Sijapata kazi hata ya kujitolea tangu nimalize chuo, nifanyaje!

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Salaamu kwanza nianze kujitetea katika makosa ya uandishi sababu ni kwamba natumia simu ndogo nashindwa kuweka aya vizuri! Hivyo basi tuvumiliane na nitaandika kwa kifupi. Mimi ni muhitimu wa ngazi ya shahada X katika chuo X tangu nimalize mwaka 2021 sijawahi kupata kufanya kazi kokote hata kujitolea, nimejaribu kutuma CV zangu holaa!!.

Maisha yangu hayaeleweki hata kidogo sina future kwa pesa nayoipata kwenye vibiashara na vibarua navyopata ila nimebakiwa na malengo tu. Kufupisha stori, nilishawahi kwenda kwa mganga before graduation sababu niliumwa ugonjwa wa kiswahili sasa ilitokea nikafanyiwa ramli na nikaambiwa ninalo jini la uganga hivyo sitafanya kazi zaidi ya hiyo.!

Nimeomba sana hola japo wkt mwengine nakata tamaa ila nafsi inanikutanisha na marafiki ambao wamepata kazi basi naona wivu nami najipiga moyo konde nitashinda japo sijui exactly ni lini!!

Nifanyaje?
 
Ushaanza kuamini shirki hapo utapambana na hali yako.
 
Toka nilivyopona si siri kumenifanya niwe hvyo wkt sikuwa hvyo, zaidi napoishi sasahivi ndiyo stori zao.
 
bfbfc598-a211-40f9-94ae-b5e623f806e1.jpg
 
Nimeandka uzi kwa lengo safi na nilichokiandk ni sahihi kote.sina elimu ya diploma ila ni degree mwaka 2021
 
Salaamu kwanza nianze kujitetea katika makosa ya uandishi sababu ni kwamba natumia simu ndogo nashindwa kuweka aya vizuri! Hivyo basi tuvumiliane na nitaandika kwa kifupi. Mimi ni muhitimu wa ngazi ya shahada X katika chuo X tangu nimalize mwaka 2021 sijawahi kupata kufanya kazi kokote hata kujitolea, nimejaribu kutuma CV zangu holaa!!.

Maisha yangu hayaeleweki hata kidogo sina future kwa pesa nayoipata kwenye vibiashara na vibarua navyopata ila nimebakiwa na malengo tu. Kufupisha stori, nilishawahi kwenda kwa mganga before graduation sababu niliumwa ugonjwa wa kiswahili sasa ilitokea nikafanyiwa ramli na nikaambiwa ninalo jini la uganga hivyo sitafanya kazi zaidi ya hiyo.!

Nimeomba sana hola japo wkt mwengine nakata tamaa ila nafsi inanikutanisha na marafiki ambao wamepata kazi basi naona wivu nami najipiga moyo konde nitashinda japo sijui exactly ni lini!!

Nifanyaje?
Ndugu,

Wewe hutafuti KAZI, unatafuta AJIRA,

Ajira ni chache, KAZI ni nyingi. Amka asubuhi, tembea tembea, ukikuta foreman anaajiri vibarua jiandikishe,

Piga KAZI, ukitoka, vaa smart ,Rudi nyumbani Ukiwa na chochote kitu,

Ukifanya KAZI za kawaida Kwa uaminifu, utapata connection Kwa wasimamizi Hadi Kwa bosses,

Ukipata appointment nao, toa vyeti vyako, utapanda kuanzia hapo.

Ni dhambi Mwanaume kulalamika kuwa hakuna Ajira wakati KAZI zipo nyingi.
 
Back
Top Bottom