sijaenda shule mpaka leo

mariam22

Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
9
Reaction score
1
Habari zenu wadau, mie nilichaguliwa kidato cha tano shule ya machame sasa mzazi wangu amejaribu kunitafutia uhamisho kwenda jagwani kwasababu ya afya yangu[nina pumu]na pia umbali wa shule , sasa ameenda wizarani mara ya tano sasa na kupeleka barua lakini hamna progress yeyote , na huko wizarani wamemwambia atajibiwa baada ya wiki moja na shule zimefunguliwa tangu tarehe 12 naomba ushauri wenu nifanye nini niende tu huko machame au nisubiri tena wiki mmoja
 

1st of,conglats 4 passing th exams nd 4 ur selection too! Cjajua umechaguliwa combo gan ila regardless ni Arts,business o science kuwa nyumbani mpaka mda huu ingali wenzako wanaendelea na masomo c hali nzuri!! Kama unaona afya yako haiwezi kabisa kukuruhusu kusoma ulipopangwa basi endelea kujaribu uhamisho,ila kama unaweza kwenda nakushauri nenda now,maana nilichogundua in Adv education katika shule za serikali shule haina influence yeyote na matokeo ya m2! Aliepata 1 akiwa kibaha atapata hiyo hiyo shule yeyote,na aliyepata 4 kwingine atapata hiyo hiyo hata kibaha!TRUST ME KWA GOV SCHOOLS,HIGH LEVEL NDO ILIVYO PIGA UA!!
 
Asante kwa ushauri wako , na pia nawaza labda nianze tution kwa sasa ili angalau niweze kwenda sawa na wenzangu waliopo shule
 
Nenda huko machame tu bi dada...tatzo lako unataka ubaki dar ili upate muda wa kujirusha!
 
Mariam22,hongera sana kwa kufaulu. Kwa mimi nakushauri nenda machame kwani hali ya hewa ya huko japo ni baridi lakini siyo kiivyo kwani wapo waliosoma wakiwa na pumu na waliweza. kwa wizarani kupata uhamisha utachelewa sana na unaweza usipate kabisa. wewe angalia unataka nini kwa sasa kisha muombe mungu akusaidie. Mambo mengine kama yanaonekana kuwa magumu yasikuumize kichwa.
 
Nenda huko machame tu bi dada...tatzo lako unataka ubaki dar ili upate muda wa kujirusha!
Hapana kaka sina nia hiyo ila tu nahofia kupata asthma attack nikiwa sehemu ya baridi na sina ndugu yeyote wakaribu machame
 
Hongera kwa kuchaguliwa kuendelea na masomo

Shughulikia uhamisho ukiwa shuleni..acha excuse binti...hakuna kama elimu siku hizi.

Nunua majaketi dress warm allthe time nenda kasome ,na ushughulikie uhamisho ukiwa unaendelea na masomo.
Unaweza toa excuse kwa ndugu ,jamaa na rafiki kuhusu kuchelewa kwako mwaka au kufeli ukaeleweka..ila system na dunia inavyokwenda haina excuse..careful.
 
Hapana kaka sina nia hiyo ila tu nahofia kupata asthma attack nikiwa sehemu ya baridi na sina ndugu yeyote wakaribu machame
ina maana maraim wewe ukipata nafasi ya kwenda kusoma ulaya kwenye baridi usikokuwa na ndugu hutaenda? Usipende kudeka nenda shule maisha ya home yapo tu. wala hufi kwa kwenda kusoa huko.
 
Hapana kaka sina nia hiyo ila tu nahofia kupata asthma attack nikiwa sehemu ya baridi na sina ndugu yeyote wakaribu machame

acha uoga bana mbona watu wanaenda ulaya na kunabaridi hatari,nenda machame dogo mi nitakuwa ndugu yako nitakuwa nakutembelea au hata grand ma wangu atakuwa anakuja.shule ipo sehemu bomba sana stand ya daladal na gate la sule ni mwendo wa dakika 1,shule ipo karibu na machame hosptal 1.5 km.usafr wa mo town upo wa kumwaga kuanzia 5am up to 6:30pm.karibu machame dogo acha kulea ugonjwa baridi sio kali sana wacha kusikiliza hadith za wabongo ukitoka bongo saa moja na dar ex au kilimanjar saa 9 au 10 utakuwa ushafka xul.
 
kwa mfumo wa serikali ni vigumu kupata uhamisho kabla ujaanza masomo hivyo nakushauri uende shule kwanza baada ya miezi sita ndo utapata uhamisha a lafu ushofu hali ya machame ni nzuri utaimudu
 
Asanteni wote kwa ushauri wenu , ni bora nikajaribu yakinishinda nitaomba uhamisho nawashukuru wote waliochagia nikifika shule nitawajulisha thanks
 
Asanteni wote kwa ushauri wenu , ni bora nikajaribu yakinishinda nitaomba uhamisho nawashukuru wote waliochagia nikifika shule nitawajulisha thanks

nikija moshi mwezi wa 7 ntakua mtu wako wa karibu mariam,thawa?
 
nikija moshi mwezi wa 7 ntakua mtu wako wa karibu mariam,thawa?
senetor mwache asome
Binti nenda kwanza machame ili uhamisho ukimalizika ndo utoke huko na kwenda na jangwani
 

Pole mdogo wangu,nakushauri uende tu Machame ukaanze huku mzazi anafuatilia uhamisho.Na pia unaweza kwenda kuongea na Mkuu wa shule ya Machame akakusaidia kupata uhamisho kwa haraka(anaweza kukuandikia barua ya kuthibitisha kwamba mazingira yamekushinda hvyo upatiwe uhamisho).Mambo ya serikali yanaenda taratibu dada!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…