sifa za mahaba

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Posts
4,201
Reaction score
236
Nimechoka
Nawasili nipokeya
sibadili yako niya
tafadhali niridhiya
yangu haii nimechoka
Wangu moyo wanitanga
kwa surayo kutoenga
njoo mbiyo wa muanga
mwendaniyo nimechoka.
Nakwambiya la hakika
Nisikiya muhibuka
Naumiya kwa mashaka
kungojeya nimechoka.
Nakujuza si dhihaka
li aziza nakutaka
ukiweza nieleka
kujiliza nimechoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…