Sijavutiwa na Toyota Harrier a.k.a Tako la Nyani

Kwenye Brevis nakuunga mkono hata mie nimetumia magari aina nyingi mpaka range ila Huwa naimiss sana brevis najikusanya nitafute ikae nyumbani iwe ya kuzugia siku Moja moja
 
Last week nimeendesha BMW X3,

Alaaniwe aliyeanzisha ku agiza Toyota nchi hii, kwa wenzetu zambia, kenya, Uganda, botswana BMW, subaru,WV na mercedez ni magari yaliyozoeleka sana tu na spare ziko za kutosha.

Taste ya BMW ni tofauti sana, gari ni nzito sana, ukitembea na 140 ni kama uko 80, inakuangalia tu upige kibati utakavyo na haiyumbi, hata ukipishana na roli husikii kupepesuka.

Security ya gari hata ukila hii mizinga midogo midogo angalau ni guaranteed kuliko uwe kwenye hizi harrier zetu.

Inataka uwe na service ya vitu genuine, Hydrolic oil yake ltr 1 inauzwa 45k hadi 50..yote kwa yote ni gari poa sana ukiwa na familia na trip za mikoani.
 
Umesahau kusema kitu hiki ambacho kila Mjerumani mweusi hua anakiimba:

'Bmw/Benz ina milango mizito ukiufungua/ukifunga mlango wake utausikia tu ulivyo mzito' 😄😄😄
 
serikali yako ndio iliyoupa promo toyota
 
Umesahau kusema kitu hiki ambacho kila Mjerumani mweusi hua anakiimba:

'Bmw/Benz ina milango mizito ukiufungua/ukifunga mlango wake utausikia tu ulivyo mzito' 😄😄😄
Umesahau kusema kitu hiki ambacho kila Mjerumani mweusi hua anakiimba:

'Bmw/Benz ina milango mizito ukiufungua/ukifunga mlango wake utausikia tu ulivyo mzito' 😄😄😄
Hahahahahah kwani ni uongo mkuu?
 
Natamani siku moja uendeshe Subaru forester XT, iliyowekewa recommended engine oil, halafu weka petrol ya TOTAL, PUMA au VIVO. Then njoo hapa utoe mrejesho.
 
Natamani siku moja uendeshe Subaru forester XT, iliyowekewa recommended engine oil, halafu weka petrol ya TOTAL, PUMA au VIVO. Then njoo hapa utoe mrejesho.
Tupe uzoefu wako Mkuu na forester XT
 
Tupe uzoefu wako Mkuu na forester XT
Hizi gari ni nzuri Tu tena saana hasa kwenye performance ukilinganisha na TOYOTA RAV4, harrier, na hata vanguard, hata nissan dualis, Xtrail na SUV nyingine nyingi Tu ambazo unaweza zilinganisha na forest XT. Shida ya watanzania wengi bado wanamawazo mgando kwamba Toyota ndio ya kuwa nayo kutokana na mazingira yetu ya kibongo ( unaweza kuwa kweli to some extent). Mm natumia forester almost 10 yrs na sijawahi pata shida yoyote kubwa kwenye engine, ni vifaa vidogo vidogo Tu. Spears za forester zipo nyingi Tu japo zipo slightly higher than Toyota. Ila ukifunga kifaa cha forester unaweza kaa nacho Hadi unauza gari. Mafundi wapo wazuri Tu na kama kunachangamoto wanauwezo mkubwa wa kufix na kutatua shida zote kwenye gari. Ukimiliki hii ndinga usitumie oil ambazo sio recommended, nahisi ni pamoja na gear box oil, steering fluid na hata break fluid. Hakikisha unatumia mafuta ambayo yamependekezwa na lazima yawe 5w-30 synthetic. Ukitumia ya Subaru wenyewe inakuwa poa zaidi. Haya petrol pia kuna baadhi ya kampuni ukiweka gari haichanganyi haraka, weka petrol ya TOTAL, hii ni nzuri sana na ukiweka utapona gari inachomoka faster, petrol nyingine nzuri ni VIVO na PUMA. Changamoto ya hii gari naona ni fuel consumption japo pale kwenye dashboard anarange 9km/L Hadi 10km/L. Ila kuna za 2WD nasikia zinatumia mafuta kidogo zaidi shida Tu ni kwamba sio AWD/4WD.
 
Ila tuache uongo huwezi kulinganisha Germany machines na Mjapan. The only category Japanese cars are the best is reliability, otherwise zimezidiwa kila mahali

Fuel consumption, resale value pia hasa kwa upande wa Toyota
 

Likianza kuwasha mti Xmas [emoji319] kwenye dashboard halafu una hela kuunga unga lazima utakumbuka harrier tu
 
Hizo changamoto ulizoorodhesha ndio zinazopelekea Toyota kupendwa, mtu yupo nanyamba hiyo total, sijui oil ya 5w-30 unazitoa wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…