Narudia tena kuwa sioni kama kweli sura hizo zina ubavu wa ku-reform system iliyokwishajengeka ndani ya serikali hii ya Tanzania. sioni kama mmoja wao kati ya hao anayesubiriwa kuteuliwa kukiuza CCM kuwa anaouwezo wa kukemea uzembe wa baadhi ya watumishi wa umma, mwenye uwezo wa kukemea ufisadi uliokithiri ndani ya Tanzania hii! CCM wamejiloga wenyewe! kwangu mimi Magufuri ni WAZIRI MKUU au anafaa kuongoza wizara na si nchi. MIGIRO sioni hata kama anatosha ndani ya wizara achilia mbali nchi. Magufuri ni mtu wa maamuzi ya haraka haraka bila kutafakari kitakachotokea mbele baada ya maamuzi. Hata hivyo, sioni kama anao uwezo wa kuwakemea viongozi aliofanya nao kazi ndani ya serikali kwa muda mrefu sana. Naona sura ya kuwafumbia macho pindi watakapovurunda au hata kushiriki ufisadi. Niona sura ya kuwavumilia kina Simbachawene wanaojimilikisha mafuta na gesi kwa kupitisha miswada kwa dharura. SIIONI SURA YA KUKEMEA UFISADI KATI YA HIZO TATU BORA WALIZOLETA. Kwangu mimi labda angekuwa mzee wa busara MWANDOSYA! Kidogo huyo sura ya UONGOZI WA JUU KABISA ANAYO, kama ilivyo kwa Dr. Slaa, Walioba, A. Ramadhani. Hivyo kura yangu imebaki kwa Dr. Slaa endapo atapitishwa na upande wa pili.