Ramea
JF-Expert Member
- Mar 19, 2015
- 2,146
- 4,084
Beberu ni Mbuzi dume, hii ni tafsiri sawia kwa Mtanzania wa kawaida wa kule Nyololo na Nanjilinji. Sifa kubwa ya beberu huyu, ni kupiga kelele usiku kucha, kunusa mikojo ya majike zizini na kuwa na harufu kali ya mwili.
Kuna beberu yule wa kikoloni, wakoloni katika hatua ya juu ya ubepari wao, waliitwa mabeberu. Hawa ndiyo ambao walikuwa maadui wa nchi za kiafrika hadi kipindi Cha uhuru miaka ya 1960's.
Ingawa uadui huo uligeuka kuwa urafiki baada ya uhuru na hasa baada ya kuanguka kwa Soviet Union. Nchi nyingi ziliendelea kuwa na urafiki na watawala wao chini ya miavuli Kama ya Francophone states zilizokuwa chini ya wafaransa na nchi nyingine chini ya jumuia ya madola, kwa makoloni ya kiingereza.
Turudi kwenye mada, adui na agenda kuu ya Tanzania yetu sasa hivi ni "ubeberu" tulianza na uchochezi na uzalendo Kama defensive mechanism. Vikashindwa ingawa wachochezi na wakosa uzalendo wameteseka na pengine kufungwa na kupotea kusikojulikana.
Najaribu kujiuliza, kwanini utitiri wa kuchukua fomu ya Urais Zanzibar usiangaliwe kama Kuna mkono wa Mabeberu Kama ilivyo agenda kuu Tanzania Bara? Kwanini tusiwaite wachochezi watia nia wa Urais wa Zanzibar? Kwanini tusiwaone kuwa wakosa uzalendo? Najaribu kuwaza kwa sauti.
Nadhani Mabeberu wa Tanzania Bara ni wazungu, wakati mabeberu wa Zanzibar ni Mbuzi dume, Yule anayenusa mikojo ya majike na kunuka mwili.