Mashaka Siwingwa
Member
- Jun 27, 2020
- 6
- 4
Na; Mashaka Siwingwa
Watu wengi sana wamekuwa wakiamua kufanya au kuanzisha biashara na kupanga malengo kwa biashara hizo. Hata hivyo, biashara hizo huanguka na kupotea kabisa kwa mtaji pasipo na kueleweka ile hali mtu huyu aliweka malengo na kuyasimamia. Lakini watu wengi wamekuwa wakisahau kama kuweka malengo peke yake siyo tatizo bali tatizo ni hayo malengo ni ya namna gani?
Makala hii itaangazia juu ya sifa kadhaa za malengo ya biashara au ya jambo lolote unaloamua kulifanya kwenye maisha yako. Ni imani yangu kwamba makala hii itakuwa msaada kwako wakati unaenda kuanzisha biashara na namna ambavyo malengo yako yanatakiwa kuwa. Karibu tujifunze pamoja.
Sifa ya kwanza ya malengo ya kibiashara ni kuwa mahususi, mahususi kwa maana kwamba nilazima yawe wazi kwa kile ambacho unataka kukifanya. Nilazima katika malengo uainishe unataka kufanya biashara au shughuli gani? Kama lengo ni kufanya biashara basi unapaswa kusema unataka biashara gani na ya kiwango gani.
Hapa namaanisha kwamba malengo hayapaswi kuwa ya kubahatisha bahatisha au yasiyoeleweka. Unapoweka malengo yanapaswa kugusa kile unachokifanya hata mtu mwingine anapoyasoma aweze kuyaelewa. Kwa mfano, unataka kufungua duka la vifaa vya ujenzi, malengo yako ni lazima uoneshe ni duka la vifaa vya ujenzi la namna gani unataka kufungua.
Duka lenye ukubwa kiasi gani na mtaji kiasi gani katika muda uliojiwekea. Lengo ni lazima litaje ukubwa na thamani ya duka unalolifungua na hatua za kulifungua. Kwa maana kuwa, unaweza kuwa na lengo kubwa la jumla ambalo ni kumiliki duka kubwa la vifaa vya ujenzi ndani ya miaka mitano. Lakini ukawa na malengo mahususi ambayo yataonyesha hatua za wewe kulimiliki duka hilo.
Namna utakavyoanza na kiasi cha mtaji utakachoanza nacho, namna utakavyoliendesha na namna litakavyokua likipanuka kila baada ya muda fulani.
Pili, malengo yako ni lazima yaweze kupimika. Ili kujua umefikia malengo ama la ni lazima lengo liweze kuonesha kipimo sahihi cha wewe kulitathimini. Kipimo kinaweza kuwa pesa au ukubwa. Kwa mfano unaweza kusema lengo ni kufungua duka la vifaa vya ujenzi lenye thamani ya shilingi milioni kumi ndani ya miaka mitano.
Hii inamaanisha kuwa baada ya miaka mitano utaweza kupima kama umefikia malengo uliyojiwekea. Kipimo cha malengo yako kitakuwa ni thamani ya duka lako kwa wakati huo. Malengo yasiyopimika yanakosa uelekeo na hayafai katika biashara, huwezi kujua kama unakua ama la, unapata hasara ama la, kwakuwa hakuna kipimo ulichojiwekea.
Kwa mfano, umesema unataka kufungua duka la vifaa vya ujenzi, kweli ukafungua lakini hujaweka kipimo cha kupima kama biashara yako inakua ama la. Lazima uweke malengo ambayo unaweza kuyapima baada ya muda fulani. Kipimo cha malengo kinaweza kuwa katika mfumo wowote, silazima kuwa pesa tu.
Kwa mfano, unaanzisha biashara ya kuuza maziwa unaweza kuweka malengo yakufikisha uuzaji wa lita mia tano ndani ya miaka miwili, unauza nguo unaweza kuweka uuzaji wa suruali mia moja ndani ya miezi sita. Namna ya kuyapima malengo yanategemea na aina ya biashara unayotaka kuifanya, kitu cha muhimu ni kwa malengo kuweza kupimika.
Sifa ya tatu ni malengo kuweza kufikika. Kufikika kwa malengo kunatokana na hali halisi ya biashara yako. Ni vizuri kuwa na malengo makubwa lakini kuweka malengo makubwa ambayo hayawezi kufikika kwa kuzingatia hali halisi kutakukatisha tamaa mapema na kukupunguzia kasi ya biashara.
Unaweza kuacha biashara kwa kudhani hupati faida kwa kuwa tu hujafikia malengo ambayo hayakuendana na uhalisia. Kwa mfano, unafungua banda la mama lishe halafu unaweka malengo ya kufungua hoteli ya kitalii ya nyota tano ndani ya miaka miwili.
Kwa hali ya kawaida na akili ya kawaida lengo hili ni gumu sana kufikika au halifikiki kabisa. Linawezekana likawa lengo lako na si vibaya kuwa na lengo kama hilo lakini unapaswa kuangalia hali halisi. Kama mambo yataenda vizuri utakuwa ukirekebisha malengo yako kadiri biashara yako inavyokuwa ikiendelea.
Lakini pia unaweza kuweka malengo makubwa huku ukizingatia muda kwa maana ya kuweka muda mrefu zaidi, muda wenye uhalisia. Mama lishe kuwa na lengo la kufungua hoteli ya kitalii ndani ya miaka kumi na tano inaweza kuwa kitu kigumu, muhimu ni kuhakikisha unakuwa na malengo mahususi ya muda mfupi.
Weka uhalisia katika biashara yako, malengo makubwa ambayo hayafikiki yanakuonesha namna ambavyo haupo makini. Kumbuka kwamba kufanya biashara ni jambo halisi na si ndoto. Kamwe usifananishe malengo na ndoto. Unaweza kuwa na ndoto kubwa lakini kuweza kuzifikia ndoto hizo ni lazima uwe na malengo ambayo utayatekeleza kwa awamu kulingana na uwezo wako na hali halisi ya wakati huo.
Sifa ya nne na ya mwisho ya malengo mazuri ni yale yenye kipimo cha muda maalum wa kuyafikia. Malengo yako ni lazima yaweke muda wa kuweza kuyatekeleza. Muda ni kitu muhimu sana katika kuweka malengo. Usipoweka muda katika malengo yako utashindwa kujipima na malengo yanaweza kubakia kuwa ndoto ambazo hazitekelezeki.
Lengo kuu unapaswa kulipa muda mrefu kidogo ambao kwa kawaida ni kuanzia miaka tatu mpaka kumi na malengo mahususi yanapaswa kuwa ya mwaka mmoja mmoja. Hapa namaanisha kuwa, lengo kuu ni wazo lako zima la biashara na namna ambavyo unataka biashara yako kuwa katika kipindi fulani.
Malengo mahususi ni hatua za kulifikia lengo kuu. Ni mabadiliko ambayo yanategemewa kuonekana katika biashara yako kila mwaka ili kuweza kufikia lengo kuu. Hii inatokana na ukweli kuwa huwezi kulifikia lengo kuu kwa mkupuo mmoja, hivyo unapaswa kufanya mambo hatua kwa hatua.

Upvote
2