Sifa za vyoo vya uswazi.

Sifa za vyoo vya uswazi.

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Pongezi kwa waanzilishi wa kampeni ya usichukulie poa Nyumba ni choo. imekuwa kama mazoea watu kutoyapa kipaumbele mambo yenye umuhimu kwenye maisha ya kila siku na kuona ni vitu tu vya kawaida ila ukweli ni kwamba tendo la kuenda haja ni la lazima na sio la hiyari. Kwa vile na Mimi nimetokea uswazi nimeona sio vibaya kushare sifa za vyoo vya uswazi na tabia za watumiaji wake.

1. kinatumiwa na familia zaidi ya tatu na kila familia ina wastani ya watu wa 4 jumla watu 12.

2. Kinakuwa akina bomba la maji ndani ukibanwa na haja unabeba maji kwenye kopo kwa ajili ya kujisafisha wewe ila sio kwa ajili ya kuacha choo kwenye mazingira ya usafi.

3. Sometimes choo kinageuka bafu kutokana na foleni kubwa ya kuoga majira ya asubuh na jioni.

4. Vingi ni vya shimo ukienda unaona level ya stock ilipofikia

5. Ni kawaida kukuta mzigo ujaflashiwa

6. Wanawake wanaongoza kukojoa pembeni ya tundu la choo kukwepa UTI.

7. Vinatoa harufu sana usipokuwa makini unaweza toka na harufu kwenye nguo zako.

8. Ustaarabu sifuri waweza kuta makohozi au matapishi

Kuishi kwenye mazingira kama haya ya choo ni heri ukachukua jembe lako ukajiendea zako porini ukamaliza haja zako. Tubadilike tutumie nguvu kubwa kwenye kujenga na kutunza vyoo kwenye mazingira ya usafi..

Usichukulie poa Nyumba ni choo.
 
..........................................................
 
9.mlango mbovu au hauna komeo(komeo ni mkono wako) au mlango haupo mbadala ni pazia/mkeka

Nawakilsha
Kajunjumele moja
 
Sijui ni mimi tu ndio inanitoke au la...

Tena ukute nyumba za kupanga kuna kina mama fulani hivi wadaku wanapenda kupikia karibu na choo kabisa[emoji849][emoji849]

Sasa mziki pale unaposhikwa na lile tumbo la gesi mzee, mana raha yake ni kupiga vitu kama Scania 113. Unaingia toi unajibana kchizi[emoji23][emoji23][emoji23]
 
urefu wa choo unategemea urefu wa mama mwenye nyumba
 
Sijui ni mimi tu ndio inanitoke au la...

Tena ukute nyumba za kupanga kuna kina mama fulani hivi wadaku wanapenda kupikia karibu na choo kabisa[emoji849][emoji849]

Sasa mziki pale unaposhikwa na lile tumbo la gesi mzee, mana raha yake ni kupiga vitu kama Scania 113. Unaingia toi unajibana kchizi[emoji23][emoji23][emoji23]
Hiyo situation ni hatari unaweza tamani kuweka ringtone kwenye simu ujifanye unapigiwa ili utoe kitu fasta.
 
Back
Top Bottom