Sifa za watu uliowazidi wasiotaka uendelee kufanikiwa

Sifa za watu uliowazidi wasiotaka uendelee kufanikiwa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
SIFA ZA WATU ULIOWAZIDI WASIOTAKA UFANIKIWE!

Anaandika Robert Heriel.

Leo sitaandika mambo mengi. Andiko hili litakusaidia kuwaelewa watu na kukufanya usiwe na Stress za kijinga.

Zifuatazo ni miongoni mwa sifa za watu uliowazidi.

1. Wanapenda kujilinganisha na wewe.
Ukiona unatabia ya kujilinganisha na watu wengine jua watu unaojilinganisha nao wamekuzidi. Saikolojia ya mwanadamu inafanya kazi Kwa namna hiyo. Anapenda kujilinganisha na waliomzidi.
Kimsingi wanakuwa wanashindana na wewe aidha direct or indirect way

Yani wanapenda umuone upo Sawa naye ilhali hampo Sawa.


2. Wanapenda Kukufuatilia na kujifanya wanakujua
Wakati wewe umesahau Jana ulikula nini, wanaokufuatilia wanakumbuka mpaka ulichokula juzi.
Watu uliowazidi wanatabia ya Kupenda kukufuatilia maisha yako,
i. Umevaa nini. Umerudia nguo, nguo uliyovaa inagharama gani n.k
ii. Unaishi wapi, ndani kwako kukoje, Mkeo au mumeo yukoje na anafanya nini?
N.k.

Kimsingi mtu uliyemzidi atataka Ajue maisha yako, yaani ukitaka taarifa zako zote basi nenda Kwa uliowazidi watakupatia detail zako zote.
Watakuweka kwenye vilinge na vijiwe vyao wakujadili mpaka ukome.

Majirani uliowazidi ndio wanakujua vizuri kuliko waliokuzidi. Jirani aliyekuzidi kwanza Hana time na wewe.

3. Wanapenda kukukatisha Tamaa.
Watu uliowazidi wengi wao utawajua Kwa sifa ya maneno Yao kuwa, hutaweza, hutofanikiwa.
Utasikia wakisema, hiyo biashara ni mbaya haina pesa. Ilhali yeye hajawahi kufanya hata biashara ya henge.
Huyo mwanamke/mwanaume hutofika naye popote ilhali yeye hata mchumba anayeeleweka hajapata achilia mbali ndoa.

Kozi gani hiyo au kazi gani hiyo haina hata pesa, ilhali kwenye ukoo wao karibu wote hakuna mwenye kazi yenye Mshahara wa kueleweka Kama hiyo kazi anayoidharau Ati usiifanye

Kiufupi Watu uliowazidi wanapenda kuwa sehemu ya washauri wako ili wakuangushe😀😀. Na wala sio ili wakufanikishe.
Kumbuka mtu aliyekuzidi nadra Sana kukupa ushauri Kwa sababu hajui mambo yako wala hafuatili mambo yako. Mara nyingi mpaka ukamuombe ushauri.
Ila uliowazidi Kwa vile wanakufuatilia ndio wanakuwa wakwanza kukupa ushauri bila hata kuwaomba.

4. Wanakuchukia bila ya kuwakosea chochote.
Labda kosa lako ni ulivyowazidii.
Yaani watu wengi uliowazidi sio ajabu wakawa na chuki na wewe kisirisiri au waziwazi.

5. Watasambaza habari za uzushi na mbayambaya Kwa watu.
Utasikia watakuambia; unaroho mbaya, hausaidii ndugu au wazazi wako utafikiri wao wanasaidia wazazi wao.
Labda Kwa vile walikuomba labda msaada wa TSH 100,000/= ukampa Tsh 50,000 bado watasema hukuwasaidia.

Watakuambia mafanikio uliyoyapata ni yakitapeli, ufisadi au ushirikina utafikiri wao hawakuwahi kwenda Kwa Waganga, tena wengi wao mpaka Chale wanazo.
Sema labda Kwa vile waganga waliokutana nao ni waganga WA mchongo.

Wengine watasema Mkeo anakuendesha kisa na mkasa hutaki Mkeo wamfanye Kama Mke WA Ukoo. Basi ilimradi.

6. Wanajihisi unawadharau.
Mtu aliyekuzidi hata ukimdharau yeye Hana shida Kwa sababu atakuchukulia unamatatizo ya Akili.
Lakini mtu uliyemzidi hata Kama hujamdharau ataona umemdharau Kwa sababu ya kujiona Duni au kutokujiamini.

7. Wanapenda kukuringishia
😀😀 Mtu uliyemzidi akibahatisha Jambo Fulani basi atafanya juu chini ajionyeshe kwako ili umuone, anakuringishia ati na yeye yumo au anaweza😂😂. Ukimpongeza atachukia 😀 yeye alitaka uponde au umkosoe Kama yeye anavyokukosoaga ili aone unamuonea wivu😂😂

8. Hupenda kusema bila yeye usingefika hapo Ulipo.
Mpaka mtu anatoa Kauli hiyo basi jua ushampiga Gap. Au upo mbioni kumpiga Gap yaani keshaona kuwa amekushindwa.
Mtu aliyekuzidi wala huo muda wa kusema hayo maneno kwako Hana.
Yaani Heshima na hadhi yake hazijengwi Kwa kukusema wewe.

Ila mtu uliyemzidi atataka naye aonekane naye yumo.

9. Hupenda kuona anaakili kukushinda sema tuu wewe unabahati.
😂😂 Mara nyingi watu uliowazidi wanatabia yakujiona ati wanaakili kukushinda.
Yaani ukiona unajiona unaakili kumshinda mtu aliye na pesa kukushinda, elimu kakushinda, mamlaka na hadhi kakushinda, familia Bora kakushinda. Jua umeshazidiwa.

Utasikia; yaani jamaa mjinga Sana, kajenga nyumba ya Ghorofa tatu badala angejenga nyumba ya kawaida alafu hiyo pesa nyingine akajenga nyumba ya kupangisha.
Au yaani kanunua Gari la gharama linalokula Mafuta wakati angewekeza alafu baada ya miaka mifano ndio anunue hiyo Gari😂😂
Basi ilimradi tuu!

10. Hukuangalia Kwa jicho la mkunjo na kubetua midomo.
😂😂 Ukipita Kanisani labda ni mwanamke au kwenye sherehe au kwenye shughuli yoyote ukawa umetupia mavazi ya maana ukawa umependeza, uliowazidi utaona namna wanavyokuangalia Kwa macho ya husda huku wamebetua midomo yao😀😀.
Mbona wakipita waliovaa kawaida haangalii hivyo😀 lakini wewe kuvaa Kwakwakwa zao na vazi la gharama imekuwa nongwa😉

11. Wanataka uishi Kama Malaika!
Watu uliowazidi wanataka ATI uwe kama Malaika. Ati usinywe pombe Sana, Usiwe Malaya, usivae nguo za uchi.
Yaani wanapenda kukuwekea visheria sheria Fulani hivi.

Ukifanya kosa kidogo watataka kanisani upewe adhabu au utengwe kabisa😂😂 usipopewa adhabu inakuwa gumzo.
Wakati wao wanafanya hayohayo.

Ukiwa Kama mpambanaji kamwe usihangaika na watu uliowazidi wao siku zote wapo kwaajili ya kukukatisha tamaa. Wapo Kwa ajili ya kutaka muwe sawa, hiyo ndio furaha Yao
Mara nyingi wapo kwaajili ya kutaka ushindwe.
Wanapokufuatilia Sana haimaanishi wanakufuatilia Kwa mazuri isipokuwa mabaya.

Zingatia, wapo ambao wamekuzidi lakini ujio wako kadiri wanavyokutathmini wanakuona Kama mtu ambaye utawapita.
Siku zote mtu unayemhofia hata kama umemzidi jua atakushinda tuu, ni suala la Muda. Hayo ndio huleta maofisini vita, fitna na mpaka ushirikina.

Kumbuka; wapo wachache uliowazidi ambao wanaroho njema, wao hanawa Baya na mtu. Hivyo kuwa Makini kwani Dalili na sifa za uliowazidi wenye roho Mbaya nimeshataja.

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es
 
Uliposema leo hutoandika mengi basi nikasema acha nisome, maaweeee!!!
 
SIFA ZA WATU ULIOWAZIDI WASIOTAKA UFANIKIWE!

Anaandika Robert Heriel.

Leo sitaandika mambo mengi. Andiko hili litakusaidia kuwaelewa watu na kukufanya usiwe na Stress za kijinga.
Huwa nakuelewa sana mzee baba nime comment kabla ya kusoma
 
Dawa yao ni moja tu. Don't hang up with them.

The lesser they know about you the better.
 
Mi nikishikaga pesa nakua sina hasira kabisa hata nikiskia Kuna watu wananisema vibaya huwa nanyamaza ila nikipigika nakua na hasira kinoma ukiniletea mazarau nakukata wenge chap tu

😀😀😀

Mimi nikikosa kichwani ndio kinauma.
 
Back
Top Bottom