Kama ulipata Div One, two, three tafsiri yake ulikwenda kidato cha sita hivyo huna sifa za kuajiriwa kama form four, hivyo kuna wa kidato cha sita pia wanaajiriwa na kama ulikwenda kidato cha sita ukapata Div 1,2,3 bila shaka ulikwenda chuo kikuu hivyo huna sifa ya kuajiriwa kama form six maana unayo degree.
Sasa matangazo ya ajira yao inaajiri kidato cha nne,kidato cha sita na wenye elimu ya chuo kikuu hivyo omba kulingana na Elimu yako shindana na wa elimu yako usiwazibie riziki wenzako na Uache Majungu. Wewe unadegree halafu unataka uombe kama form four halafu ukifika kazini ujitambulishe unayo degree unataka kazi za watu wa form four afanye nani?
Wanaajiri watu kulingana na mahitaji yao siyo upendavyo wewe.
Majeshini wanazo Elimu zao hata kama hujui kusoma wanakufundisha kile kitu wanachoamini utakiweza wala Elimu ile siyo kama yetu ndiyo maana wao siyo kama sisi.