shibela
JF-Expert Member
- Jul 3, 2018
- 1,068
- 3,507
Alfajiri ya Leo kwenye saa 11:30 hivi natoka nyumbani naenda kwenye mihangaiko yangu! Nilikuwa upande wa magari yanayorudi toka mjini! Upande wa magari yanayoenda mjini kulikuwa na msururu wa magari, gari ya mwisho ilivyomalizikia ghafla mbele yangu upande huo nikaona jeneza katikati ya Barabara nikafikicha macho labda sioni vizuri jamani ni jeneza kabisaa jeneza!!!na nilikuwa kwenye 40km/h yaani nimeona vizuri kabisa,Sasa sijaelewa lilikuwa linasafirishwa limedondoshwa kama limedondoshwa ina maana waliokuwa nalo hawajaona??? Sielewi nini kimetokea au kama kuna mtu alishawahi kukutana na situation kama hiyo wananzengo!!