliziwa,magoli hadi wazira
Kuishabikia Yanga,uwe na moyo wa nondo.
4.Jangwani ndo timu yetu, Japo Yanga tu wakiwa
Yeboyebo jina letu,jana lilisahuliwa
Tuacheni peke etu,majina tukitungiwa
Kuishabikia Yanga,uwe na moyo wa nondo.
5.Matobo twatunguliwa,na kupoteza majira
Manji anachunguliwa,Simba ataajiriwa
Yanga tunauguliwa,hadi tuwe matahira
Kuishabikia Yanga,uwe na moyo wa Nondo.
6.Ni kweli Yanga ni butu,kama tunavyodhaniwa
Hatunayo bulungutu,zamani tumeishiwa
Tulicheze makurutu,labda tutathaminiwa
Kuishabikia Yanga,uwe na moyo wa nondo.
SHAIRI- MOYO WA NONDO
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
1.Jina jipya tumepewa,Yanga tunaitwa chura
Hatuna tena ngekewa,Simba azidi parura
Ila kweli twaonewa,kisa twakosa ngawira
Kuishabikia Yanga,uwe na moyo wa nondo.
2.Ama kisa jezi zetu,rangi yake yachukiwa
Kilio Jangwani kwetu,magoli twashindiliwa
Yanga inaukurutu,inafaa kufuliwa
Kuishabikia Yanga,uwe na moyo wa nondo.
3.Kama tunabaguliwa,tunapocheza mpira
Chenga nyingi twazoliwa,zinatupoteza dira
Kipenga twapuliziwa,magoli hadi wazira
Kuishabikia Yanga,uwe na moyo wa nondo.
4.Jangwani ndo timu yetu, Japo Yanga tu wakiwa
Yeboyebo jina letu,jana lilisahuliwa
Tuacheni peke etu,majina tukitungiwa
Kuishabikia Yanga,uwe na moyo wa nondo.
5.Matobo twatunguliwa,na kupoteza majira
Manji anachunguliwa,Simba ataajiriwa
Yanga tunauguliwa,hadi tuwe matahira
Kuishabikia Yanga,uwe na moyo wa Nondo.
6.Ni kweli Yanga ni butu,kama tunavyodhaniwa
Hatunayo bulungutu,zamani tumeishiwa
Tulicheze makurutu,labda tutathaminiwa
Kuishabikia Yanga,uwe na moyo wa nondo.
SHAIRI- MOYO WA NONDO
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com