Habarini wadau.
Hivi juzi nilienda angaza kupima Ukimwi. Majibu yakatoka nikaambiwa niko poa. Yaani negative.
Nilitoka na furaha sana. Kiasi cha kutouliza tarehe ya kurudi nilipewa kikadi changu.
Baada ya kufika nyumbani kukiangalia hakijaandikwa tarehe ya kurudi. Hii inamaanisha nini?
Najiuliza maswali mengi sana hapa. Mshauri alisahau kuniandikia tarehe ya kurudi?
Ushauri wadau maana naona stress zinaanza kurudi tena upya.