Sifa za mfalme Juha

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Kwa waliosoma Tamthiliya ya Mfalme Juha (Farouk M Topan) nchi ilivyokuwa inaongozwa na sheria zake tukumbushane.

Kuhusu sheria .
Watoto wa bibi kizee walienda kuiba nyumba mbovu ikawaangukia ,bibi akaenda kushitaki kwanini nyumba iwe mbovu ,kesi ikapelekwa kwa mfalme ,mfalme akasema akamatwe fundi ,fundi alipokamatwa akasema waliokoroga zege walikoroga vibaya..waliokoroga zege wakaletwa ,wakasema wakati wanakoroga alipita jamaa mnene anayeitwa Bakari ,wakashangaa hadi maji yakazidi ,mfalme akasema aletwe Bakari ,akaulizwa kwanini unanenepa hadi watu wanakushangaa na kazi inaharibika ,adhabu yako ni kunyongwa ,kabla ya kunyongwa mwalimu wa bakari akatokea ,akasema jamani mimi ni mwalimu wa dini ,ukinyongwa peponi unakutana na raha ,ukiwaza tu kitu unaletewa ,kuna warembo wa kila aina, naomba mi ninyongwe niaba ya bakari nikale raha ,mfalme Juha kusikia hivo akajibu ,nimefanya mema kwenye hii nchi mi ndo nayestahili hiyo starehe naamuru ninyongwe kwa niaba ya bakari si mtu mwingine ,basi wakamnyonga Mfalme.

Mnayokumbuka mtaongezea kuhusu huyu mfalme anayetaka awe kiranja wa malaika
 
Mi ninachokumbuka Mfalme Juha alitaka mpaka mabinti mahari yao yapimwe kulingana na uzito wao!!
 
Tupieni pdf ya kitabu kizima watu tujisomee wenyewe hapa na wala siyo kutuhadithia wakati mnajua fika wengine wataongezea na yasiyokuwemo... maana sisi kizazi cha Android hatuna tunachokijua kwenye hili
 
Ingekuwa ndio sasa hiyo mahari yangu ungekoma
Nisingekoma, kwa maana pengine mahari yako tukikuweka kwenye mizani upande wa pili tunathaminisha na gunia la mahindi la kilo 55! [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
 
Mimi sikumbuki lolote, huenda memory yangu ina walakini au?
 
Nimecheka mpaka nimeonekana kituko aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…