View attachment 3695438
Ibada ya kumuaga marehemu Mzee Burudi Nabwera katika Kanisa la Friends Church, Lang’ata, Nairobi, Jumatano, Oktoba 21, imeibua mjadala wa kisiasa baada ya Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula kuondoka kanisani pindi tu Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna alipoitwa kuhutubia.
Tukio hilo limevutia hisia kwa sababu linajiri wakati ambapo tofauti za kisiasa kati ya viongozi hao zimekuwa zikijitokeza waziwazi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Mudavadi na Wetangula wamekuwa wakitilia shaka uwezo wa miungano mipya ya upinzani kushindana na Rais William Ruto, huku Sifuna akiendelea kuhamasisha uungwaji mkono wa vuguvugu la Linda Mwananchi.
Je, unadhani kuondoka kwao kulikuwa na ujumbe wa kisiasa?
Sifuna aliendelea na hotuba yake, akianza kwa kauli ya ucheshi, "This is Nairobi," iliyowafanya baadhi ya waombolezaji kucheka.
Ibada hiyo ilikuwa ya kumuaga Mwanadiplomasia mkongwe na aliyekuwa Waziri Burudi Nabwera, ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Lugari na balozi wa Kenya nchini Marekani.
Je, Mudavadi na Wetangula kuondoka wakati Sifuna anaitwa kuzungumza ni tukio la kawaida lisilopaswa kutafsiriwa kisiasa au linaonyesha jinsi tofauti za kisiasa zinavyoanza kuathiri hata mikusanyiko ya kijamii kama ibada za mazishi?