Elections 2010 Sifa za ushindi wa JK

Elections 2010 Sifa za ushindi wa JK

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
11,662
Reaction score
6,888
Synovate siwaelewi kabisa kwa ili, naomba wana-JF mnisaidie! Wamesema asilimia 84 wana imani na JK, asilimia 78 JK ni mtendaji mzuri, halafu asilimia 61 watamchagua JK 31 Okt 2010.

Maswali: je, kama wenye imani na JK ni 84% na wanaomchagua JK ni 61%, kwa nini wale asilimia 23% ya wenye imani naye wasimchague? Je, kama wenye imani na JK ni 84%, halafu 78% wanaukubali utendaji wake basi kwa nini hao 6% wenye imani naye, hawakubali utendaji wake? Halafu 17% kati ya 78% wanaokubali utendaji wake, ni kwa nini hawatamchagua JK kuwa Rais?
 
daima mwongo hukamatwa kwa sentensi zake. REDET na Synovate ni taasisi maji taka zinazofanyia research zao mtaa wa Lumumba, kuna kajengo pale mkabala na lango la shule ya msingi mnazi mmoja.
I had great respect na synovate, lakini naiona ni taasisi isiyo na manufaa kabisa.
Hata kujumlisha na kutoa hawawezi??
 
Back
Top Bottom