Sijaandikiwa tarehe ya kurudi baada ya kupima UKIMWI

Sijaandikiwa tarehe ya kurudi baada ya kupima UKIMWI

ankol

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
2,355
Reaction score
4,260
Habarini wadau.

Hivi juzi nilienda angaza kupima Ukimwi. Majibu yakatoka nikaambiwa niko poa. Yaani negative.

Nilitoka na furaha sana. Kiasi cha kutouliza tarehe ya kurudi nilipewa kikadi changu.

Baada ya kufika nyumbani kukiangalia hakijaandikwa tarehe ya kurudi. Hii inamaanisha nini?

Najiuliza maswali mengi sana hapa. Mshauri alisahau kuniandikia tarehe ya kurudi?

Ushauri wadau maana naona stress zinaanza kurudi tena upya.
 
Rudi tena mkuu si umejitakia mwenyewe kujitesa?!
 
Imekuwa confirmed hawaoni sababu ya kurudia...
 
Bwana alitoa na bwana ametwaa.....Jina lake lihimidiwe......REST IN PEACE KAMANDA.....UTASHUHUDIA UKAWA WANACHUKUA NCHII UKIWA JUU MAWINGUNI.....
 
Sio lazima wanasema tu njoo baada ya miezi 3
 
Hapo ndugu yangu nenda kituo kingine ukapime.
 
Makosa yanatokea. Kaa miez mi3 pima tena japo Mara nyingine usipoandikiwa tarehe inamaanisha ni Positive..
 
Wamesaahau tu ndugu kwanza hongera kwa kutua zigo la stress ___________ Hakuna kitu kigum kama kuingia ile mahali daaaaaaa hongera sanaaa _____ Rudi kamwambie akuandikie vile vineno rudi japo ukweli waujua mwenyewe kwani baada ya vipimo kabla hujapewa awad / taji lako AKA majib kuna kaushauri kanahusikaga kabla unaanza kuhis ndio tayari nini ??? Kumbe kawaida tu ________ Mie nahis kupima skuiz unakuwa na tension zaidi ya job interview
 
Kumbuka kipimo hiki kinachotumika sasa ni tofauti na kile cha miaka ya kabla ya 2012
 
Basi tena tuandae magunia ya mpunga.
 
Angaza ilikufa siku nyingi sijui, Umepima mitaani kwa nani?
 
Back
Top Bottom