Sijaona Mwanamke aliyenifaa..... Afunga ndoa akiwa na miaka 99

Gagurito

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Posts
5,600
Reaction score
806
wadau wa Jf mambo vp? Kuna bwana anaitwa Gilbert Raia wa marekani mwenye miaka 99 ameishangaza dunia kwa kuoa mara yakwanza akiwa na umri wa miaka 99. Mzee huyo alikuwa mwanajeshi wa marekani aliyepigana vita ya pili ya dunia. Amemuoa mama mjane kikongwe mwenzake wa miaka miaka 86, wote wakiwa hawana uwezo wa kutembea zaidi ya kutegemea wheelchair. Alipo ulizwa na waandishi wa habari ni kwa nin ameoa akiwa na umri huo mzee huyo alijubu kuwa "KTK MAISHA YAKE HAJAWAHI KUMPATA MWANAMKE MWENYE MAPENZI YA DHATI, MWANAMKE WA AINA YAKE, AMENGOJEA KWA MUDA MREFU KUMPATA MWENYE MAPENZI YA KWELI, CHAGUO LA MOYO WAKE. AMEOA KWA KUWA HUYO MKEWE (Kikongwe wa 86yrs) ANAMAPENZI YA DHATI KWAKE!"

Mmh wataalamu wa mapenzi na ushauri nasaha wa MMU mwasemaje kuhusu hilo?
 
thats greatttt
du kumbe wake wa kuoa walipotea tangu 1940s?

siku izi magumash ndo weng...
 
Amen...mfano unaoishi kwamba mapenzi na ndoa yanawezekana pasina tendo la ndoa?
 
Msimamo dot com. Sasa kama hawawezi kutembea........mmmh!!! Staki hata kushangaa!!
 
Msimamo dot com. Sasa kama hawawezi kutembea........mmmh!!! Staki hata kushangaa!!
Mzee alikua ni afande ktk jeshi la marekani teh! Miaka 99 duh!
 
Alikuwa anatafuta the perfect one, ambaye naweza kusema hayupo kwa kweli! Usijashangaa, baada ya muda ukasikia divorce ya babu na bibi...mhhhh!!!
 
Alikuwa anatafuta the perfect one, ambaye naweza kusema hayupo kwa kweli! Usijashangaa, baada ya muda ukasikia divorce ya babu na bibi...mhhhh!!!
Teh! Do wish this to happen to you?
 
mi siwashangai hao maana na mm nahis nitaolewa nikiwa mzee maana sijamuona wa kwel mpaka sasa
 
Nyingine nimeishuhudia jana kipindi cha chereko TBC,mzee wa miaka 94 na bibi wa miaka 80,mzee ni mwanasheria wa shirika la reli na mkewe bado ni mwanafunzi anachukua masters UDOM,safi saaana!
 
Nyingine nimeishuhudia jana kipindi cha chereko TBC,mzee wa miaka 94 na bibi wa miaka 80,mzee ni mwanasheria wa shirika la reli na mkewe bado ni mwanafunzi anachukua masters UDOM,safi saaana!
Duh! Hii kali mkubwa!
 
babu akaamua kuchukua kifaa chake cha miaka 86 teh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…