SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,265
Nimesikia mara nyingi Spika au Mwenyekiti wa vikao vya Bunge akimwambia Mbunge: Kaa chini! Maneno haya yanasemwa kwa ukali kidogo kuonyesha uzito wa mamlaka alio nao spika au mwenyekiti. Sipendezwi hata kidogo na haya maneno na jinsi yanavyotolewa kwa sababu kwangu naona yamejaa aina fulani ya uvunjaji wa heshima kwa wabunge.Unapomwambia mtu 'kaa chini' ni pale mtu huyo anapokuwa amesimama sakafuni au kwenye udongo na unataka akae kwenye hiyo sakafu au udongo - ndio maana ya 'kaa chini!' Sasa mbunge mzima kasimama na pembeni mwake kuna kiti cha heshima cha kukalia unamwambia 'kaa chini!' una maana gani? Ningekuwa mbunge kisha nikaambiwa hivyo, ningepita viti vyote na kwenda kwenye ile nafasi isiyokuwa na kiti na kukaa sakafuni.Hiyo ndio maana ya 'kaa chini!' Lugha sahihi ni 'Mheshimiwa Mbunge keti.
Naichukia sana hii lugha ya 'kaa chini!'.Naona kama ina chembechembe za dharau/kutoheshimiana.
Wasemaje?
Naichukia sana hii lugha ya 'kaa chini!'.Naona kama ina chembechembe za dharau/kutoheshimiana.
Wasemaje?