sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Nakumbuka niliwahi kwenda kituo cha polisi kwa kosa flani hivi dogo tu ila ghafla likakuzwa sana ionekane mimi ni muhalifu mkubwa, ni siku niliyojifunza waweza kuumwa kichwa usiku ukakamatwa kwa uzururaji ila polisi wakaikuza kesi iwe unachorea ramani majambazi, sasa kule kituoni huwa wanaandika makabila, mimi kwa asili ni mtu wa mkoa flani upo kwenye rada za matukio, yani hata sikuhojiwa vizuri maafande wakakadiria nimefanya tukio wakaanza kuambiana kabisa "kesho mahabusu wakija hili liwe la kwanza kupakiwa, hawa watu ndio zao" nashukuru mambo yalimalizika hapo hapo kituoni kitanzania.
Nakumbuka pia kuna kipindi niliwahi kweda mkoa flani kikazi sasa siku kabla ya kwenda mvua ilizinyeshea nguo, asubuhi imefika bado mbichi ikabidi ninyooshe suruali zangu za marinda na mashati, huko nilikofika watu walini kadiria ni msabato na ustaarabu wangu uliwafanya wanione kijana wa kuigwa, siku nilipoenda bar kupiga vyombo kesho yake kila kona swali lilikuwa "ni yeye kweli mliyemuona bar" ?
Nasikiaga nao waarabu wanapinga sana mambo ya kupewa roles za ugaidi kwenye muvi lakini huyohuyo anaepinga akiwekewa kitita acheze role ya Osama anaona cha kufia nini, hizi muvi nazo huwa zinajenga picha watu wa mataifa flan wana tabia flani kumbe wala si wote.