Sijamuelewa kabisa huyu mwandishi wa Mwanasport

Sijamuelewa kabisa huyu mwandishi wa Mwanasport

Show Game

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
316
Reaction score
1,099
Kwenye ile gem ya Yanga vs al ahly, naona mwandishi anaandika eti Yanga amembana Al Ahly!

Aisee like seriously?

Hivi nani alipaswa kubanwa kati ya mwenyeji na mgeni? kiutaratibu wa kisoka..
Screenshot_20231205-110042.jpg
 
Ni sahihi aliyebanwa ni Al Ahly sio kwasababu uenyeji bali kwa angle ya ubora wa timu.
Al Ahly ni bingwa mtetezi na pia ni wa kwanza katika rank za ubora. Yanga alikuwa ni underdog kwa Al Ahly kwa kila angle. Ni sawa na Real Madrid akaenda kucheza na Wigani nyumbani kwake na kutoa sare. Je ni yupi atakuwa kabanwa?
 
Kwenye ile gem ya Yanga vs al ahly, naona mwandishi anaandika eti Yanga amembana Al Ahly!

Aisee like seriously?

Hivi nani alipaswa kubanwa kati ya mwenyeji na mgeni? kiutaratibu wa kisoka..View attachment 2833704
Kawaida. Wakati mwingine ni vigumu kuekewa akili kubwa kwa wewe mwenye akili ndigo, najua kadri ya muda unavyoenda utaelewa vizuri sana japo itachukua muda

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Kwenye ile gem ya Yanga vs al ahly, naona mwandishi anaandika eti Yanga amembana Al Ahly!

Aisee like seriously?

Hivi nani alipaswa kubanwa kati ya mwenyeji na mgeni? kiutaratibu wa kisoka..View attachment 2833704
Ni sahihi alivyoandika, maana Yanga ilitazamiwa zaidi kuja kupoteza mechi kuliko kupata sare au kushinda. Kitendo cha Yanga kupata sare ni sawa kabisa na kusema imeibana Ahly
 
Sehemu kubwa ya mchezo yanga ndiyo alikuwa anaongoza ku press Hata possession half time ilikuwa 54% yanga al ahly 46% .

Alivyotoka nzengeli ndiyo waarabu wakapata nafasi na kufanya counter kadhaa.
 
Ni sahihi alivyoandika, maana Yanga ilitazamiwa zaidi kuja kupoteza mechi kuliko kupata sare au kushinda. Kitendo cha Yanga kupata sare ni sawa kabisa na kusema imeibana Ahly
Ni dhana potofu kuwa ilitazamiwa Yanga afungwe. Zile zama za Waarabu kuziona timu zetu ni daraja zimekwisha sasa hivi tunatoana nao jasho. Japo kuwa mimi ni Simba lakini kabla ya ile mechi nilitazamia Yanga angemfunga Al Ahly.
 
Matazamio makubwa ya Al Ahly kushinda sio kwa sababu ya Uarabu wao, bali kwa sababu ya wastani mzuri wa muendelezo (consistence) ya matokeo yao ya hivi karibuni. Wazee wa kuweka mzigo hapa wanaelewa vizuri. Hata katika predictions za betting, probability kubwa ilikuwa ni Ahly kushinda

1701854339661.png
 
Back
Top Bottom